Hisa za Vodacom Tanzania, imegeuka kuwa kitendawili kwa Tanzania

Kila kitu wanakufanyia mpaka kukuwekea hela bank kama watagawa.

Mmmh kwahyo kunakua na mahesabu mawili?moja kwa ajili ya wanahisa wa nje na nyingine kwa ajili ya wale originals?
Wote ni wanahisa hamna original wala copy ni aina tuu ya his a inakuwa tofauti
 
Tatizo mkuu unapokosea ni pale unapokazania kulilaumu soko baada ya kujilaumu wewe mwenyewe kutojua timing za soko la hisa... Wewe unalalamika unapata hasara wakati huohuo kwa hisa hizohizo wenzako wanapata faida
Mfano angetime akauza zilivyopanda we unadhan angepata sh.ngapi?
Yaani ye anachosema ni kuwa hata kama zimepanda faida ni kidogo yaani hailipi!!!!
 
Mfano angetime akauza zilivyopanda we unadhan angepata sh.ngapi?
Yaani ye anachosema ni kuwa hata kama zimepanda faida ni kidogo yaani hailipi!!!!
Mkuu sina hakika kama ni mfatiliaji sana, IPO ya swala ndani ya miez miwili bei ilishoot toka 500 hadi 2000, yan mara nne kwahyo mjanja kama aliweka milion 1 tu ndan ya miez miwili alipiga milion 4.. Ipo ya DSE ndani ya kipind kichache bei ilidouble, nashindwa kuelewa faida chache kivipi.. Ndomana nawaambia msichukie soko wala msilaumu soko, jifunzeni tu timing, kwenye soko la hisa pesa zipo nying tu
 
Mfano angetime akauza zilivyopanda we unadhan angepata sh.ngapi?
Yaani ye anachosema ni kuwa hata kama zimepanda faida ni kidogo yaani hailipi!!!!
Jamaa analaumu soko halina faida kwasabab limewahi kumtia hasara, mimi hata siku moja siwezi kulilaumu soko la hisa kwasabab nature yake ndo ilivyo ili wajanja wapate lazma wajinga wasiojua timing wawepo kuwawezesha wajanja kupata faida sokoni..
 

mkuu uko vema
nashukuru kwa ufafanuzi
 
Sio mzoefu sana na haya mambo mara kwanza nilimshuhudia mzee wangu alinunua hisa za Precision Air kipindi hiko sasa sikujua hata alipata faida kiasi gani naendelea kujifunza mkuu.......na nishakuelewa kuwa kikubwa ni timing na uangalie hali ya siasa na mwelekeo wa uchumi wa nchi
 
Jamaa analaumu soko halina faida kwasabab limewahi kumtia hasara, mimi hata siku moja siwezi kulilaumu soko la hisa kwasabab nature yake ndo ilivyo ili wajanja wapate lazma wajinga wasiojua timing wawepo kuwawezesha wajanja kupata faida sokoni..
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] sawa mkuu nimekupata,kikubwa ni ujanja!!
 
Ila mkuu gawio si linagawiwa kulingana na idadi ya hisa ulizo nunua..mfano mtu aliye nunua hisa 5000. na aliye nunua his 10000 watapata ratio sawa ya gawio???
Gawio linatokana na idadi ya his a ulizonazo.mwenye nyingi ndio mwenye gawio kubwa.
 
Mkuu troll umenipa elimu kubwa sana siku ya Leo tarehe 20.04.2017...


