Hili wimbi la maparachichi ya kijani na makubwa yalojazana Dar yanatoka wapi?

Hili wimbi la maparachichi ya kijani na makubwa yalojazana Dar yanatoka wapi?

hayo maparachichi ni GMO, kwani yanachukua muda mfupi mti wake kukua, kukomaa na kutoa matunda, yana gamba gumu (tofauti na maparachichi ya kawaida ambayo yakiiva hulainika upesi), pia ladha yake ni tamu sana. Kwa kifupi siku hizi kuepuka GMO ni ngumu sana kwani mimea mingi imeboreshwa ili kuweza kustawi kwa muda mfupi na kutoa mavuno mengi.
Acha uongo
Karibu Njombe ujionee
Parachichi Kuna Aina mbalimbali usikariri uliyoyazoea pekee,tembea uone
Njombe, Burundi na Rwanda
 
Mimi niliuliza nikaambiwa ayanatoka Burundi. Nikawaza sana, ila huwa najiuliza haya maepo ya sh 300-500 mazima kwel?
 
Hayana shida hayo, yanatoka Burundi na hupatikana kwa wingi kwa mikoa ya jirani
 
Acha uongo
Karibu Njombe ujionee
Parachichi Kuna Aina mbalimbali usikariri uliyoyazoea pekee,tembea uone
Njombe, Burundi na Rwanda

Kwani kupatikana Njombe ndo isiwe GMO.! Mbegu [miche] zake umepata wapi?
 
Hayo maparachichi unayoyazungumzia yanatokea BURUNDI.

Ni Organic kabisa ondoa shaka..!
Kwa wingi wa hayo mapaeachichi sidhani kama sio gmo
Moja ya lengo la modification za genes ni kuongeza uzalishaji , they seems to tick all the boxes,, makubwa , matamu na ni mengi, sio rahisi sana kwa parachichi la kawaida .
 
Hayo maparachichi unayoyazungumzia yanatokea BURUNDI.

Ni Organic kabisa ondoa shaka..!
Inawezekana kweli

Nilikuwa mtabilia Jkt ile ilikuwa kambi ya zamani ya wakimbizi wa burundi kulikuwa kuna maparachichi makubwa sana sijawahi yaona mahali pengine kokote

Na kulikuwa na migomba ya aina fulani mirefu sana itakuwa ni mbegu za huko
 
hayo maparachichi ni GMO, kwani yanachukua muda mfupi mti wake kukua, kukomaa na kutoa matunda, yana gamba gumu (tofauti na maparachichi ya kawaida ambayo yakiiva hulainika upesi), pia ladha yake ni tamu sana. Kwa kifupi siku hizi kuepuka GMO ni ngumu sana kwani mimea mingi imeboreshwa ili kuweza kustawi kwa muda mfupi na kutoa mavuno mengi.
Samahani
GMO ndo nini kiongozi
 
Kwani kupatikana Njombe ndo isiwe GMO.! Mbegu [miche] zake umepata wapi?
Kwa zama hizi za utandawazi kubisha kitu bila kutafuta taarifa zilizozagaa sehemu mbalimbali ni upumbavu
 
Kwa scale ile sidhani kama ni natural, labda uniambie hao waburundi wanazalisha parachichi kwa ajili yetu tu wao hawali,
Acha ushamba na ubishi, hizi ni zama za utandawazi, tafuta taarifa kamili kuhusu unachokibishia..hizo parachichi ni mbegu asilia huko Burundi na Rwanda na maeneo jirani Kama Kigoma na Ngara.
Yapo mengi Sana nao wamepata soko hapa bongo.
Parachichi Kama zilivyo embe Kuna species mbalimbali kutokana na maeneo.
 
Punguza comment uongo kama hujui chochote.
Hii ni Grafting broo.
Unakumbuka asexual reproduction uliyofundishwa form 3?

Karibu SHAMBANI.
PUNGUZA KUONGEA USIVYOVIJUA.

Parachichi GMO na MCHINA katoka wapi?
Muwe mnatafuta kwanza taarifa ndio mje m comment.
Mmekaa kwenye lami huko mna comment tu "MCHINA" mara "GMO"

Karibu mjifunze
1. Kwanini makubwa
2. Kwanini hayana nyuzi

View attachment 2101973

#YNWA
Grafting huwa tunafanya hata kwenye miche ya michungwa mbona huwa haileti tofauti ya tunda ?
Hebu eleza kwa nini acicado hizo hazina nyuzi na ni kubwa
 
Acha ushamba na ubishi, hizi ni zama za utandawazi, tafuta taarifa kamili kuhusu unachokibishia..hizo parachichi ni mbegu asilia huko Burundi na Rwanda na maeneo jirani Kama Kigoma na Ngara.
Yapo mengi Sana nao wamepata soko hapa bongo.
Parachichi Kama zilivyo embe Kuna species mbalimbali kutokana na maeneo.
Sijabisha ila kama unasoma comments zangu nafanya kuhisi tu kwamba chances za hizo avocado kuwa genetically modified ni kubwa ,

Kwenye hizi zama za utandawazi ndio hatari zaidi maana wagu wanajaribu kuficha codes kwenye vitu obvious, unachotakiwa ni kutumia common sense tu na ndio nilichomaanisha na kufanya.

Engineering inayotumika kwenye Gmo ina lengo la kuboresha production na quantity, huku iki compromise quality, tuliyokuwa tunayaona kwenye kuku broiler tumeyaona kwenye apples , embe, zabibu nk, sishangai kuyaona kwenye avocados.
 
Kweli kbs Maparachichi natural hayana tabia ya kufanana complete kutoka mti mmoja na mwingine yanakuwa na kautofauti flani. Lakini haya ya kijani yanafanana sanaa utafikiri yote yametoka mti mmoja lazima apo kuna kaartificial flani ndani yake tusidanganyane apa.
 
Back
Top Bottom