Himaya ya kirumi(Roman Empire) haijawahi kutawala dunia

Himaya ya kirumi(Roman Empire) haijawahi kutawala dunia

Kwa nini watu wengi huwa wanaizungumzia Roman Empire kama himaya kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani au iliwahi hata kuitawala dunia wakati uhalisia ni tofauti kabisa?

Roman Empire kwa kipimo chochote kile sio mojawapo ya himaya kubwa duniani, hii ni Himaya iliyochukua eneo la Ulaya magharibi tu kwa ukubwa pamoja na Uturuki na mashariki ya kati kwa chache.

British Empire ndio Empire kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani ikifuatiwa na ya Wachina na Mongol.
Screenshot_20240821-080524_Biblia.jpg

amri inatolewa mahali mtu anapotawala angekuwa hatawali dunia nzima angepata wap mamlaka ya kuagiza watu kama hapo juu?
 
Roman Empire haijawahi kutawala dunia, Roman Empire ilitawala eneo la Ulaya magharibi tu, sehemu za Mashariki ya kati na Misri. Haikufika sub-saharan Africa, haikufika sehemu kubwa ya Asia kama huko India, China, Haikufika America.
Hizo ndio sehemu kubwa sasa miaka hiyo , Sehemu nyingine hakuna faida huku Africa kulikuwa na mapori .
 
Kipindi hicho Africa wangetawala nyani maana,population ilikuwa ndogo sana ukiondoa misri,kipindi hicho dunia ilijirundika Eurpe na Asia na Egypt,maeneo mengine hayakuwa yanevumbuliwa au kujulikana au yalikuwa na watu wachache hence low impact
Dunia ilikuwa kubwa tu China-Han dynasty ilikuwa inastawi, India kulikwa empires zao wanauza spices na gold sio poa,
 
Hizo ndio sehemu kubwa sasa miaka hiyo , Sehemu nyingine hakuna faida huku Africa kulikuwa na mapori .
Umewahi kusikia kuhusu silk Road iliyoanzia China?
 
Nadhani waliopita wamelkuelezea vizuri mkuu...
Kabla ya kina Columbus au vasco da gama kuijulisha Ulaya kuwa kuna sub Saharan Africa au America. Hizo sehemu hazikuwa zikijulikana wala kuna kuwa na significance kubwa kwenye maendeleo ya dunia ya kipindi hicho..

Hivyo "dunia" ya kipindi hicho ilikuwa ni Ulaya, mashariki ya kati na Asia..

Japo ni kama nakuelewa unapoisema Roman Empire kiutawala maana sikuwahi kusikia kama ilifanya extension hadi Asia. Japo yote haya yanahitaji historical facts sio ni nini tunahisi
Roman Empire haikugusa India na China ambazo walikuwa wanajua zipo na hadi bidhaa zao zilikuwa zinawafikia kupitia network ndefu ya biashara ya Silk Road.
 
Eneo la mediterranian hadi middle east ndio lilikuwa civilized na lenye ushawishi.
America yote hakukuwa na la maana, hadi wazungu walipokimbilia huko.
China na mbali kote kulikuwa hakuna ishu. Hata ukisikia mjerumani katWala Tanganyika haimaanishi kila familia ilijua katawala.

Utawala wa uingereza ulikuwa ni soft tu tena weak huwezi kulinganisha Roman empire ambayo iligawa eneo lote katika majimbo ambalo kuna vikosi vya kijeshi vyenye nguvu kubwa na mfumo imara wa mawasiliqno huku magavana wote wakiripoti Italy kwa kaisali.
Umeitajaje Amerika (new world)kwenye Roman empire wakati ilikuwa haijajulikana!
 
Itakuwa walikuwa wanazumgumzia ulimwengu wao tu uliokuwa katika himaya yao.
ww sio kwamba ni muongo tu bali n mbishi piah........ulimwenguni mwote afu ww unasema utumbo gan sjui.......huwezi kukataa mamlaka ya Roma kutawala dunia na hata sasa Roma ya kidini tunatawala dunia ndo maana Nyerere mwinyi mkapa kikwete magu samia wote .....wameenda Roma kuna nini huko roma ??? ni kwa sababu roman tunatawala..........huwezi kuyakataa mamlaka na ushawishi wa Roma.
 
