Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Kwenu Masheikh na wahadhiri wetu Nawasalimien Assalam Aleikum. Jana mmefanya press conference, mmezungumza na kutoa kauli yenu kuhusu hatua ya Sheikh Ponda kusimama na kuwataka Waislamu na wananchi wamchague mheshimiwa Lissu katika uchaguzi huu. Mmepinga vikali kauli yake kuwa Waislamu wamekubaliana kumchagua Ndugu Lissu katika uchaguzi huu, naomba niwakumbushe yafuatayo. 1. Je, mnafahamu kuwa kuna waraka wa shura ya maimamu unaoelezea mtu gani anafaa kuchaguliwa? Kabla hamjamuita Sheikh Ponda muongo kwamba eti waislamu hawana makubaliano juu ya mtu gani wa kumchagua, ningependa muurejee waraka wa majuzi wa shura ya maimamu, umetoa orodha ya Sifa nyingi sana za mtu anayefaa kuchaguliwa sifa mojawapo awe mtu anayependa HAKI. Sasa nyie Masheikh wetu hebu tuambieni, kama kwenye waraka wa Shura maimamu wamekemea suala la kutokuwepo kwa haki nchini katika utawala huu wa rais Magufuli, hapo Shura ya Maimamu ina maana gani inaposema waislamu wachague mtu wa HAKI?, Kiufupi shura inaelezea kuhusu kubadili utawala kwenye uchaguzi huu na hicho ndicho Sheikh Ponda anachokifanya sasa hivi, Yaani kujaribu kusimamia azimio la Shura la kuondoa utawala wa dhulma na kuleta nchini utawala wa HAKI. Waislamu tunasimama na wapenda haki wote nchini bila kujali dini zao. 2. Wahadhiri na Masheikh wetu mmeonyesha double standard Kwenye hiyo press conference mliyofanya hapo jana, mlikuwa chumba kimoja na Masheikh wanaoipigia kampeni CCM waziwazi, mlikuwa na Alhadi (huyu siyo sheikh anyway ni mjanjamjanja tu aliyesoma dini), Pia alikuwepo Sheikh Majini, wote hawa wameipigia kampeni CCM waziwazi, Tena huyo Alhadi amefanya kufuru kubwa kwa kuomba kwa jina la asiye ALLAH, na mnafahamu Qur'an imefundisha nini kuhusu wale wafanyao shirki wana hukumu gani mbele ya ALLAH. Kwenye hiyo press conference nilitegemea Ustaadh Mazinge umpe kwanza huyo Alhadi vifungu vya Bible na Qur'an kuonyesha kuwa amekosea kwa sababu wewe ni mtaalamu wa elimu ya Comparative religions (yaani malinganisho ya dini mbalimbali kwa kutumia vitabu vyao) na tunakupenda na kukuheshimu sana kwa kazi uliyoifanya kwa Takriban zaidi ya miaka 25 sasa. Tulitegemea umuambie Alhadi auombe radhi umma wa Waislamu kwa kuidunisha dini yetu, wakati inapaswa iwe juu na kusiwepo kuchanganya haki na batili hata kidog katika dini. Sasa utamnyoosheaje Kidole Ponda wakati pembeni yenu wamekaa wakosaji wa wazi? 3. Waislamu tunaumizwa sana na Masheikh wetu walioko jela kiuonevu Leo hii sisi ni wakiwa, Masheikh wetu wako jela, wako jela Dar, Arusha, Mtwara, wako Jela kila mahali. Sisi waumini tunaumia, nyoyo zetu zimepigwa ganzi, tumejishika tama, tunahuzunika sana. Ni nani atakayetufundisha neno la ALLAH, ni nani atakayetupa faraja ya mtume wetu, ni nani atakayetufundisha mema tupate faida za duniani na mbinguni kama siyo Masheikh wetu walio jela?. Wamewekwa ndani na serikali ya CCM, wananyakuliwa mmoja mmoja kama mwewe anyakuavyo kifaranga na kuswekwa ndani. Sasa kweli nyie wahadhiri Mnamnyooshea kidole Ponda mtu anayetaka aingie madarakani mtu wa HAKI ili awatoe jela Masheikh wetu?. Uislamu umefundisha, ukiona Jambo baya liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea, na ukishindwa hata kukemea basi chukia, ila hiyo option ya mwisho ni udhaifu wa Imani. Hebu nyie wahadhiri wetu mnaomnyooshea kidole Sheikh Ponda leo, Mmekemea lini mbele ya hadhara ya Watanzania suala la Masheikh wetu kukaa ndani bila haki? 4. Sheikh Ponda yuko sahihi, hatua yake ni kwa maslahi ya umma wa kiislamu Katika nchi hii vyama vya siasa, chaguzi na haki za kikatiba ni vitu halali na vya kisheria. Ni mfumo wa kubadili uongozi ili kila mtu au kundi fulani la jamii kuweka utawala ambao wanahisi watanufaika au kupata ahueni, fursa na manufaa fulanifulani. Napenda kuwafahamisha wahadhiri wetu kuwa kumekuwepo kilio katika jumuia za kiislamu kuhusu Udini wa wazi katika awamu hii, Shura ya maimamu ilitoa waraka wenye kuonyesha kisayansi kabisa teuzi zilizofanywa na awamu hii zinavyonuka udini. Teuzi zimelalia upande wa imani moja mpaka aibu almost kwa uwiano wa 80:20. Haya kwanza kabisa aliyakemea Sheikh Khalifa na baadae Shura ya maimamu ikatoa waraka mzito, wa kishujaa na wa kukumbukwa juu ya jambo hili. Sasa kwa ubaguzi huu wa dhahiri kabisa usio na aibu nyie wahadhiri wetu mnaanza kumpiga mishale mtu ambaye anatumia taratibu halali zilizoko nchini ili kusimika utawala utakaotenda haki kwa wote? Hatua anayoichukua leo Sheikh Ponda ni hatua kama ambazo Masheikh wetu walichukua kumsaidia Nyerere ili kumtoa mkoloni ili kusimika utawala mpya utakaoheshimu maslahi yao na haki yao. Sheikh Ponda hana tofauti na masheikh akina Tambaza, Ramia, Chaurembo na wengineo waliosimama bega kwa bega na Nyerere kung'oa utawala dhalimu na kuleta utawala wa haki. 5. Masheikh na wahadhiri wetu tunaomba mtuache, tarehe 28 tuna jambo letu Dhulma huondolewa kwa mkono na kauli. Kauli yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU na mkono wetu ni Kura zetu. Tunawaomba wahadhiri wetu mtuache, hii ni nafasi adimu na adhimu ya kuondoa Dhulma na Uonevu katika nchi. Huyu Tundu Lissu anayetetea haki zetu Si Muislamu lakini ni Mtu wa Haki, huyu hana tofauti na Annajaashi (King Negus of the ancient Ethiopia), alikuwa ni Mfalme Mkiristo lakini mpenda Haki na muadilifu, huyu ndiye aliyeunusuru Uislamu na Waislamu kwa kuwapa hifadhi katika himaya yake wanafunzi wa mtume waliokimbia mateso na manyanyaso ya wapagani wa Makka. Tundu Lissu ni mkiristo mpenda haki, huyu ndiye anayetufaa na siyo yule ambaye hatupi nafasi za kutosha kwenye serikali yake halafu anatuhadaa kutujengea misikiti, lini sisi tumewahi kuwa na shida ya kujengewa msikiti na mtawala?. Sisi Shida yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU! Mwisho kabisa nitoe nasaha kwa Watanzania wenzangu Hatua ya Sheikh Ponda ni hatua ya kizalendo sana, Si hatua ya Udini hata kidogo, Maana kama Ponda angekuwa mdini maana yake angemuunga mkono Hashim Rungwe au Lipumba ambao ni waislamu wenzie. Ponda kamuunga mkono Lissu ambaye yeye Lissu na Magufuli ni wa Imani moja na dhehebu moja ila tofauti yao kuu ni kuwa Lissu ni mtu wa Haki wakati Mgombea wa CCM si mtu wa haki hata kidogo (Ana double standard na ndimi mbili). Tuungane kumuweka Lissu madarakani ili atuondolee dhulma ya kutisha katika nchi!
 
