Hili la watangazaji wa radio kuandaa matamasha, limekaaje?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Tumeshuhudia baadhi ya watangazaji wa Radio wakiandaa matamasha yao binafsi kuwatumia baadhi ya wanamziki kutumbuiza. Hivi hii inaruhusiwa na mabosi wao au inakua part ya mikataba yao na mara nyingi kama msanii fulani akiwazingua kutumbuiza kwenye matamasha yao basi atapigwa ban ya nguvu kwani nyimbo zake hazitapigwa daima.

Binafsi hawa watangazaji hawatakiwi kujihusisha na haya matamasha nadhani itakua nje ya majukumu yao pia kutopiga nyimbo za wasanii kwa kigezo cha kutowasupport kwenye maonesho yao ni unyonyaji mkubwa.

Jamani wadau mnalionaje hili
 
Toa mifano hai! Lakini mara nyingi huwa management zao huwa zinawapa support!

Lakini pia kuna ukweli kabisa ikiwa msanii amepewa offer ndogo na akaikataa lazima ataundiwa zengwe...kimsingi matamasha yanayo andaliwa na wasanii na pia wamiliki wa media yana wanyima haki nyingi wasanii na wanakuwa hawana pakusemea!

Ni wasanii wachache wenye guts za kukataa offer za Clouds media au Eatv limited na pengine hawapo! Pengine wasanii wetu hawako huru kabisa na hawana pakutokea maana hao ndio wadau wa music ukienda kinyume nao utapotea tuu!

Kibaya zaidi hata makampuni ya simu au ya bia/soda wakitaka kuandaa matamasha wana kwenda kwenye hizo media na ndio zinapanga nani aitwe au lah....

Ni wazi hatuna msanii ambaye yuko huru kabisa na ana uwezo wa kupambana pekee bila hizo media mbili au moja wapo na kama mnafikiri yupo basi ana wadanganya tuu!

Hata kipindi cha mgogoro wa Clouds na Jide tuliona jide alikimbilia EATV hebu jiulize kwanini hakustand alone? Ukweli ni kwamba wasanii wetu hawako huru kabisa ....
 
Mkuu unaujua mziki vizuri hongera, na kwenye jukwaa la siasa ukiwa thinker kama hivi itakuwa poa sana.
 
Tumeshuhudia baadhi ya watangazaji wa Radio wakiandaa matamasha yao binafsi kuwatumia baadhi ya wanamziki kutumbuiza. Hivi hii inaruhusiwa na mabosi wao au inakua part ya mikataba yao na mara nyingi kama msanii fulani akiwazingua kutumbuiza kwenye matamasha yao basi atapigwa ban ya nguvu kwani nyimbo zake hazitapigwa daima.

Binafsi hawa watangazaji hawatakiwi kujihusisha na haya matamasha nadhani itakua nje ya majukumu yao pia kutopiga nyimbo za wasanii kwa kigezo cha kutowasupport kwenye maonesho yao ni unyonyaji mkubwa.

Jamani wadau mnalionaje hili

Unaweza kumzuia mwalimu kuuza kashata ama Ice cream?
 
Ila inabidi waishi kwa kujipandisha na sio kusubiri kunyenyekea kwa kila kitu hata hizo media zitawaogopa na kusema huyu ana standards za juu na anapendwa atatuvutia pesa lazima tumlete ns utaona matunda...sasa unakuwa na mambo ya ajabu na standards zako zipo chini kweli mtu unategemea nini...kupost upuuzi kwenye social media bila kufikiria...kulalamika eti wengine wanafanyiwa hivi au vile je wewe umefanya jini wakubabaikie wakikupigia sinu unapokea kama vile Mfalme wa dunia kakutafuta...ukiambiwa bei ndogo na unajua ndogo unaogopa unakubali bila kujibu na kusema mimi ni hivi au vile...so utapanda lini?

Ndio kama wengi wameshaongelea humu wengi hawajitumi wanabaki na ma wivu ya kijinga bila kufata wivu wa kuendelea kama kutaka kujua kafikaje hapo nami nifike...
 
Back
Top Bottom