Hili lilikuwa tusi eti sasahivi ni sifa

Hili lilikuwa tusi eti sasahivi ni sifa

Faza, kama una kamusi ya Kiswahili hapo fungua halafu uangalie neno 'nyoko' uone fasili yake.

Mara nyingi watu tunapenda kusadiki kuwa tunakijua Kiswahili kwa sababu tu 'inaonekana' tunakiongea vizuri bila shida lakini msamiati wetu unakuwa si mpana kivile.

Kama una kamusi ya Kiswahili (inavyoelekea kuna watu wengi hawana kamusi za Kiswahili majumbani mwao) wewe litazame tu hilo neno uone.

Unaweza kumaliza utata huu kwa kunukuu maelezo yaliyoandikwa kwenye hiyo kamusi uliyonayo. Wengi wetu tuna kamusi za kiswahili - English!
 
Sasa hawa wasiojua kuwa 'nyoko' ni mama ni watu wa wapi hawa?

Mwingine kasema kabisa eti yeye ni mtu wa Pwani lakini hajawahi kulisikia hilo neno.

Asikutishe na neno mtu wa pwani, wengine hawajui kiswahili, uhenda ni mmasai aliyezaliwa pwani, So yuko sahihi.
 
Kwa waliosema nyoko ni mama wapo sahihi kwa tafsiri sahihi ya kamusi. Mimi kwa upande wangu nadhani neno MSHENZI ndio limebadilika maana.
 
Back
Top Bottom