Nasubiri tamko kutoka kwa Maaskofu wangu wa Katoliki kuhusu kumtenga na kutomchagua yule mgombea mkatoliki aliyeahidi hadharani kuoa mke wa pili kinyume kabisa na utaratibu wa Kanisa letu linalo amini uwepo wa ndoa ya mke mmoja tu!
Ni yule aliye ahidi kumwoza mama yake mzazi kwa mtu aliyempa jogoo?
 
Mtu anyependa haki anatukana wazee kuwa ni professorial rubush, anashiriki ndege na mali za nchi zikamatwe, anashiriki kwa wezi wa madini yetu, anashiriki nchi isipate misaada muhimu, anadharau kwa watu wengine na kujiona yeye ni msomi kuliko wengine, anataka kujitenga na zanziba, aliyemtukana babawa taiga na kumzodoa.

Anapendelea ndoa ya jinsia moja.

Je, huyo ndi mnamtaka?
Vipi kuhusu anayebagua wananchi wake kwa kutopeleka miradi yamaendeleo kwenye majimbo ya wapinzani?
 
Aliyewafunga masheikh ni muislamu mwezako ambaye alipigiwa kura na waislamu kwa kuambiwa na Sheikh Ponda,sasa Sheikh Ponda anakuja tena kutuambia tumchague mtu mwengine ila safari hii anayetuambia tumchague ni kafiri.

Sasa hapo ndio najiuliza huyu kafiri ana nini hadi sie waislamu tumchague? maana huyu kafiri ni kama walivyo wanasiasa wengine tu wengi wanafki na hana tofauti na hao.

Huyu kafiri Lissu alituambia kuwa Lowassa ni fisadi ila baadaye anakuja kusema Lowassa sio fisadi na ndio maana hajashtakiwa alikula matapishi yake,sasa inakuaje Sheikh Ponda atuchagulie mtu mnafki kama huyu?ataweza kweli kutekeleza hiyo ahadi aliyoitoa kwa waislamu na huu unafki wake?

Huyu Lissu alisema ACT si chama cha upinzani kwamba kinatumika na serikali kuvuruga upinzani na akamtaja hadi Zitto kabwe kuwa anatumika na serikali hivyo si mpinzani,ila leo Lissu anashirikiana na ACT wakati alishasema kuwa hicho si chama cha upinzani bali kipo hapo kuuwa upinzani.

Sasa mtu kama huyo sie waislamu tumchague wa nini?

Tukusikilize wewe ,tumpigie kura Magufuli tuendelee kuyapata haya mateso au tumsikilize Sheikh Ponda tumchaguwe Lisu aliyeahidi kuyaondosha madhila haya?
 
Attachments

  • VID-20201021-WA0000.mp4
    18 MB
Kwani Sheikh Ponda wakati anawaambia mumpigie kura Kikwete yeye hakuwa anajua hayo masuala ya tume ya uchaguzi au kipindi hicho tume ilikuwa inatenda haki?

Sheikh Ponda pamoja na nyie mlishiriki katika kuweka utawala wa ccm 2010 na wakati watu wamekuwa wakilalamikia hiyo serikali ya ccm kutotenda haki,malipo yake wanayalipa masheikh wa uamsho sasa hivi.

Mie huwa sipigi kabisa kura wala kushabikia chama chochote na sio msukule wa huyo Sheikh Ponda.

Kutokupiga kura ndio unawarahisishia kazi hao unaojifanya kusema ni madhalimu
 
Attachments

  • VID-20201021-WA0014.mp4
    5.2 MB
Siasa ipi unayotaka kutuambia , au ya kuwaweka hawa aliotudhulumu muda mrefu ??? Ndugu zetu wako majela kwa makosa ya kubambikiziwa na Majambazi hawa , unataka tujikalie kimya ??
Ushawahi kuwa na ushahidi halisi wa hayo unayoyasema, mbali na kusikiliza mtandaoni?

Aina hii ya siasa ya kuzuliana majukwaani, kupakaziana uzushi Uislamu hairuhusu kwani inapiga vita uongo na uzandiki wa mambo hayo. Kufungamana na siasa hiyo ni makosa, hivyo Sheikh Ponda hayupo sahihi na amekiuka mifumo ua kiislamu.

