Hisa za NMB zimeshuka kwa 50% ndani ya miezi 12

Ishu ya mwalimu bank wala haina nguvu hapa ishu ni serikali kutoa pesa zake kwenye mabank ya biashara NMB ikiwemo na bado wasipokuwa wabunifu watayumba sana,wajipange kwakweli.

Tamko la Serikali kuhamisha account zake ni la January 2016, na kabla ya hapo trend ilikuwa ya kushuka.

Feb 2015, bei 4,300/- wakati Feb 2016 bei ni 2,200/-.

Kwa hiyo hiyo ya kuhamisha acc nayo siyo sababu, na sina uhakika kama kweli hilo zoezi limeshafanyika.



Sababu ninazoweza kuzifikiria ni:-
1. Ushindani wa kibiashara, benki nyingi Multinationals zilizokuwa hazitoi mikopo midogo midogo zimeanza kutoa, kwa hiyo zinakuja kupambana na NMB moja kwa moja

2. Mikopo inayofeli, watu wengi tumeshindwa kulipa mikopo kwa wakati, hivyo kupelekea hasara kwa mabenki husika, ukiangalia kwenye mahesabu yao utakuta impaired loans zinaongezeka kila kukicha

3. Mitandao ya simu kuja kufanya kazi za kibenki imepunguza sana fedha benki ilizokuwa inapata kama vile trensfer charges, withdraw charges, ATM charges etc etc. Ndiyo maana sasa hivi kila benki inajaribu kuwa na mobile banking ili kukimbizana na hizi kitu.

4. Ongezeko la mabenki kama alivyosema The Boss pia siyo la kubeza, na wote wanagombea soko moja

5. NMB imejenga jengo lake hapa karibu na Serena, ile ni investment kubwa sana na lazima kwa namna moja iathiri mzunguko wa fedha, mfano fedha ambazo wangewekeza kwenye Bonds, Bills au kuzikopesha zikaleta interest zimeenda kwenye kujenga, na ukute pia na wao wana mkopo wa hilo jengo (kama ni part financing ambayo ni obvious) watakuwa wanasevu riba pia.

Hayo ni baadhi tu.
 
pole ila shukuru tuu Mungu, maana ungenunua za nmb ungehuzunika mara 3 zaidi
 
Nashukuru kwa darasa ninalopata hapa.Naomba munielimishe kuhusu matarajio ya mabenk kushusha Interest rate baada serikali na taasisi zake kuhamishia Account zao kwenda BOT. Kwa sasa nadhari interest za benk kadhaa Ni 22%, kwa wale walio na ufaham mpana wa mambo haya ya kibenk wanaweza kupredict kama hii adjustment ya hizi rate yaweza kufanyika kabla ya next Financial Year? Ahsante
 
mkuu mbona hizi hisa zske zimeanza kushuka kwa kasi kuanzia mwaka jana kabla ya serikali kufanya huo uamuzi? na kama sababu ni hiyo mbona wenzao wa crdb wapo almost stable?
Kuna weza kukawa na sababu nyingi zinazopelekea kushuka kwa bei ya hisa za NMB, lakini hoja ya taasisi za serikali kupeleka pesa zao BOT lazima itakua ni mojawapo.

Kwakuwa sasa wewekezaji wanakadiria kupungua kwa faida ya NMB siku za mbeleni kutokana na NMB kupungukiwa na kiasi cha fedha ambacho alikuwa akizitumia kwenye masoko ya fedha kujipatia faida.

Sababu ingine inaweza kuwa ni mwelekeo wa serikali katika kubana matumizi lakini na mpango wa serikali wa kuhakikisha halmashauri pia zinaweka fedha zake BOT yaani Trasury Single Account.

Uwanzishwaji wa benki ya walimu unaweza kuwa umechangia kwa kuzingatia kwamba labda wateja wengi wa NMB ambao ni walimu sasa wataanza kupokea pesa zao kupitia benki hio, hivyo kuendelea kupunguza uwezo wa kifedha wa NMB.

Sababu zote hizi, pamoja na zingine zimepelekea watu kuamini kuwa faida ya NMB itapungua, gawio litapungua hivyo ni busara kuuza hisa kwa sasa, na supply imeizidi demand na matokeo yake bei ndio inashuka.
 

...Rai, keep up the good work ya kuelimisha watu humu. Ushabiki ni mwingi kwenye post za maana kama hizi humu, kiasi cha kuathiri objectivity ya thread nzuri kama hizi.

..."Mikopo inayofeli" ni umiza kichwa sana kwa mabenki hapa. Hivi karibuni, mabenki yamepoteza mamilioni ya fedha kwenye mikopo, na bado yataendelea kupoteza kutokana na mdororo wa uchumi unaoanza.

...Hili suala kwenye mikopo ndilo linalofanya riba iwe kubwa -hapa bado hujaweka mfumuko wa bei, gharama za uendeshaji, n.k.- na risk premium inapanda.
 
Kwanza kabisa, kwa hali ya kawaida inafaa tutegemee riba za mikopo kupanda hivi punde (in the shortrun) kutokana na kwamba mabenki sasa hayana pesa tena ambayo walikuwa wakiitumia kuizungusha na kupata faida kubwa iliopelekea ma CEOs kujilipa bonus. Kwakuwa sasa kutakuwa na uhaba wa pesa kwahiyo shilingi itakuwa na thamani kuwa nayo, kwahivo mkopaji atalazimika kuilipia riba kubwa kuipata. Lakini hili pia litasaidia kuimarisha sarafu yetu dhidi ya dola ya kimarekani.

