Toa mifano hai! Lakini mara nyingi huwa management zao huwa zinawapa support!
Lakini pia kuna ukweli kabisa ikiwa msanii amepewa offer ndogo na akaikataa lazima ataundiwa zengwe...kimsingi matamasha yanayo andaliwa na wasanii na pia wamiliki wa media yana wanyima haki nyingi wasanii na wanakuwa hawana pakusemea!
Ni wasanii wachache wenye guts za kukataa offer za Clouds media au Eatv limited na pengine hawapo! Pengine wasanii wetu hawako huru kabisa na hawana pakutokea maana hao ndio wadau wa music ukienda kinyume nao utapotea tuu!
Kibaya zaidi hata makampuni ya simu au ya bia/soda wakitaka kuandaa matamasha wana kwenda kwenye hizo media na ndio zinapanga nani aitwe au lah....
Ni wazi hatuna msanii ambaye yuko huru kabisa na ana uwezo wa kupambana pekee bila hizo media mbili au moja wapo na kama mnafikiri yupo basi ana wadanganya tuu!
Hata kipindi cha mgogoro wa Clouds na Jide tuliona jide alikimbilia EATV hebu jiulize kwanini hakustand alone? Ukweli ni kwamba wasanii wetu hawako huru kabisa ....