Hili nimeliona sana tu kwa Walinzi wa Majumbani sehemu mbalimbali je, ni sahihi Kiulinzi au wanahitaji Msasa zaidi?

Kuna babu mmoja mmakonde alikuwa analinda hardware fulani hapo Dar maeneo ya msasani kwa muda mrefu sana. Huyo babu amelinda hiyo hardware tokea ikiwa ndogo hadi kuwa hardware ya jumla na rejareja yenye mtaji mkubwa.

Kwa ufupi hiyo hardware na maduka ya jirani hayakuwahi kuibiwa kabisa wakati babu akiwa analinda. Yule Mzee baadae alifariki, wakabadilisha walinzi na kila mara wakawa wanaibiwa.
Yule babu alikuwa ikifika muda analala na hakuna mtu aliyekuwa anaiba.
Najiulizaga mpaka sasa yule babu alikuwa anatumia mbinu gani au teknolojia gani sijapata jibu.
 
Mlinzi ni asilimia 50% na ww mwenyewe ni asilimia 50% yaani umemuacha mwenzako nje ili akustue panapotokea tatizo !! Sasa atakustuaje?

Tabia yake ni kusikiliza radio ,usiku kucha mbona leo sisikii hiyo radio? Usivute shaka! Amka angalia kuna nn? Kila siku nikiamka nikimchungulia nakuta amekaa palepale mbona leo HAYUPO PALE? chunguza zaidi.

Mlinzi wako u amchukuliaje? Thamani yake kwako ipo vp? Unajali afya yake? Unajisikiaje ukihakikisha umempa chakula, maji ya kunywa chupa ya chai / kahawa.

Asubuhi mnazungumza nn? Unaonesha kujali kazi yake? Unamuachia chochote kama nauli?

MLINZI NI WA THAMANI KUBWA SANA KWAKO MHESABU KUWA NI MWANAFAMILIA.
 
Kule kwetu nilikatiza usiku saa saba hivi kwenye hoteli fulani nikakuta walinzi wa sehemu zingine karbu wapo wote na redio na jiko la mkaa wanachoma mahindi cha ajabu walinikalibisha pia yaani hawaulizi unafanya nn usiku wao wanaangalia sura tu
Baadae rudi ukaote nao moto halafu uguse geti. Utakuja hapa kutoa ushuhuda mkuu. Kila laheri
 
Uliposema tu kuwa alikuwa ni Mmakonde nimeshajua kwanini Wezi walikuwa hawaendi Kuba hapo. Wamakonde noma.
 
Najaribu kupata point yako ni ipi lakini nimeshindwa,
By the way walinzi binafsi lazima wapate mafunzo ya awali ya ulinzi. Hivyo makampuni makubwa ya ulinzi hufundisha maaskari wao guard basic courses ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji. Mfano
1. Doria
2. Kwanini watu hutenda uhalifu
3. Utambuzi, upekuzi, haki za binadamu, crime scene management n.k..
Hivyo mlinzi anapokuwa duty kitu mhimu ni visibility yake au huitwa physical presence . Wengi hawana mafunzo ya awali na pia mapungufu ya kibinadamu na ukichwa ngumu wa kitanzania. Kuwa makini na Hawa Jamaa wakati mwingine wao hugeuka wezi badala ya kulinda. Ulinzi Bora ni kutafuta kampuni ya ulinzi na si kuajiri wewe mwenyewe. Inatosha
 
Kuna jamaa yangu huwa analaza gari mahall ,kachomolewa vifaa vya gari , yaani IST imebaki meno nje, cha chakushangaza Mlinzi alimkuta yupo katika gari nyingine kalala! Yaani yeye ndiyo kamuamsha.
 
Walinzi wanamlinda Rais. Huyo wa nyumbani kwako ni mtu anayekaa macho ili mshenzi akitokea awahi kupiga simu polisi.
 
Ebana ni tabora nini ipuli?
 
Binadamu Usiku tumeumbwa tulale mlinzi hawezi kuwa timamu usiku mzima bila kuwa na push factors...hili ni somo siku nikipata muda nitaliweka hapa vizuri.
 
Tabia ya kuajili wafungua mageti mnawaita walinzi sisawa
Hakuna neno Kuajili ( kama ulivyoandika hapa ) katika Lugha ya Kiswahili bali kuna neno la Kuajiri. Tatizo lenu mnakuja Kuchangia Mada zangu hapa JamiiForums huku mkiwa na Chuki nami ambaye mnanichukia pasipo sababu halafu Mungu anawalaani kiasi kwamba hadi mnakosea hata Kuandika vyema maneno Sanifu ya Lugha yetu pendwa na tukuka ya Kiswahili.
 
We kuweza kukatisha usingizi haha acheni usiku mrefu nyie, mlinzi na kirungu jambazi na pistol , mlinzi tafuta chimbo lenye giza tulia no kelele kam mbu wengi tumia dawa, muda wa wezi saa tisa nane na kumi asubuh unalal kwa machale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…