Hisa za Kampuni ya kuchimba gas (Swala Tanzania)

Hisa za Kampuni ya kuchimba gas (Swala Tanzania)

akohi

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Posts
787
Reaction score
526
Wakuu mi naomba kujuzwa maana nilishitukiwa tu kuona kwenye tv ufunguzi wa mauzo ya hisa pale DSE.

Utaratibu wa kununua hisa ukoje kwa tuliochelewa?

Asante.
 
aliyeweka post. huna update. mbona zilitangazwa sana. na wameishafunga mda wa kuuza. siku ile ulikuwa uzinduzi............tena bei yao kama cjakosea ilikuwa tsh 200 per share..... ilitakiwa ununue certain minimum shares.... . ...anyway post yako it indicates that huna uelewa mzuri kuhusu mfumo wa shares........wasiliana na wadau tutakupa shule mkuu
 
kununua hisa moja sio chini ya mil 10.

Duh huyu jamaa sijui ni muongo au ana roho mbayaaaa, siku ya ufunguzi wa soko hisa1 ilikuwa ni Tshs 500, the following day dau likapanda hadi kufikia 500 kwa hisa1
 
Hisa za kampumi ya mafuta na gasi swala zilianza kuuzwa kwa mara ya kwanza mwezi mmoja uliopita,hivi sasa wale walionunua hisa hizo katika mauzo ya awali kwa tshs 500 @, hivi sasa wanaweza kama wanataka kuziuza hisa zao kwenye soko la hisa la upili ktk DSE kulingana na bei ya soko ambayo sasa hivi iko kati ya tshs 600 na 700 @.Wewe ambae hukuwahi kununua hisa za swala katika mauzo ya awali bado unaweza hata kesho kununua hizo hisa katika soko la upili la DSE kwa bei hizo hapo juu,bado hujachelewa kwa kuwa ukisubiri baadae zinaweza kuwa na bei mbaya kama unavyoona TBL na TCC hivi sasa. wasiliana na mawakala wa soko la hisa ili uweze kununua hisa za swala na makampuni mengine yaliyoorodheshwa katika soko letu dogo la hisa.:wof:
 
Siku moja nitawekeza huko. Ila naomba isije kuwa kama ile ndege yetu
 
Duh, huyu mjali tumbo hajielewi kabisa. Hivi kweli kwenye dunia kama hii ya leo ya utandawazi bado kuna watu aina hii. Kama huelewi kitu bora ukae kimya, au uulize maana ujito thamani kabisa.
 
hisa moja ilikuwa inauzwa sh 500 mkuu. baada ya kulist tu ikafika sh 600. na sasa hivi ni sh 625. Mimi nimewekeza huko kaka.
 
Wakuu mi naomba kujuzwa maana nilishitukiwa tu kuona kwenye tv ufunguzi wa mauzo ya hisa pale DSE.

Utaratibu wa kununua hisa ukoje kwa tuliochelewa?

Asante.

wasiliana na wakala anayetambulika na soko la hisa (DSE). Cheki na Solomon Stock Brokers-0714269090, wapo ppf hse morogoro rd/samora ave kwa dar. pia core securities wapo samora ave. kwa sasa zinauzwa TZS 625 kwa share ila mpaka mchana huu hamna wauzaji, asubuhi ndo ziliuzwa sana. kesho huenda wakapatikana.
 
SWALA=NICOL hapo ni patamu

umesema point. ila kwa swala mambo yatakuwa poa sana kwa wale walionunua mapema. walichofanya swala ni kutumia hali ya mvurugano wa gesi kujipatia pesa ya kuendeleza utafutaji. watanzania wengi walitaka kumiliki rasilimali za gesi na mafuta na ndo hapo swala wakachomekea.
 
Vp kuna minimum number ya kununua?
 
Akohi vp? Mbona umepotea? tangu ulivyoondoka Shelys sijakuona tena. Upo Dar au Mwanza?
 
wasiliana na wakala anayetambulika na soko la hisa (DSE). Cheki na Solomon Stock Brokers-0714269090, wapo ppf hse morogoro rd/samora ave kwa dar. pia core securities wapo samora ave. kwa sasa zinauzwa TZS 625 kwa share ila mpaka mchana huu hamna wauzaji, asubuhi ndo ziliuzwa sana. kesho huenda wakapatikana.

hiyo hisa nikinunua mimi ninafaidika vipi mdau
 
Back
Top Bottom