Siasa halali kwenye Uislamu ni ile ya mfumo wa uongozi wa serikali ya kiislamu pekee. Na si hii ya kuongea uongo na uzandiki, kuzushia mtu na akija upande wa pili basi mnamsifia.... Kiyfupi dini haiendani na siasa za namna hiyo
 
s munaleta udini bas nchi hii hataweza kuongoza mwislam hata siku moja, sie wakrist ni weng kinyama nchi hii!! all in all acheni ujinga wa kuleta udin wa kiislam hapa ponda kakosea anashili adhabu yake kutoka kwa masheh.
 
Ushawahi kuwa na ushahidi halisi wa hayo unayoyasema, mbali na kusikiliza mtandaoni?

Aina hii ya siasa ya kuzuliana majukwaani, kupakaziana uzushi Uislamu hairuhusu kwani inapiga vita uongo na uzandiki wa mambo hayo. Kufungamana na siasa hiyo ni makosa, hivyo Sheikh Ponda hayupo sahihi na amekiuka mifumo ua kiislamu.

Siasa halali kwenye Uislamu ni ile ya mfumo wa uongozi wa serikali ya kiislamu pekee. Na si hii ya kuongea uongo na uzandiki, kuzushia mtu na akija upande wa pili basi mnamsifia.... Kiyfupi dini haiendani na siasa za namna hiyo

Ponda ameunga mkono upinzani kwa sababu upinzani umeonyesha dhamira ya dhati ya kuwaachilia huru masheikh wetu na hilo ni jambo zuri na la kuigwa na kila muislamu nchini.

Kuiunga mkono CCM kwenye uchaguzi huu maana yake ni kuisaidia katika uonevu na udhalimu wake dhidi ya masheikh na maulamaa wetu!

Sheikh Ponda hajakiuka mfumo wowote wa kiislamu la sivyo wewe unataka kutuma meseji kuwa waislamu wasipige kura, wasigombee wadhifa wowote wa kisiasa nchini. Yaani unamaanisha mzee Mwinyi na Kikwete walitenda dhambi kugombea uraisi na kuwa maraisi!!!. Ajabu hii!!!

Yaani ukija na mawazo hayo unamaanisha masheikh wote waliomsaidia Nyerere kumng'oa mkoloni wote walikiuka uislamu n.k

Unao mfano wa nchi yeyote duniani inayoongozwa kwa mfumo unaouita wa kiislamu?, au elezea mfumo wa kiutawala wa kiislamu ni upi na mfano wake ni upi?

Mawazo yako siyo sahihi!
 
4. Sheikh Ponda yuko sahihi, hatua yake ni kwa maslahi ya umma wa kiislamu
Katika nchi hii vyama vya siasa, chaguzi na haki za kikatiba ni vitu halali na vya kisheria. Ni mfumo wa kubadili uongozi ili kila mtu au kundi fulani la jamii kuweka utawala ambao wanahisi watanufaika au kupata ahueni, fursa na manufaa fulanifulani. Napenda kuwafahamisha wahadhiri wetu kuwa kumekuwepo kilio katika jumuia za kiislamu kuhusu Udini wa wazi katika awamu hii, Shura ya maimamu ilitoa waraka wenye kuonyesha kisayansi kabisa teuzi zilizofanywa na awamu hii zinavyonuka udini. Teuzi zimelalia upande wa imani moja mpaka aibu almost kwa uwiano wa 80:20.

Haya kwanza kabisa aliyakemea Sheikh Khalifa na baadae Shura ya maimamu ikatoa waraka mzito, wa kishujaa na wa kukumbukwa juu ya jambo hili. Sasa kwa ubaguzi huu wa dhahiri kabisa usio na aibu nyie wahadhiri wetu mnaanza kumpiga mishale mtu ambaye anatumia taratibu halali zilizoko nchini ili kusimika utawala utakaotenda haki kwa wote?

Hatua anayoichukua leo Sheikh Ponda ni hatua kama ambazo Masheikh wetu walichukua kumsaidia Nyerere ili kumtoa mkoloni ili kusimika utawala mpya utakaoheshimu maslahi yao na haki yao. Sheikh Ponda hana tofauti na masheikh akina Tambaza, Ramia, Chaurembo na wengineo waliosimama bega kwa bega na Nyerere kung'oa utawala dhalimu na kuleta utawala wa haki
Ninaweza kukubaliana na post yako.

Ila kwa hili huwa siamini Sana.

Kweli ingekua mbaya Kama teuzi zote zingekua za Dini moja.

Ila hatuwezi kulazimisha lazima uwiano uwe 50:50.

