jamani huyu Triple G (GGG) ni mtu hatari hamna tena. Kuna wakati Mayweather alikuwa anachonga ngenga jamaa akasema kama anataka pambano lipigwe tuu. GGG alisema hamuogopi Mayweather na staili yake ya 'Ping Pong' yaani ya kigana kwa kuvizia. (GGG yeye hupigana kwa kwenda mbele tu huwa harudi nyuma) Hata hivyo, Mayweather Sr. (Baba wa Mayweather) aliogopa akasema mwanake hawezi kupigana na 'Giant' akimaanisha GGG. Huyu jamaa anashikilia mikanda minne ya uzito wa middle weight kwa maana ya kuwa kawapiga mabondia wanne walikouwa mabingwa wa uzito wa middle weight. Canelo kwa upande wake ni uzito wa chini na siyo Middle weight. Canelo kuna baadhi ya mapambano amewahi kupewa ushindi lakini kiukweli ilikuwa kama kabebwa yalikuwa sare au alishindwa (mfano angalia pambano lake na Erislandy Lara (July 12, 2014). kwa upande wa GGG jamaa mapambano yake yote aliyoshinda hana hata chembe ya utata. mtafute u-tube ndo utamjua vizuri.