Hirizi ya Lwandamina yaonekana mwenyewe akanusha!!

Hirizi ya Lwandamina yaonekana mwenyewe akanusha!!

Hivi viongozi wa Yanga wana nini cha ziada wanachokihitaji kutoka kwa huyu jamaa???

Haiwezekani mtu tangu akabidhiwe timu hakuna siku hata moja timu ikafanya vizuri ,kila kukicha afadhali ya jana.

Inabidi viongozi waingilie kati suala hili ,wachukue uamuzi mgumu wa kuvunja mkataba naye tu maana hakuna namna tumechoka kumvumilia.

Yaani ushindi kwetu imekuwa suala la bahati sana na hata ukifuatilia magoli yote tulioshinda mpaka sasa kwa mechi chache tulizocheza ni magoli ya kubahatisha sana.

Mashabiki tumechoka kwa kweli mtatuuua siku si zetu .

[emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57]
Weka picha.
 
Mkuu unachosema ni sahihi kabisa yaan sasa hiv ni bahati nasibu kocha kwetu ni hans van plujim sijui kwanni walimtoa huyu mzee mm namkubali sana roho iliniuma sana walivyomtosa sikuona sababu za msingi kabisa
 
Rwandamila mbona mzuri tu.
Tangu ligi ianze Yanga fc, wamecheza mechi nne.
Mechi mbili wameshinda vs Njombe na Lipuli
Mechi mbili wametoa sare vs Majimaji na Mtibwa.
Au inatakiwa Yanga washinde mechi zote...!
Kumbukeni timu zote zimejiandaa vizuri nazo pia zinahitaji ushindi.
Yanga wamecheza mechi tano mbili waneshinda (mji njombe na ndanda) tatu wametoa sare (lipuli, majimaji mtibwa) uwe na kumbukumbu kabla ya kukimbilia kupost
 
We jamaa una chuki na Lwandamina tu mana mda mwingi unaandika thread za kumponda. Team inacheza vizuri tu tatizo ufungaji ndo tatizo na ilo ni suala la washambuliaji sio la kocha.
Kama leo Buswita kakosa yeye na goli badala apige juu anapiga chini, Ngoma nae anapiga kichwa uku anafumba macho apo utamlaumu Kocha?
Ndivo kocha alivowafundisha
 
Hivi viongozi wa Yanga wana nini cha ziada wanachokihitaji kutoka kwa huyu jamaa???

Haiwezekani mtu tangu akabidhiwe timu hakuna siku hata moja timu ikafanya vizuri ,kila kukicha afadhali ya jana.

Inabidi viongozi waingilie kati suala hili ,wachukue uamuzi mgumu wa kuvunja mkataba naye tu maana hakuna namna tumechoka kumvumilia.

Yaani ushindi kwetu imekuwa suala la bahati sana na hata ukifuatilia magoli yote tulioshinda mpaka sasa kwa mechi chache tulizocheza ni magoli ya kubahatisha sana.

Mashabiki tumechoka kwa kweli mtatuuua siku si zetu .

[emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57]
Mkuu shida ya yanga haina mdhamini ukijitosa wewe kudhamini tutakushangilia na huyo kocha mzambia ataondoka na kuletwa kocha Mkali
 
Ila kumbuka Lwandamina tumekuwa naye tangu mwaka jana mzunguko was kwanza kipindi ambacho Manji hakuwa na maswahibu yoyote yale.

Lakini je hata hiyo mwaka jana alikuwa anafanya vizuri?
Ndio, Yanga chini ya Lwandamila wakati wa udhamini wa Manji ilikuwa inafanya vizuri.
Kumbuka zile mechi za mwisho Yanga ilishinda kalibu zote tena zilikuwa ngumu sana.
Nakumbuka mechi dhidi ya Azam na Mbeya City, mechi zilikuwa kali sana na Obrey Chirwa aliyekuwa katika kiwango kizuri alikuwa ndiye mfungaji wa mechi zote ngumu hadi Yanga ikawa bingwa.
Tatizo Yanga kwa sasa inakosa udhamini wa uhakika na sio kocha.

Amini hivyo.
 
⚽ una wenyewe na wenyewe ndio

Mnyama mwaka wetu huuu
 
Back
Top Bottom