Himaya ya kirumi(Roman Empire) haijawahi kutawala dunia

Himaya ya kirumi(Roman Empire) haijawahi kutawala dunia

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwa nini watu wengi huwa wanaizungumzia Roman Empire kama himaya kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani au iliwahi hata kuitawala dunia wakati uhalisia ni tofauti kabisa?

Roman Empire kwa kipimo chochote kile sio mojawapo ya himaya kubwa duniani, hii ni Himaya iliyochukua eneo la Ulaya magharibi tu kwa ukubwa pamoja na Uturuki na mashariki ya kati kwa chache.

British Empire ndio Empire kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani ikifuatiwa na ya Wachina na Mongol.
 
Kwani vita ya 1&2 (wwI & II) zilipigwana na Dunia nzima.
Roman empire ilitawala mda mrefu na kutawala wababe wote wa Dunia, Uingereza ilitawala mda mfupi tena kwakupewa baada ya vita ya pili ya Dunia.
 
Kwa kipindi kile ilitawala dunia ndio maana sehem zilizo kua zina watu wengi ziliwekwa chini ya roman empire kamsome vizuri Julius Caesar ndo utajua.Tawala zilizo wahi kuitawala dunia ziko nne tu na Roman ndo ilikua ya mwisho na ilikua na nguvu sana ukitofaitisha na kipindi cha Alexander the great.
 
Mkuu unatakiwa ujue kuwa huwa inasemwa kuwa walitawala dunia 'iliyokuwa inajulikana kwa wakati huo". Na kumbuka kwakuwa wao wenyewe ndio waliandika na hawakuwa wanajua sehemu nyingine zaidi ya wao walipokuwa basi walikuwa sawa kimantiki.

Lakini kadiri siku zilivyoenda na sehemu zote za dunia kujulikana basi kauli ya kwamba walitawala dunia inawatatanisha msioweza kung'amua nilichoandika kwenye aya hiyo ya kwanza.
 
Eneo la mediterranian hadi middle east ndio lilikuwa civilized na lenye ushawishi.
America yote hakukuwa na la maana, hadi wazungu walipokimbilia huko.
China na mbali kote kulikuwa hakuna ishu. Hata ukisikia mjerumani katWala Tanganyika haimaanishi kila familia ilijua katawala.

Utawala wa uingereza ulikuwa ni soft tu tena weak huwezi kulinganisha Roman empire ambayo iligawa eneo lote katika majimbo ambalo kuna vikosi vya kijeshi vyenye nguvu kubwa na mfumo imara wa mawasiliqno huku magavana wote wakiripoti Italy kwa kaisali.
 
Inategemea dunia ilikuwa inamaanisha nini wakati ule na wakati huu. Hata British Empire haikufika kila mahali yapo maeneo mengi tu hawakufika, lakini tunasema walitawala dunia.
Kwa nini watu wengi huwa wanaizungumzia Roman Empire kama himaya kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani au iliwahi hata kuitawala dunia wakati uhalisia ni tofauti kabisa?

Roman Empire kwa kipimo chochote kile sio mojawapo ya himaya kubwa duniani, hii ni Himaya iliyochukua eneo la Ulaya magharibi tu kwa ukubwa pamoja na Uturuki na mashariki ya kati kwa chache.

British Empire ndio Empire kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani ikifuatiwa na ya Wachina na Mongol.
n
 
Kama waroma waliweza kupenyeza mfumo wa kalenda unaowezesha kujua muda na tarehe . Hii ni dalili kuwa waroma walikuwa na nguvu ya kuitawala dunia . Na mfumo huu wa kalenda ndo unatumiwa na nchi nyingi duniani mpaka leo na kesho ikiwemo marekani.
 
Pia legacy zao zimetapakaa dunia nzima

Namba za kirumi
Dini ya kirumi wao ndio walitengeneza mazingira isambae kote duniani.
Hata tabia ya askari kunyoa ndevu dunia nzima asili yake ni rumi.
Kalenda inayoongoza dunia.
Etc
 
Kwani vita ya 1&2 (wwI & II) zilipigwana na Dunia nzima.
Roman empire ilitawala mda mrefu na kutawala wababe wote wa Dunia, Uingereza ilitawala mda mfupi tena kwakupewa baada ya vita ya pili ya Dunia.
Vinaitwa vita vya kidunia kwa sababu kila taifa liilishiriki, either kwa kuwa uwanja wa vita, kutoa askari, pesa, silaha, mahitaji ya kivita n.k
Roman Empire ilidumu muda mrefu ila haikutawala wababe wote wa dunia.
Uingereza haikutawala muda mrefu ila ndio ambayo imetawala sehemu kubwa zaidi ya dunia na katika kilele chake baada ya vita vya pili vya dunia ilikuwa ikitawala robo ya dunia.
 
Kwa kipindi kile ilitawala dunia ndio maana sehem zilizo kua zina watu wengi ziliwekwa chini ya roman empire kamsome vizuri Julius Caesar ndo utajua.Tawala zilizo wahi kuitawala dunia ziko nne tu na Roman ndo ilikua ya mwisho na ilikua na nguvu sana ukitofaitisha na kipindi cha Alexander the great.
Roman Empire haijawahi kutawala dunia, Roman Empire ilitawala eneo la Ulaya magharibi tu, sehemu za Mashariki ya kati na Misri. Haikufika sub-saharan Africa, haikufika sehemu kubwa ya Asia kama huko India, China, Haikufika America.
 
Mkuu unatakiwa ujue kuwa huwa inasemwa kuwa walitawala dunia 'iliyokuwa inajulikana kwa wakati huo". Na kumbuka kwakuwa wao wenyewe ndio waliandika na hawakuwa wanajua sehemu nyingine zaidi ya wao walipokuwa basi walikuwa sawa kimantiki.

Lakini kadiri siku zilivyoenda na sehemu zote za dunia kujulikana basi kauli ya kwamba walitawala dunia inawatatanisha msioweza kung'amua nilichoandika kwenye aya hiyo ya kwanza.
Roman Empire walikuwa wanajua kuhusu China na Silk Road japo hawakuwahi kufika.
 
Roman Empire haijawahi kutawala dunia, Roman Empire ilitawala eneo la Ulaya magharibi tu, sehemu za Mashariki ya kati na Misri. Haikufika sub-saharan Africa, haikufika sehemu kubwa ya Asia kama huko India, China, Haikufika America.
Nadhani waliopita wamelkuelezea vizuri mkuu...
Kabla ya kina Columbus au vasco da gama kuijulisha Ulaya kuwa kuna sub Saharan Africa au America. Hizo sehemu hazikuwa zikijulikana wala kuna kuwa na significance kubwa kwenye maendeleo ya dunia ya kipindi hicho..

Hivyo "dunia" ya kipindi hicho ilikuwa ni Ulaya, mashariki ya kati na Asia..

Japo ni kama nakuelewa unapoisema Roman Empire kiutawala maana sikuwahi kusikia kama ilifanya extension hadi Asia. Japo yote haya yanahitaji historical facts sio ni nini tunahisi
 
Back
Top Bottom