Hili la wizi na wawekezaji kuanza kusita limenishtua sana

Hili la wizi na wawekezaji kuanza kusita limenishtua sana

Rais Samia ametujuza hivyo leo.

...kwamba wizi na umeanza kurejea kwa kasi katika Idara nyingi za Serikali.

...zaidi ametujuza hata wawekezaji waliokuwa katika hatua za mwisho kabisa za kumalizia taratibu za uwekezaji wameanza kusita!

Haya mambo yanahitaji mjadala mpana kwa maslahi ya Nchi.
Mbona rahisi tu. Kama yeye ameamua kuendeleza umagufuli maneno ya nini? Afanye kama angalifanya magufuli. Awatumbue tu na kuwakabidhi kwenye vyombo vya haki.
Kuendeleza sera za magufuli haihitaji maneno ila vitendo. Fisadi wakigundua samia ni mtu wa maneno tu fisadi watarejea tena kwa nguvu.
 
Rais Samia ametujuza hivyo leo.

...kwamba wizi na umeanza kurejea kwa kasi katika Idara nyingi za Serikali.

...zaidi ametujuza hata wawekezaji waliokuwa katika hatua za mwisho kabisa za kumalizia taratibu za uwekezaji wameanza kusita!

Haya mambo yanahitaji mjadala mpana kwa maslahi ya Nchi.
Ni katika muda huo mfupi wa mwezi mmoja ambao amekuwa madarakani, au haya yalianza kabla ya hapo?

Haya mambo yanaposemwa na kuyaacha yakielea bila ya ufafanuzi juu yake yanatia shaka sana juu ya ukweli wake

Kwa nini imekuwa hivyo.
 
Rais Samia ametujuza hivyo leo.

...kwamba wizi na umeanza kurejea kwa kasi katika Idara nyingi za Serikali.

...zaidi ametujuza hata wawekezaji waliokuwa katika hatua za mwisho kabisa za kumalizia taratibu za uwekezaji wameanza kusita!

Haya mambo yanahitaji mjadala mpana kwa maslahi ya Nchi.
eeehhhh bwana wewe mchukie au mpende lakini kigogo anasema kweli. nakumbuka post yake moja wakati watu wanauliza alipo Magu na yeye alishasema kuwa magu kasharudisha number, aligusia hili kuwa watu wameanza kuiba mawizarani na hadi resrve bank. Sasa hayo Rais mwenyewe amekiri.
 
Fisadi wakigundua samia ni mtu wa maneno tu fisadi watarejea tena kwa nguvu.
Na hapa tayari anawafungulia mlango waaaa!

Alichotakiwa kufanya, ni kuiga staili ile ile ya mtangulizi wake. Atembee kwa mguu hadi pale hazina na kuondoka na wawili au watatu hivi kwa mpigo; halafu ndio aje kutueleza matokeo ya kazi yake.

Huyu mama atapata taabu sana na hawa watu asipochukua tahadhari mapema.
 
Mama anatumia mawaziri wenye mawazo yaleyale ya enzi za Mwendazake,hakika watamuangusha Sana.
 
Mama anatumia mawaziri wenye mawazo yaleyale ya enzi za Mwendazake,hakika watamuangusha Sana.
 
Wamesita kwa mambo mawili;
Moja, inawezekana walifanya makubaliano ambayo hayakuwa na mazingira ya rushwa. Sasa watendaji wamekuja na mahitaji ya rushwa kwa kuwa mwendazake hayuko.
Pili, inawezekana terms za mwanzo zilikuwa finyu na kuna nafasi ya kuzipeleka kwa Rais mpya kuona kama kuna nafuu. Makubaliano ya biashara huwa ni ya muda mrefu sana na magumu.

Kama la kwanza ndio lililotokea, tuna taabu kama nchi!
 
mbona hajawataja hao wezi ingekuwa makufuli angeasema hadharani na mbona hajachukua hatua huko mbele ya safari mtaona mengi maneno matamu sio vitendo
 
Back
Top Bottom