Hili la Viwanja na NIDA lisisubiri hadi Julai 2021

Hili la Viwanja na NIDA lisisubiri hadi Julai 2021

Serikali ikiamua kila kitu kinawezekana. Tukitaka nchi tuweze kurithisha watoto wetu, haya mambo lazima yafanyike sasa
 
Huko Ardhi kwa ujumla kunahitajika overhaul. Kupata hati ni mtihani mgumu sana.....inachukua miaka! Binafsi, nimengaika kupata hati ya kiwanja Dodoma toka 2018 na malipo yote nililipa.....hatuwezi kuendelea kama nchi kwa aina ya watu tulionao kwenye wizara hiyo ya Ardhi.

Kama sekta za Ardhi na Majengo zikiongozwa vema, tunaweza kupata kodi karibu robo au zaidi ya bajeti yetu.
 
Kuna watu wanapora viwanja wananchi wanyonge kwa kivuli cha kujiita wao ni wawekezaji.

Mtu anataka kununua nyumba yako na ya yule na ya yule mtaa mzima au kijiji kizima harafu anakupangia bei hii kweli ni haki??hivi ndivyo biashara zinavyokuwa??Wananchi wanarubuniwa na hawa wanaojiita matajiri serikali pia iliangalie hilo kuna watu wameuza maeneo yao kama kwa kushinikizwa ss hivi wanaishi maisha kama ya digidigi.

Kama tajiri alinunua eneo kubwa la kiwanja serikali ichunguze mchakato mzima wa ununuzi je ulikuwa wa haki kweli.

Wengine wanajiona untouchable kwamba serikali haiwezi kuwashughurikia sababu wao ni sehemu ya serikali .
 
Back
Top Bottom