Adverse Effect
JF-Expert Member
- Oct 8, 2017
- 2,049
- 5,449
Kuna babu mmoja mmakonde alikuwa analinda hardware fulani hapo Dar maeneo ya msasani kwa muda mrefu sana. Huyo babu amelinda hiyo hardware tokea ikiwa ndogo hadi kuwa hardware ya jumla na rejareja yenye mtaji mkubwa.
Kwa ufupi hiyo hardware na maduka ya jirani hayakuwahi kuibiwa kabisa wakati babu akiwa analinda. Yule Mzee baadae alifariki, wakabadilisha walinzi na kila mara wakawa wanaibiwa.
Yule babu alikuwa ikifika muda analala na hakuna mtu aliyekuwa anaiba.
Najiulizaga mpaka sasa yule babu alikuwa anatumia mbinu gani au teknolojia gani sijapata jibu.