Hili la wanasiasa kushambulia taasisi ni wazi kuwa hakuna mifumo Tanzania

Hili la wanasiasa kushambulia taasisi ni wazi kuwa hakuna mifumo Tanzania

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Imeibuka hulka ya wanasiasa kushambulia taasisi na watendaji majukwaani.

Ni dhahiri kwamba mifumo ina mapungufu. Hivi PM anashambulia taasisi au mtendaji ambaye juu yake kuna bodi, katibu mkuu na waziri, hii ni hulka gani? Micromanagement sio ideal.

Yupo mmoja alihangaika na principal officers Tanesco wakati juu yake kuna manager, mkurugenzi na hata CEO.
Hili la MSD ni hivyo hivyo, serikali inapaswa ijue mapungufu na kutengeneza mifumo.

Kuanika mapungufu pengine bila hata kuthibitisha ni udhaifu.

Tungekuwa na siasa imara, wapinzani walipaswa watokee kwenye hizo hoja kwamba serikali imeshindwa kusimamia taasisi na watendaji wake
 
... very interesting indeed! Mamlaka zote za uanzishaji taasisi ni zao; mamlaka za uteuzi kuanzia watendaji wakuu wa taasisi ni zao. At last wanaishia kulalamika. Tujenge mifumo.
 
Atakaykutwa eneo la kazi ndiyo huyo huyo...
 
... very interesting indeed! Mamlaka zote za uanzishaji taasisi ni zao; mamlaka za uteuzi kuanzia watendaji wakuu wa taasisi ni zao. At last wanaishia kulalamika. Tujenge mifumo.
Hawa jamaa ni kama vile mfyatua bunduki kupelekea kujeruhi/kuua halafu akalaumu risasi iliyotoka kwenye bunduki kuwa ndio imejeruhi/imeua.
 
Hizi thinking inabidi zibadilike. Hatusemi wafiche maovu, hapana. Bali tuondoke na mfumo wa ajabu ajabu.
Tena pesa zinazopigiwa kelele duh. Sio za level ya PM.
 
Back
Top Bottom