Hili la wizi na wawekezaji kuanza kusita limenishtua sana

Hili la wizi na wawekezaji kuanza kusita limenishtua sana

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Rais Samia ametujuza hivyo leo.

...kwamba wizi na umeanza kurejea kwa kasi katika Idara nyingi za Serikali.

...zaidi ametujuza hata wawekezaji waliokuwa katika hatua za mwisho kabisa za kumalizia taratibu za uwekezaji wameanza kusita!

Haya mambo yanahitaji mjadala mpana kwa maslahi ya Nchi.
 
wanasita kwasababu gani? walitarajia nini ambacho wameona hawatakipata kwa rais huyu? mwekezaji mwaminifu lazima angependa kuendelea kwa mama kwa upole na kupenda kwake majadiliano na kusikiliza watu. hao wanaokimbia waende tu waje wapya kwasababu lazima watakuwa sio wazuri.
 
Bora fedha ziingie kwenye mzunguko kuliko awamu ya tano watu wanapiga juuu kwa juu
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Labda jambo kubwa tunalopaswa kulitafutia majibu ni kuwa, kwa nini Watanzania wengi wana DNA ya kukosa uaminifu?
 
nchi imejaa MANYANI. mama akicheka atavuna mabua. watu wanaiba utadhani wataishi milele.

siku hapa iletwe sheria ya Mchina tu. ukileta ubadhirifu kitanzi au mvua za maana jela na kufilisiwa.
Mama anacheka na nyani atavuna mizizi siyo mabua tena.
Maana hayo mabua unaweza wapelekea ng’ombe wakala
 
Mama kuna kitu anakivizia ili na yeye aanze kuuma
Nalog off
 
Tofauti ya Ulaji wa mbuzi na punda ni kuwa
Mbuzi anakula majani huku akihama na kwenda sehemu nyingine
Na Punda akila anang’oa mpaka mizizi akijua wengine wasikute kitu na hao ndio baadhi yao
 
Back
Top Bottom