HIP HOP FREESTYLE: Maneno yako ya mwisho kabla sijafa

HIP HOP FREESTYLE: Maneno yako ya mwisho kabla sijafa

Scars

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
48,055
Reaction score
116,512
Maneno yako ya mwisho yatakuwaje endapo akatokea mtu akakuwekea bastola kichwani kisha akakupa nafasi uongee maneno yako ya mwisho kabla hajakuua??

Naanza na mimi

Je nitatamani niwaombe msamaha wale wote niliowakosea kabla sijafa?, ili nikifa niende pepo yenye furaha isiyo na maafa/

Je nitajutia maamuzi yangu niliyoyafanya kipindi ambacho nina afya, au nitasizi na kukomaa kimafia?/

Au nitapiga kelele kuomba msaada kwa watu niepukane na kifo, Au kupiga dua kushirikisha malaika wamshushe kristo/

Ugekua wewe ungeweza kumsamehe hadi muuaji ambaye atayateketeza maisha yako, au roho yako itakua ngumu kufunguka kama lango la gereza la keko/

Utaweza kuyafanya hayo ili kuipata pepo uliyoaidiwa na dini yako, au utajivika ukauzu kupuuzia habari za dini na mambo ya upako/

Utakumbuka kutaja ID yako ili tukukumbuke nasisi kwa mchango wako, au hutajali utafanya mambo kibinafsi kivyako vyako?/

Je utajutia kupoteza muda wako,,,kwa watu ambao hawajawahi kuweka muda wao kwa ajiri yako??/

Utakufa ukiwa bado unakinyongo na mimi, kwa zile mada nazozipinga hapa jamvini?/

Inamaana hujawahi kufurahishwa na mimi, hata kwa zile post za utani wa vituko mitandaoni?/

Please dont let me down, nami pia ni mtu japo ngozi yangu ni brown/

.............Mwisho.......

Usisahau kuweka na yako


Mvumbo Daby
Da'Vinci
kurlzawa
 
IMG_20191206_182318_517.jpeg
IMG_20191206_182308_007.jpeg
 
Mimi Shule iliua kipaji changu! Nimewahi kuwa karibu na wasanii kadhaa, lakini sikuupa Mziki nafasi! Mkuu km bado, fanya uzame studio
Mi mziki hua napenda kuchana just for fun sijawahi kuwa na kipaji cha kunifikirisha niende studio

Lakini kipaji hakifi unaweza ukaendelea kutwanga japo hakuna mpunga kwenye kinu
 
Nafurahi kuona wana mna show love, japo sina tungo za maana lakini mnanipa shavu/
Tungo zangu nachana kwa manati, kwa mzani na vina scar sikupati/
Junsi unavyo flow speed ka Fiati, mizani yako mind blow ka Baruti.

Wana tunakushoo lovu, sikumoja upate shavu/
Ukatambe kimabavu, mbele ya mces chakavu/

Scar si uongo unajua, mistari konkii kuitua
 
Tungo zangu nachana kwa manati, kwa mzani na vina scar sikupati/
Junsi unavyo flow speed ka Fiati, mizani yako mind blow ka Baruti.

Wana tunakushoo lovu, sikumoja upate shavu/
Ukatambe kimabavu, mbele ya mces chakavu/

Scar si uongo unajua, mistari konkii kuitua
Hahaahaa umetishaa
 
Back
Top Bottom