Maana mteuzi huangalia mtu ambaye atamfaa kwa kazi anayohitaji ifanyike. Sasa Kama katika uteuzi wake ikatokea umelalia upande Fulani tusiamini Kama alidhamiria kulalia huko.

Tuangalie Je Kuna ubaguzi wa dhahiri wa sera , ama Sheria au utendaji wa kupendelea upande mmoja au kukandamiza upande mmoja.?

Hapo lazima wananchi wote tukemee na kushinikiza vitendo hivyo vikome.

Ila swala la Nani kateuliwa, Kama anafuata taratibu za Kisheria na katiba( katiba yetu Haina upendeleo wa Kidini).

Basi hiyo sio hoja.
 
Hatuzungumzi kubalance, kusema kweli mimi mwenyewe siyo shabiki wa kubalance ila kuna fairness fulani ikikosa unaiona wazi kuwa sonething is wrong!

Hebu fikiria, hivi kwa nini haijawahi kuwa kinyume, yaani all the time kila teuzi zinazoinvolve watu wengi unakuta watu wa imani moja ni wengi kuliko wa imani nyingine? .

Usiniambie kuwa hakuna waislamu wa kutosha wenye elimu na vigezo vya kushika nafasi maana waislamu wenye ekimu na sifa wapo kutosheleza kila aina ya nafasi, maana nafasi na teuzi zote hazizidi watu 2000, na kuna maelfu na maelfu ya waislamu wenye madigrii, uzalendo, ujuzi, nidhamu na kila aina ya sifa.

Hivi una habari kuwa rais akiamua anayo mamlaka ya kuteua 80% ya hizo teuzi kuwa ni wasukuma kushika nafasi za wakuu wa mikoa, wa wilaya, wakurugenzi n. k. kisha akajitetea kuwa kwani hawa niliowateua hawana sifa?. Na kweli kila ukiangalia vigezo wanavyo!. Lakini akifanya hivyo siyo sahihi ni Ukabila wa wazi. Hivyo hivyo kuteua 80% watu wa dini moja wakati hata watu wa dini nyingine wapo wenye vigezo ni udini wa wazi!

Ngoja nikupe challenge tu, itokee raisi Muislamu nchini halafu kia teuzi anagonga 80% waislamu, 20% Wakiristo halafu uje uone kelele za udini zitakavyomuandama kila kona!

Jiwe hana aibu ananuka udini ajabu!
 
Ushawahi kuwa na ushahidi halisi wa hayo unayoyasema, mbali na kusikiliza mtandaoni?

Aina hii ya siasa ya kuzuliana majukwaani, kupakaziana uzushi Uislamu hairuhusu kwani inapiga vita uongo na uzandiki wa mambo hayo. Kufungamana na siasa hiyo ni makosa, hivyo Sheikh Ponda hayupo sahihi na amekiuka mifumo ua kiislamu.

Siasa halali kwenye Uislamu ni ile ya mfumo wa uongozi wa serikali ya kiislamu pekee. Na si hii ya kuongea uongo na uzandiki, kuzushia mtu na akija upande wa pili basi mnamsifia.... Kiyfupi dini haiendani na siasa za namna hiyo

Kwa hivyo ndugu yangu aendelee kusota gerezani kwa kosa la kwenda kuposa mtoto wa mtu aliyebambikiziwa kesi ya ugaidi. Viongozi wa CCM waendelee kutuibia pesa tunazokatwa kodi huku wengine wakijijengea majumba zaidi ya 30 . Unataka Tuusubiri huo uongozi wa mfumo wa kiislamu?
 
Nitoe mimi, asinihusishe kabisa na sichaguliwi wa kumchagua

Ndugu yangu naomba kura yako umpigie Lissu ili akawatoe maulamaa na masheikh wetu wanaosota Jela kwa sababu ya udhalimu wa serikali ya CCM

Kura yako ni msaada kwa wake, watoto, ndugu na familia za masheikh wetu zinazoangamia na kuteketea kwa ukosefu wa kiongozi wa familia ndani ya nyumba.

Kama wewe siyo muislamu basi wanusuru ndugu zako binadamu wenzio wako jela kwa sababu ya uonevu wa serikali ya CCM

Kama wewe ni muislamu basi jua ndugu zako hao katika imani wana hali ngumu sababu ya dhulma. Na wewe una dhima ya kuwasaidia. Sasa wasaidie hawa kwa kuweka mtu madarakani atakayekwenda kuwaachia huru.
 
