Kadgo
Nimezaliwa naye tumbo moja namuita pacha, mama ananiambia kanizidi dakika tu sio mwaka.../
Yupo hai hajafa hivi navyoongea, amenihasa amenifunza haswa nisije potea.../
Ni identical twins, two kings same blood same color same height and two beings.../
Sasa niende home alipotoka baba, na mama mzazi pia ndio root ya grandfather.../
Kwa raha ndugu yake upendo ndani ya familia, maisha kuongeza mwendo mienendo ikaanza tabia.../
Kufungua ukurasa madarasa yakafuatia, ikafika muda wa kuachana na pacha ambaye namuaminia.../
Siku moja niko stand nasaka mlungula, kosa jinsi niliyovaa nikavishwa misala ya kulwa.../
Kipigo cha mbwa mwitu nikashtuka siku kadhaa, siku muwekea bifu moyoni sikutaka balaa.../
Siku zikapita ikafika siku ya mnada, sokoni napita pembeni yuko siter na father.../
Ghafla mbele yangu akatokea pedeshee, mwenye visanga na kulwa na hakutaka nijitetee.../
Akaanzisha ugomvi mbele ya umati father akaingilia, bwashee si akaitoa risasi dingi akaitoka dunia.../
Kwa macho nikishuhudia najuta kufafana, najua dunia ni njia kulwa acha unachofanya.../
Song: pacha