Kwa kipindi cha mda mrefu,(in the longer run) tutaona mabenki sasa yakienda kushawishi wananchi kuweka pesa zao benki, yaani deposit mobilization, ambayo itaambatana na kupanda kwa riba za kuweka fedha benki yaani deposit rates,ambapo ma benki yatalazimika kuvutia wateja kuweka hela kwenye mabenki yao.Jambo hili litazua ushindani wa kweli kwenye sekta ya mabenki na hatimaye tutashuhudia riba za mikopo zikishuka huko mbeleni.
 
Jambo hili litazua ushindani wa kweli kwenye sekta ya mabenki na hatimaye tutashuhudia riba za mikopo zikishuka huko mbeleni.

...erique, nadhani tunajua ni kitu gani kinashusha riba katika mikopo.

...Haya ni maswali ya kujiuliza. Je, inflation itakuwaje wakati huo? Hivi interest nzuri kwenye deposits si itaongeza cost of funds? Tatizo jingine litakuwa risk premium.

...Ukiniuliza, nitakwambia kwamba riba hapa ni kubwa kwa kuwa gharama za uendeshaji benki ni kubwa (suala linaloweza kuwekwa sawa, kwa kiasi fulani, na ushindani katika soko), default rate, ukubwa wa kodi benki inazolipa, n.k..
 

Issue ya risk premium sio kitu pekee kinachopelekea riba za juu, isitoshe hivi sasa tayari credit reference bureau ambayo inasaidia mabenki kutambua risk profile ya mkopaji.Pamoja na project ya vitambulisho vya taifa itakapomalizika risk ya mkopaji itakuwa inafahamika na benki kwa kiasi kikubwa.

Uwepo wa riba kubwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa cost of fund, hao mabenki wenyewe wanalipa riba kubwa kwenye hizo pesa wanazotumia kukopesha.

Mfano, NSSf anaweka hela zake kwenye benki mojawapo na kwakuwa Nssf ni mteja mkubwa ana nguvu ya kubagain riba anayotaka kulipwa, yaani deposit rate. Na riba hii inaweza kufikia hata asilimia 17 hadi 18. Benki hio ndio atatumia hela za nssf kuzungusha ili apate faida, lazima atacharge lending rate ya kuanzia asilimia 20, ili nayeye akapate kumlipa nssf deposit rate ya asilimia 17 au 18.
 
...Sidhani kama hizo rates zitashuka. Moja, mabenki yanaenda pata defaults kadhaa tayari, hivyo kuwa makini katika kupunguza hasara na kulinda faida. Mbili, factor kadhaa za kiuchumi zinatakiwa kuonekana mwelekeo wake kabla ya maamuzi muhimu kama hayo.

...Next financial year will tell.

Note: Accounts hazijahamishwa, as such, zimepunguzwa! Thats my reading of things.
Disclaimer: Sina ufahamu mpana kwenye mambo haya!
 
...Nashukuru kwa mchango wako!

...Angalia pia nilipo quote post yako, nimeongeleo hayo.

...Vitambulisho vya taifa vitamaliza vipi risk? Au una maanisha vitasaidia ku identify na ku locate wateja? Je, tenure ya mtu katika ajira na ardhi si kipimo cha muhimu?

...Nadhani, quality ya miradi (business projects za watu) tunayofanya nayo ina maana sana katika ku determine risk.
 
Fedha ambazo zilikuwa zinakaa kwa muda mrefu kwenye mabenki ndio zimehamishiwa BOT, na ndio ambazo zilikuwa zinatumiwa na mabenki kujipatia faida.

Pesa kwaajili ya matumizi ya kila siku kwaajili ya hizi taasisi ndio zimebaki kwenye mabenki. Sasa pesa hizo zilizobaki kwenye mabenki haziwezi tumiwa na mabenki kwaajili ya kuzalisha faida.
 

...My thinking is, hata hizi zinaweza kutumiwa. Kwa maana ya kwamba, at any time, kutakuwa na kiasi fulani cha fedha.
 
...My thinking is, hata hizi zinaweza kutumiwa. Kwa maana ya kwamba, at any time, kutakuwa na kiasi fulani cha fedha.
Kwanza ni kidogo sana, kwaajili ya kukidhi mahitaji ya taasisi ya mwezi moja, Pili, unatumiaje fedha ambayo mwenyenayo anaitumia kidogo kidogo kila siku.?
 
Kwanza ni kidogo sana, kwaajili ya kukidhi mahitaji ya taasisi ya mwezi moja, Pili, unatumiaje fedha ambayo mwenyenayo anaitumia kidogo kidogo kila siku.?
...Je, huwezi ku determine ni kiasi gani on average kinakuwapo? kwa wengine fedha hiyo yaweza kuwa ndogo, lakini mamilioni kwa wengine, say, small business owners ni nyingi.
 

Bila kusahau frauds kubwa kubwa zinazofanywa na bank officials.
 
mkuu nimekukubali kwa theory zako, mwenyewe nilikua nadhani mabenki watapandisha rates za kukopesha ili ku discourage watu kukopa sana kwa kuwa hawana hela za kuwakopesha (serikali imezihamisha) na itapandisha rate za interest kwenye deposits pia ili watu wakaweke fedha, ila nikitafakari hii itakua ni majanga kwa uchumi wetu kwa kua watu watakua hawaanzishi miradi kwa wingi kwa kukosa mikopo au kuogopa riba kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…