Aliyewafunga masheikh ni muislamu mwezako ambaye alipigiwa kura na waislamu kwa kuambiwa na Sheikh Ponda,sasa Sheikh Ponda anakuja tena kutuambia tumchague mtu mwengine ila safari hii anayetuambia tumchague ni kafiri.

Sasa hapo ndio najiuliza huyu kafiri ana nini hadi sie waislamu tumchague? maana huyu kafiri ni kama walivyo wanasiasa wengine tu wengi wanafki na hana tofauti na hao.

Huyu kafiri Lissu alituambia kuwa Lowassa ni fisadi ila baadaye anakuja kusema Lowassa sio fisadi na ndio maana hajashtakiwa alikula matapishi yake,sasa inakuaje Sheikh Ponda atuchagulie mtu mnafki kama huyu?ataweza kweli kutekeleza hiyo ahadi aliyoitoa kwa waislamu na huu unafki wake?

Huyu Lissu alisema ACT si chama cha upinzani kwamba kinatumika na serikali kuvuruga upinzani na akamtaja hadi Zitto kabwe kuwa anatumika na serikali hivyo si mpinzani,ila leo Lissu anashirikiana na ACT wakati alishasema kuwa hicho si chama cha upinzani bali kipo hapo kuuwa upinzani.

Sasa mtu kama huyo sie waislamu tumchague wa nini?
BORA LISSU IKIWA UTAMUONA KAFIRI KULIKO MUISILAMU MNAFIKI IKIWA UTAMUONA NA JEI KEI..
BORA KAFIRI KULIKO MUISLAM MNAFIKI
 
BORA LISSU IKIWA UTAMUONA KAFIRI KULIKO MUISILAMU MNAFIKI IKIWA UTAMUONA NA JEI KEI..
BORA KAFIRI KULIKO MUISLAM MNAFIKI
Lissu asingekuwa mnafki asingempigia kampeni Lowassa 2015 ambaye alituambia ni fisadi,ila alivyo mnafki akala matapishi yake kisha akatuambia et kama Lowassa ni fisadi mbona hashtakiwi?

Lakini kama haitoshi Lissu alituambia kuwa ACT si chama cha upinzani na hakijawahi kuwa chama cha upinzani bali kipo hapo kuuwa upinzani kinatumika na serikali,na akamtaja hadi Zitto kabwe kuwa sio mpizani anatumika na serikali. Sasa alivyo mnafki et sasa hivi anashirikiana na chama kisicho cha upinzani(ACT), Lissu atuambie ni lini ACT kimekuwa chama cha upinzani hadi yeye amekubali kushirikiana nacho?

Huyu ni namfki na maneno yake ya kisiasa kama walivyo wanasiasa wengine,sasa kama waislamu wameingia kwenye 18 za huyu mwanasiasa basi ni uamuzi wao ila hakuna kitu hapo.
 
Ndugu yangu naomba kura yako umpigie Lissu ili akawatoe maulamaa na masheikh wetu wanaosota Jela kwa sababu ya udhalimu wa serikali ya CCM

Kura yako ni msaada kwa wake, watoto, ndugu na familia za masheikh wetu zinazoangamia na kuteketea kwa ukosefu wa kiongozi wa familia ndani ya nyumba.

Kama wewe siyo muislamu basi wanusuru ndugu zako binadamu wenzio wako jela kwa sababu ya uonevu wa serikali ya CCM

Kama wewe ni muislamu basi jua ndugu zako hao katika imani wana hali ngumu sababu ya dhulma. Na wewe una dhima ya kuwasaidia. Sasa wasaidie hawa kwa kuweka mtu madarakani atakayekwenda kuwaachia huru.
Mkuu Lisu hakutumwa na Amsterdam kuja kuwaokoa au kuwasaidia waislam usijidanganye kabisa, Lisu ana maslahi yake binafsi si Kwa waislam wala watanzania, wewe mchague Mimi nitachagua nitakaye, pia hakuna kiongozi upande wa pili atamsaidia Islam kama tumeshindwa kusaidiana wenyewe
 
Back
Top Bottom