Hili limekaaje wadau, Hebu nipeni ushauri kuhusu hili jambo la ndoa

Hili limekaaje wadau, Hebu nipeni ushauri kuhusu hili jambo la ndoa

Liverpool_Jr

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2019
Posts
1,220
Reaction score
1,415
Tokea Form 6 nimekua nikiwaza kujiajiri tuu, ila vile maisha ya kiyatima na kimaskini yamenichelewesha kidogo.
Ila nashukuru Mungu Nina miaka 30 na mambo yanaenda (I have started Small..!!).

Nilikuaga mwajiriwa wa private nikaenda serikalini, nikasoma na sasa ni Free soul..!!.

SHIDA IKO HIVI...

Tokea mwaka 2018 nyumbani (walezi) wamekua wakiniuliza ""UTAOA LINI?"" sijawahi kutoa jibu kwasababu ""HATA HUYO WA KUOA SINA..!!""

Nilikuaga na mmoja akazingua na kuniita "KAFIR"" sababu ya ukristo wangu japo nilimsaidia sanaa yule fala mpaka akawa na maisha poa.
ALINIFANYA NIPOTEZE HAMU YOTEE NA LADHA YA KOA au KUISHI NA MWANAMKE PAMOJA TENA.
Tokea jambo litokee ni miaka 5 ila SIJAWAHI TENA KUWAZA.

Kuwaambia nyumbani kuwa SINA MPANGO wa kuoa naogopa maana walezi wangu kila Siku wanaongelea ""Marehemu wazazi wangu wanahitaji kuoana wajukuu wakiwa hukohuko peponi..!!""
Halafu huwa nawaheshimu sanaa walezi wangu, maana bila wao NISINGEKUA HAPA KABISAA.
Naogopa kuwavunja moyo na ukicheki ni wazee (60's).

Na sababu hasa ya KUDELETE KUOA ni..

1. Nimeamua kujiajiri kwa kuinvest.
Sasa najiuliza, Unajihangaisha mwenyewe na kupata mali kiasi, halafu unaoa.
Huyo mke baada ya miaka kadhaa anakwambia tuachane..
YAANI MALI NILIZOTAFUTA MWENYEWE KWA MIAKA ZAIDI YA 5 LEO NIGAWANE NA MTU KISA NI MKE WANGU?
•Juhudi zangu zote ziishe kirahisi hivi, KISA NDOA?

2. Wanaonizunguka asilimia kubwaa wanalia na MATESO YA NDOA ZAO.
Hawa walezi wangu sometimes ni wasuluhishi na huwa wananishirikisha nitoa mawazo yangu.
•SASA WANATAKA NA MIMI YANIKUTE AU..??

3. Nimezoea maisha ya ubachelor na free soul.
Tokea nitoke home kwenda kusoma Diploma mpaka sasa Nina Masters of Science in ..... maisha yangu ni kutembea na kuzurula tu mikoani.
Sasa nioe halafu vile nianze kuomba ruhusa kwa mke wakati mi nishazoea nikiwa bored huwa naenda stendi kukata tiketi halafu ndukii...
Sijawahi KUAGA zaidi ya KUTOA TAARIFA kwa watu wa karibu sana ila SIO KUOMBA RUHUSA.
•Sasa nikishaoa si ndio vile unaanza kuomba ruhusa, kunegotiate na mambo kama hayo na Huyo mke!

4. Kama yule dada nilimkuta na stress za un-employment, nikajihangaisha mpaka akapata maisha.
Ila malipo yalikua ni kuitwa KAFIR kisa UKRISTO WANGU na mema yoteee yalisahaulika.
•Sasa Huyo ajae nae si mwanamke kama yule tu?

Najua...
KUOA NI MUHIMU, FAMILIA NI LAZIMA ila MOYO UMEGOMA KABISAAA.

Nakumbuka mwaka 2018 nilijiwekea malengo "Nikifika 2020 lazima niwe na MCHUMBA au NDOA.
Ila hata DALILI SINA..!!

Sometimes kuna kitu ndani kinaniambiaga ""Ole wako ujaribu, You will doomed""

USHAURI TAFADHALI?
Hebu MLIOA naombeni USHAURI na TECHNICS mlizotumia kuondoa hii COMPLEXITY FEAR ya haya maisha..!!!

KUOA NATAMANI ila ""....…..hiii bagosha (in JPM voice)""

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
Sio lazima kuoa ni vile tu mnafanya jambo kuwa kama la lazima


mi na enjoy tu u bachelor kama nyama na maziwa napata yanini nijiangaishe na ufugaji kuhusu mtoto mbona ntapata tu sio mpaka ndoa
 
Do what your heart tells you to...........
 
Wafu hawana uwezo wa kuona wala kutenda mtu akifa ndo kaenda mazima mpaka kristo atakaporudi ndipo parapanda italia na makaburi ya walio mema yatafunguliwa.

Pili kuhusu kuoa: suala hili lilikuwa na umuhimu zamani kwa sasa ni kupoteza muda na rasilimali madada wanaingia kwenye ndoa kama kitega uchumi japo sio wote akishaona mali zimekuwa nyingi wanaachika ili mgawane 50 / 50 kisheria

ushauri wangu: tafuta pesa wekeza sana achana na ndoa kwanza umri wako bado mdogo tafuta pesa wekeza sana achana na wanawake
 
Tatizo ni ubahiri na kukosa mifano bora ya ndoa kwenye maeneo yako( jamii unayoishi) bila shaka uko Iringa, Manyara au Pwani.
 
Tatizo imni ubahiri na kukosa mifabo bora ya ndoa kwenye maeneo yako( jamii unayoishi) bila shaka uko Iringa, Manyara au Pwani.
 
Usioe mkuu...narudia tena USiOE! Kama watoto tafuta demu piga mimba leo watoto..pambana na life lako as long as unafurahia unachokifanya.... hakuna furaha kwenye kuoa mkuu..belive me!
 
Ngoja waje.
Nachoshangaa hata mimi mchumba wako umenikana.
 
Hivi upate ndoa bora na familia yenye furaha. Huwaze kuachika ili upate 50/50?, inaingia akilini kweli?. Atakuwa mpumbavu huyo mwanamke atakayevunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.

Achana na uoga, na usichague mwanamke tu alimradi ni bora mwanamke. Chagua mwanamke bora na mwenye tabia njema, ambaye unajua apa kweli nimepata mke na najivunia. Wanawake wote si sawa. Na ndoa zinatofautiana mkuu. Na ww pia ujihakikishie kuwa tabia yako ni njema na utammudu mkeo. Achana na uzinzi na hao wanaokushauri zaa tu.
 
Write your reply...Sio lazima kuoa ni vile tu mnafanya jambo kuwa kama la lazima


mi na enjoy tu u bachelor kama nyama na maziwa napata yanini nijiangaishe na ufugaji kuhusu mtoto mbona ntapata tu sio mpaka ndoa
We sometimes bored and need a compan
We sometimes fill empty sets in our heart.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
Back
Top Bottom