Hili la Uchumi Supermarket kutuuzia mifuko yenye nembo zao waache

mavado

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2014
Posts
1,153
Reaction score
798
Juzi bhana kuingia Uchumi Supermarket ya pale Quality Center, nimenunua mavitu kedekede, aii kufikia pa kulipa si naambiwa natakiwa nilipie mifuko! Kulipia sio tatizo ila mtoe minembo yenu..:A S angry:
 
ivi huko supa maket kuna nini vya ziada ambavyo havipatikanagi mtaani?
 
Juzi bhana kuingia Uchumi Supermarket ya pale Quality Center, nimenunua mavitu kedekede, aii kufikia pa kulipa si naambiwa natakiwa nilipie mifuko! Kulipia sio tatizo ila mtoe minembo yenu..:A S angry:

Wanasema ni njia mpya ya kudhibiti hiyo mifuko, hiyo hali nimekutana nayo mlimani city naona ni kizungumkuti tupu
 
Mkuu hata mimi limenigusa sasa hivi nachofanya naenda na mfuko wangu
 
Wanaagizwa kuuza na watu wa mazingira, wanaamini ukinunua mfuko hutautupa utautunza ili utumie tena. Wakikutwa wanatoa bure hitozwa fine
 
SHOPAz hawana hiyokitu , nenda kwenye maduka yao ,mikocheni , masaki na mbezi beach pia hawana ule ujinga wakusema hawana shilingi mia au mia mbili ya kukurudishia.
 
..nchi hii tunakurupukaga kufanya maamuzi, essence ya kuuzwa mifuko ni kupunguza matumizi ya plastic, shida huwa hatupewi elimu ya kutosha na alternative, nchi za ulaya e.g england, maduka kama Asda, tesco,aldi n.k huwa wanauza mifuko ya plastic, but huwa wana mifuko kama ya gunia ambayo ni re-usable, simply because wana mipangilio (plans) ya when n where to buy groceries, sisi kuingia supermarket ni jambo la sifa na tunaishia kununua vitu hata hatukuwaza kununua.
 
Juzi bhana kuingia Uchumi Supermarket ya pale Quality Center, nimenunua mavitu kedekede, aii kufikia pa kulipa si naambiwa natakiwa nilipie mifuko! Kulipia sio tatizo ila mtoe minembo yenu..:A S angry:
Una point mkuu. Kwa kweli watoe nembo zao hizo kabla ya kutuuzia. Hata TSN wameanza hiyo issue. Ila watasema mbona unanunua samsung na huombi kubadirishwa nembo.
 
samsung sawa coz sitembei na lile box natembe na simu ila mfukp km nmenunua haupaswei kua na nembo mathalani ya hayo maduka makubwa iwe plain na logo isiyohisiana kabisa na biashara
 
Inamaana wanashindwa kufikiria jinsi ya kufix gharama za mifuko kwenye bidhaa hadi waje kutuuzia hiyo mifuko?
Simple and basic economics zimewashinda.
 
..nchi hii tunakurupukaga kufanya maamuzi, essence ya kuuzwa mifuko ni kupunguza matumizi ya plastic, shida huwa hatupewi elimu ya kutosha na alternative, nchi za ulaya e.g england, maduka kama Asda, tesco,aldi n.k huwa wanauza mifuko ya plastic, but huwa wana mifuko kama ya gunia ambayo ni re-usable, simply because wana mipangilio (plans) ya when n where to buy groceries, sisi kuingia supermarket ni jambo la sifa na tunaishia kununua vitu hata hatukuwaza kununua.

Wacha ujinga,we unajua nchi za ulaya tu hapa Africa, hizo mifuko za gunia sio kwa sababu ni re-usable kama hujui uliza, hizo ni kwa sababu ni disposal zinaoza ardhini haziitaji further treatment hata ukipiga moto yatosha. Hata hizo serikali yetu tulivu ina Microns elekezi kwa vifungashio na mifuko tunayotumia, kwa ujinga wetu tusibeze juhudi zinazofanywa na serikali.
 
Mkuu hata mimi limenigusa sasa hivi nachofanya naenda na mfuko wangu

Ndo hasa lengo lao, hawaitaji kuingiza profit lakin kucontrol matumizi ya mifuko. Naona zoezi limefanikiwa, utunze vyema mpaka uchakae kabisa tufanye recycling
 
Ni kweli lengo ni kupunguza matumizi ya plastic. Na hakuna ubaya kwenda na mfuko wako supermarket au kikapu sokoni. Kwanza ndo wazo jema zaidi
 
Wengine wanafanya hivyo sema sisi hatujazoeshwa. ..mfano CLICKS
 
Wacha ujinga,we unajua nchi za ulaya tu hapa Africa, hizo mifuko za gunia sio kwa sababu ni re-usable kama hujui uliza, hizo ni kwa sababu ni disposal zinaoza ardhini haziitaji further treatment hata ukipiga moto yatosha. Hata hizo serikali yetu tulivu ina Microns elekezi kwa vifungashio na mifuko tunayotumia, kwa ujinga wetu tusibeze juhudi zinazofanywa na serikali.

Ujinga upo wapi hapo ewe mwenye busara Batili
 
Last edited by a moderator:
Nimenunua maziwa na mkate, nafika counter baada ya kuingiza hesabu zao wakaniambia mfuko unalipiwa , nikawaambia warudishe Pesa yangu ni bidhaa yao wachukue siwezi kulipia mfuko tena wenye nembo yao.

Muhudumu akamuita supervisor wake akaniruhusu kutoulipia. Wajinga sana management
 
Back
Top Bottom