Kwa nini watu wengi huwa wanaizungumzia Roman Empire kama himaya kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani au iliwahi hata kuitawala dunia wakati uhalisia ni tofauti kabisa?

Roman Empire kwa kipimo chochote kile sio mojawapo ya himaya kubwa duniani, hii ni Himaya iliyochukua eneo la Ulaya magharibi tu kwa ukubwa pamoja na Uturuki na mashariki ya kati kwa chache.

British Empire ndio Empire kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani ikifuatiwa na ya Wachina na Mongol.

Roman emprire sio tu inasifika kwa ukubwa wake, bali pia ni utawala uliotawala muda mrefu zaidi na athari zake zipo hadi leo.

Kwa mfano falsafa ya uongozi na dhana ya kidemokrasia wao ndio waliokuwa na kufanya ushawishi mkubwa na ndio hadi Leo tunaongozwa na dhana hizo.

Ni utawala ulianza miaka 300 na kuanguka mwaka 1453.

sijui ni karne ngapi hapo.

Historia yaonyesha yesu alikuja kuupinga utawala huu lkn walishindwa, Muhammad pia alikuja si kuleta dini bali kuupinga utawalawa huu. Na kafanikiwa kusimamisha kwa karne zake mbili za kwanza na kujumuisha sehemu kubwa ya Kusini-Magharibi mwa Asia, Afrika Kaskazini, na Uhispania. Wakiwaondoa dola ya warumi.

Kwa upande dola ya Roma ndio yenye nguvu ya kiutawala duniani hadi leo chini ya Vatican

View: https://x.com/MfalmewaX/status/1825456563353489737?t=xDW6dh0aCR1avTB2FmGpiQ&s=08

Umewahi kusikia kuhusu silk Road iliyoanzia China?
Ilisambaa mpaka wapi ? Empire ili iwe kubwa kutawala kidunia lazima iweze kwenda nje ya mipaka hata mabara tofauti.

Himaya kubwa ni ile inayoweza kutawala kuvuka mipaka mfano mfumo wa calendar watu wanatumia wa Roma karaibia 87% ya dunia .

Hizo himaya za sehemu moja haziwezi kuwa watawala wa dunia ni sawa na lugha ya kitaifa , kichina kina wazungumzaji billion 1.1 ila French wapo hata mil 400 hawafiki , ila French ni lugha ya kimataifa kuliko kichini kwa sababu ya cross-boarder kuna nchi Africa zinaongea kifaransa kama lugha ya taifa ila kichina ni kwao tu basi .​
 
ww sio kwamba ni muongo tu bali n mbishi piah........ulimwenguni mwote afu ww unasema utumbo gan sjui.......huwezi kukataa mamlaka ya Roma kutawala dunia na hata sasa Roma ya kidini tunatawala dunia ndo maana Nyerere mwinyi mkapa kikwete magu samia wote .....wameenda Roma kuna nini huko roma ??? ni kwa sababu roman tunatawala..........huwezi kuyakataa mamlaka na ushawishi wa Roma.
Roma iliitawala na inaitawala dunia katika ndoto zako, Ukatoliki ungekuwa unatawala dunia Papa asingekuwa anawaambia Russia, Israel, Sudan na Congo waache vita halafu wamuone kama kinyago tu. Huko China, India, Iran, Russia na sehemu kubwa Asia ukiwaambia habari za ukatoliki au Papa wengi wanakuona kama hamnazo tu.
Marekani imekuwa na Marais 47, wawili tu ndio Wakatoliki mpaka sasa.
 
nmekubali mawazo yako na nmeamua kukubaliana na ww kuwa hatutaelewana kwa hili.......i have agree to des-agree with u.
 
