Hip hop Facts Thread



Album ya kwanza ya AY kama solo ilitoka mwaka 2003 ikiwa na classics kama Raha tu, Machoni kama watu na Safi hiyoo.
 
Hiyo list namashaka nayo... Eminem juu ya Nas na Notorious na huyo jigga kaingiaje top 5.kwa Tupac wapo sahihi kabisa.
 
According to billboard awa ndio mcs wakali kuwai kutokea duniani




1. BIG POPA

2. Jay Z

3. Eminem

4. Rakim Allah

5. Nas

6. Andre 3000

7. Lauryn Hill

8. GhostFace Killa

9. Kendrick Lamar

10. Lil Wayne
siwezi kushangaa kutoona uwepo wa 2pac coz 2pac ni wa-kipekee,sayari ya pekee hapo hakuna wa kumlinganisha na 2pac labda kwa mbali sana rakim anafuata
 
Songalaeli Joseph Mwagala aka Songa ni rapper kutoka Singida ambaye yupo chini ya label ya Tamaduni Muzik. Anaunda pia kundi liitwalo Miraba Minne akiwa na wenzake P The MC, Nash MC na Zaiid. Songa ni miongoni mwa rappers wapya Tanzania wanaofanya vizuri sana.

Amesimama kwenye misingi yake ya Hiphop tangia day one, naweza sema ni moja ya ma-mc wakali kabisa kutokea kizazi cha sasa.



Tazama video niliyounganisha uelewe kipaji chake.
 

Attachments




Rapa bora kabisa LANGA alikuwa na biff kubwa kati yake na J Moe. Chanzo cha biff lao ni J Moe kumchana kwenye wimbo wake wa Jipange kuwa anatumia madawa ya kulevya...

J Moe '' amani kwa kaka voda milionea waambie wadogo zako waache poda wale mmea"

Langa kwenye wimbo wa 'Gangstaa' akajibu "amani kwa kaka voda milionea mwambie mo aache ushoga na umbea"

Baada ya Langa kujitangaza kaacha kula unga alitaka kufanya wimbo na J Moe ila Moe akakataa, ila aliachia huo wimbo huku akirejea ule mstari kwa kusema " amani kwa kaka voda milionea mwambie Moe nimeacha poda sili mmea"

Licha ya kupambana na kuacha madawa ila alidanja kwa overdose.

wimbo bora kabisa toka kwa Langa kwa upande wangu ni Kifo, Jela Au Tahasisi huu hapa
 

Attachments




Nash MC aka Zuzu ndio rapa wa sasa anaetumia kiswahili fasaha zaidi kwenye tungo zake.
Simwelewi kabisa huyu jamaa.
 

Kwangu ni rafiki WA kweli
 


Zaiid aka Zaidi Yao ni rapa mwenye undugu na mwanzilishi wa Kwanza Unit Crew Zavara Mponjika au zamani alijulikana kama Chief Rhymson aka MwanaVina.

Zaiid anamuita Zavara mjomba, pia zaidi ni mdogo wa mtangazaji maarufu Soud Mnete.
 
Nuff said
 
RassKass nae ana flow ya hatari.
 


Billboard ni source makini ukitaka kupresent data za music, na hakika wamefanya research kabla ya kuja na hiyo list man.[/QUOTE]
Billboard is industry centric, kwenye hiphop you have to consider loco and underground MCs, yani pamoja na ufahamu wako kwenye hiyo list kumkosa mtu kana krs-one haikupi shaka?

Fuatilua hiphop vizuri, na hiphop ya kweli haiko billboard wala kwenye mainstream media....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…