alm
Member
- Oct 16, 2013
- 88
- 108
Bila kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kijinsia nk ni jukumu letu sote kama Watanzania wapenda amani, umoja na mshikamano wa taifa letu kumwondoa Rais Magufuli mwaka huu kupitia sanduku la kura wakati wa uchaguzi mkuu unaofanyika mwezi Oktoba.
Pamoja na mazuri machache sana aliyofanya amefanya makosa na maovu makubwa kwa mustakabadhi wa mshikamano wa taifa letu kupitia kauli zake na matendo yake.
Kwa binadamu {tena Rais wa nchi} kusema hadharani atafanya watu waishi kama mashetani inatosha kabisa kuona huyo binadamu siyo wa kumkaribia achilia mbali kupewa madaraka ya kuongoza taifa.
Mungu aliyetuumba na kututaka tuyaishi mafundisho yake hata tunapomkosea anatupa muda wa kujirudi na kujirekebisha na kamwa hajawahi kututakia tuishi kama shetani, sasa inakuwaje binadamu utake binadamu wengine waishi kama mashetani?
Hii itakuwa fundisho kwake na viongozi wengine watakaofuta kwa kutambua Watanzania ni watu wapole na waungwana ila hawataki kuchezewa ovyo na viongozi wanaojiona Mungu mtu.