Hip-hop freestyle battle : special thread

Hip-hop freestyle battle : special thread

Oy! Oy! Oyiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!
Huu ni uwanja special kwa wana wanaofeel hip-hop, kama we nimkali WA freestyle Kama ni mc Una ngoma zako ziangushe hapa wana wazisikie.

Wana wa michano kuchanana no matusi Karibu tuchane tusukume gurudumu la hip-hop.

Yeah!! Mike Cheki

Kamwe sitoshinda bubu, Nina gadhabu za kutosha..... ///
Mchumba usilete gubu, mi ndo babu ninapambana na Maisha... ///
Macho kwenye ruzuku, ukizubaa unafichwa.. ///

OK! Waharibie
Mmmmh ,hapa kuna dalili ya kuibiana idea na mistari
 
..
Sometimes it's all abt the message not the Rhymes. Matter of fact I could do the ABAB rhyme pattern to finish my 16 bars
But fbomb rhymes with nepalm and it would made a hella lot more sense.....you know bomb and nepalm
 
jamani mashabiki!
shuka shuka

ata beat aijaanza!
shuka shuka

ata sijaanza kuchana!
shuka shuka

siimbi bongo fleva/ kweny beat ntawapoteza
shuka shuka

Aaaah! sishukiiii!
 
jamani mashabiki!
shuka shuka

ata beat aijaanza!
shuka shuka

ata sijaanza kuchana!
shuka shuka

siimbi bongo fleva/ kweny beat ntawapoteza
shuka shuka

Aaaah! sishukiiii!
Hahaha
 
Ngoja nikumbushie enzi zangu



"Tulianza kwa kupanga,
Kupoteza wanaopinga,
Upinzani kuutwanga,
Kwa mbinu zetu za kijinga,
Tukayaona ya Kitwanga,
Bungeni akitinga,
Kichwani pombe ziko pwanga,
Mi pointi kapuyanga

Tunayaona ya makonda,
Mbinu zote zilizopinda,
Madawa anayaponda,
Hofu kwake imetanda,
Mishe zake zimedinda,
Watu wengi wamponda,
Hivi punde atapanda,
Kizimbani huyu makonda
Kwa mbowe atasanda,
Manji atakaza mkanda,
Gwajima hatozindaa
Joto limepanda
Hii vita atashindaa....



Wareeeeeeeeee wolllloooooooo.....
Hip hop kwa damu mazwee
 
..

It's okay... Give us some bars bruh.
Start a whatsapp group ili watu tuje tu battle kwasabab kwa kuandika tu utapata ma god mc kibao ila hujui delivery yako wewe utaimagine flow yako lakini mwenzako alikuwa anaflow kama iggy azaelia


So anzishen group whatsapp watu wabattle na watu wengine wa judge na vile vile kwa kuandika huez jua kama ni freestyle inawezekana mi nimeandika verse yang toka niko form four na nimekuwa nikiiperfect nikiiweka humu si watu mtajua im the new j.cole

Hayo ni mawazo yang tu
 
Start a whatsapp group ili watu tuje tu battle kwasabab kwa kuandika tu utapata ma god mc kibao ila hujui delivery yako wewe utaimagine flow yako lakini mwenzako alikuwa anaflow kama iggy azaelia


So anzishen group whatsapp watu wabattle na watu wengine wa judge na vile vile kwa kuandika huez jua kama ni freestyle inawezekana mi nimeandika verse yang toka niko form four na nimekuwa nikiiperfect nikiiweka humu si watu mtajua im the new j.cole

Hayo ni mawazo yang tu
Atuwekee link tuje tuchanike[emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
(Safii acha Tupige Bla blaa hapa ama Nin!)

Mimi Sii Sultan, Hata Niitawale Zanzibari,
Tunaicheza Kamari mtaan, Ili tuivuke Bari,
Maisha sii Shwari, Hata Sangoma Kafeli?,
Tunaufahamu utamu wa Ugali, Lazima tuusake shambani.

Bora nife masikini, Kuliko kupewa na manzi,
Lazima niwe makini, Nisije jivika Kitanzi,
Namwamini Nungu, Kamwe Sihusudu Majungu
Daima Niwe na Changu, Tena kwa nguvu zangu.

😀😀😀 Nadhani tuishie hapa au sio. Kisingeli Hoyoooo( NO NO NO NOO Hip-Hop Hoyeee)
 
Hip hop ufedhuli,huu ukweli chukua
Kariri yangu makali,na njia kujitwalia
Mwajisifu kwa unguli,huku pua mwangukia
Rudini kwenye asili,na jamii kuihudumia

Mmejaa majigambo,kwa kazi kujipakazia
Uzwa zwa na tambo,huku mkijitutumua
Uongo usambo,mashairi kujiitia
Eti hip hop nini,utamaduni mwasemea

Elimu na watu wake,hip hop kwangu makapi
Mashairi na sifa zake,wajuzi wako wapi ?
Mwenye hoja aweke,usibweke kama papi
Hip hop uhuni teke,ukweli huu ukwepi
 
Naona mna jiresi, kwa vina vya Kipemba

Uwezo wenu mwepesi, kama vivazi vya Odemba

Tayari mnastahili kesi, kitu hamjui kisha mnaremba

Mvumbo moto wa gesi, tunajuana kwa vilemba

Anaebisha mwache aje, nimmeze kama Anaconda

Watoto watanitambuaje, wakati wanaimba moyo kidonda

Hizi harakati kama Mugabe, hawawezi watakonda

Wanasema Mvumbo mbabe, kisa nawataja kama Makonda
 
jf nyota,sijatoka,nipo mtaani nasota,ukiropoka ropoka,jela panakuita,ndio zamahizi,ni sirikali ya machizi,unga uzi,mwanangu ila usiunge ngada,ukaishia soba,home ulete msiba......
 
Yoo namba moja kushika sio kwa kasi ya kobe/
Maji yakimwagika usizoe utazoa tope/
Mwenzako akisali; sali kabla hujaswaliwa/
Pandisha morali morani aliyetahiriwa/
Mistari sii haba vina vinajaza kibaba/
Medani za shaba nnapo simama kama langa/
Mcee's wachanga wanajivika usupastaa/
Kimbilia suti na nepi bado hujavaa/
Mali imepata daftari hupotea bila habari/
Nimechoka kuunguza utambi naunguza hadi kibatari/
Kwa mgongo wa chupa mafuta usinipake/
Mdomo usiwe mtumwa uliyeponzwa na ulimi wake/ ...
Hivi ndivyo nnavyofanya/
Mama unayemlea mwana kumkemea sio kumkanya/
Yees nnayezikosha nambaa.../
Kwenye giza siwezi kupotosha mwangaaa//
oooooiiii......
 
Serikali aina shamba, kapuku nalia njaa
Msukuma anajigamba, 2020 namkataa
 
Back
Top Bottom