Hili suala kisheria limekaaje!?

Hili suala kisheria limekaaje!?

kupukupu

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2016
Posts
499
Reaction score
1,094
habari ndugu wanasheria na wadau wa JF!

Kuna mtu amekopeshwa pesa huku akiweka nyumba yake kama dhamana endapo atashindwa kulipa deni, aliwasilisha offer ya kiwanja palipo hiyo nyumba maana alidai kwamba hati ya nyumba bado hajapata.

Baada ya kufanyika hayo makabidhiano (kimaandishi) mbele ya mwana sheria, imekuja kugundulika kwamba huyu mtu anayo hati ya kiwanja tofauti na alivyosema (alidanganya).

Je, inaruhusiwa kwa mtu mmoja kumiliki offer na hati ya kiwanja kwa wakati mmoja?
Ipi njia sahihi kisheria inaweza kutumika kukabiliana na huyu mtu.?

NB; nimejaribu kufanya mawasiliano na muhusika kadai kwamba hati ya kiwanja kaipata kipindi cha hivi karibuni japo kagoma kuiwasilisha hiyo hati.
 
Hili swala lako nalijua na mdaiwa ni Mteja wangu tukutane mahakamani
 
kwani mlivyoandikishana si mmeandikishana ukiwa haujui kama ana hati? maana kama ni hivyo wewe bado utalindwa kutokana na udanganyifu aliufanya yeye bila wewe kujua hivyo umeingia nae mkataba ukiamini yote aliyokwambia ni sahihi.

swali langu ni huyo jamaa ameshindwa kulipa deni?
 
Back
Top Bottom