Roman emprire sio tu inasifika kwa ukubwa wake, bali pia ni utawala uliotawala muda mrefu zaidi na athari zake zipo hadi leo.

Kwa mfano falsafa ya uongozi na dhana ya kidemokrasia wao ndio waliokuwa na kufanya ushawishi mkubwa na ndio hadi Leo tunaongozwa na dhana hizo.

Ni utawala ulianza miaka 300 na kuanguka mwaka 1453.

sijui ni karne ngapi hapo.

Historia yaonyesha yesu alikuja kuupinga utawala huu lkn walishindwa, Muhammad pia alikuja si kuleta dini bali kuupinga utawalawa huu. Na kafanikiwa kusimamisha kwa karne zake mbili za kwanza na kujumuisha sehemu kubwa ya Kusini-Magharibi mwa Asia, Afrika Kaskazini, na Uhispania. Wakiwaondoa dola ya warumi.

Kwa upande dola ya Roma ndio yenye nguvu ya kiutawala duniani hadi leo chini ya Vatican

View: https://x.com/MfalmewaX/status/1825456563353489737?t=xDW6dh0aCR1avTB2FmGpiQ&s=08

Nafahamu Roman Empire imedumu muda mrefu sana, imekuwa na Impact kubwa kwa dunia kupitia ukoloni wa Ulaya ambao ulisambaza concepts na tamaduni zake sehemu kubwa ya dunia baada Roman Empire kuanguka Hiyo haiondoi ukweli kwamba Roman Empire haikuwahi kutalawa dunia na sio pia mojawapo ya Empire kubwa kwa idadi ya watu au eneo kuwahi kutawala dunia.

Pia Vatican haitawali dunia. China, India, Russia, Korea, Japan, Vietnam, Thailand na sehemu kubwa ya Ulaya hawana habari za Ukatoliki, Vatican au papa na wala hawatilii maanani hayo mambo ya Ukatoliki na Papa.
 
Historia ni vifurushi vya uongo vinavyo ongelea Mambo yasiyowahi kuwepo yakizungumzwa na mtu asiekuwepo wakati huo.
 
Umeitajaje Amerika (new world)kwenye Roman empire wakati ilikuwa haijajulikana!
Ndio maana nimeitaja nje ya ushawishi wa Roman empire. Huko walikuwa wanaishi waporipori. Hata hivyo US mfano eneo lenye watu ni chini ya40% ya ardhi yote ya Marekani. Kwingine ni milima na mapori tena hao watu wenyewe 90% ni wahamiaji kutoka hukohuko ilikokuwa inatawala Roman Empire.
 
Sio hivyo tu hata vita iliyopigwa ulaya tu wanaita vita vya dunia
 
Ndio maana nimeitaja nje ya ushawishi wa Roman empire. Huko walikuwa wanaishi waporipori. Hata hivyo US mfano eneo lenye watu ni chini ya40% ya ardhi yote ya Marekani. Kwingine ni milima na mapori tena hao watu wenyewe 90% ni wahamiaji kutoka hukohuko ilikokuwa inatawala Roman Empire.
Wazungu waliovamia na conquer America waliua Red Indians zaidi ya milioni 50, ni mojawapo ya genocide kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani.
 
Roman Empire ilichukua mambo mengi kutoka kwa utawala wa Wagiriki. Democracy, Philosophy, Michezo,
Rome iliitwaa na kuitawala iliyokuwa Hellenic Empire. Hivyo Rome ilijijenga juu ya ule utawala wa Kigiriki na kujumuisha zilizokuwa tamaduni zake.

Pamoja na hayo uliyosema, pia Rome ilikua na yake mengi tu iliyorithisha kwa Ulaya
 
WORLD kwa zama zile walikua wanamaanisha maeneo ya dunia wanayo ishi na kuyajua watu wa Ulaya

Wakati ule walikua hawajui au wanajua kwa uchache sana kuhusu Afrika, Asia, Amerika nk
 
Back
Top Bottom