Nimesoma comments zote hakika wewe ni Gwiji ... Barikiwa
 
Nashukuru mkuu kama umenipata, pia napenda kukutia moyo usiogope soko la hisa, ila unapowekeza inabid kuwekeza kwa uangalifu, precision air was not a good investment tangu wanaingia IPO walikuwa na madeni ya kutisha na walikuwa wanapata hasara mfululizo, sasa hivi hakuna mtu anaetaka kununua hizo hisa sokoni... Unatakiwa tu kupembua vizur ntakupa mfano mmoja au miwili.. Ujenzi wa uwanja wa ndege terminal 3 huenda ukaongeza sana idadi ya ndege na wasafiri na kampun ya Swissport inayojihusisha na kuhandle mizigo ipo listed DSE huenda ikawa ni habari nzur kwa Swissport kupata mapato zaidi na faida zaid kwahyo unaweza ukaiweka kwny consideration na unaponunua haununui tu kwa kukurupuka unaangalia na bei ya hisa kwa wakati huo na muda unaotaka kununua kama ni sahihi. Mfano mwngne kampuni ya DSE siku za usoni makampun meng sana yatakuwa listed that means more revenue na profits kwa dse nayo unaweza ukaiweka kwenye consideration. Kama crdb sasa hiv inatrade 185 ikiwa na market capilization ya around bil 485, ambayo kiukweli ni undervaluation kubwa sana inayofanywa na soko, kwahiyo crdb sasa hivi huenda ikawa ni nzuri kuiweka kwny consideration kwasabab unainunua ikiwa very low at 185 with greater probability kwamba itarise... Soko la hisa ni tamu sana ndugu zangu wala tusijivunje moyo kuwekeza kwenye hisa. Tena kipindi hiki cha magufuli ambacho kila mtu analalamika hana hela soko ndo linakuwa zuri zaidi kwasabab bei za hisa zinashuka wauzaji ni wengi kuliko wanunuaji ambapo ni fursa sasa kwa wajanja kuweza kununua hisa za makampun mazuri kwa bei rahisi
 
Nakuelewa sana mkuu Mkuu Troll.. Mi hisa za Precision zimenifanya kitu mbaya sana..
 
[emoji106] [emoji106] safi sana......sasa kwa kampuni kama voda ambayo nayo inasemekana ina madeni lukuki kama hisa zao tu zipo IPO wanauza 850 zikifika DSE sizinaweza kushuka watu wakapata hasara?
Ishu nyingine ni kuwa ninaponunua hisa ni lazima nianze na hela kubwa ili ninapotaka kuuza au mwisho wa mwaka nipate gawio kubwa?
 

Kaka mkuu, kusema ukweli Vodacom huwezi kufananisha na Precision Air kwasababu precision ni loss making company wakati vodacom ni profit making company. Madeni ya vodacom sio ya kutisha na deni alilonalo vodacom ni analodaiwa na Vodacom Group South Africa ambayo ni parent company, wala sio deni lenye effect yani kama IPP Media iwe inaidai ITV.

Naelewa mtu aking'atwa na nyoka kinachofata akiguswa na jani tu anashtuka. Ndomana watu wote waliopata hasara kwa makampuni kama Precision au NICOL wanaogopa sana soko na wanaliponda, na hiyo inaprove kuwa wao sio wawekezaji wa kweli, kwasababu mwekezaji wa kweli akikosea anajiuliza kwanini alikosea wapi aliteleza ili wakati ujao asiteleze tena na sio kulalalamika kusema soko halina faida wakati wapo wanaofaidika.

Cashflows za Vodacom ziko vizuri tu ndomana wamejiamini kusema dividend watalipa sio chini ya asilimia 50% ya profit. Here is their cash and cash equivalent

Kuna concern kwamba profitability ya vodacom imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka kutokea 2014 bil 128, 2015 bil bil 32 na 2016 bil 29. Ila ukiangalia kilichosababisha kupungua kwa faida ni Investment in Associate ambayo ilikuwa ikiwaletea hasara mwaka 2015 na 2016. Ambayo sasa hiyo hiyo associate imeuzwa kwahiyo haitaaffect tena faida ya vodacom
Angalia hapo kipengele share of loss from associate ilvyokuwa inakula faida ya vodacom, sasa hiyo associate haipo tena imeuzwa


Kuna concern kwamba eti bei 850 ni kubwa sana, jamani bei inaweza kuwa kubwa ndiyo ila pia tujiulize ukiwa unauza biashara yako ambayo umekuwa ukiiendesha kwa mafanikio kwa zaidi ya miaka 15 utaiuza bei rahisi kweli. Biashara ina goodwill ya kutosha una market share kubwa kuliko wapinzani wako, una jina kubwa na unaaminika. Kweli mlitaka muuziwe bei rahisi, ila no wonder kwasababu ndiyo kawaida yetu watz. Kwa mtizamo wangu hiyo bei iko fair tu.

Nimalize tu kwakusema ndugu zangu kina troll na wengine hamna haja ya kuliogopa soko, wawekezaji tupo kwenye game kujifunza kilasiku ili tufaidike na uwekezaji wetu, tuache kufaninisha biashara ya hisa na biashara zingine kama kilimo, kwasababu biashara zingine utahitaji kuzisimamia kilasiku utahusika 100% kwenye operating activities wakati kwenye hisa wewe unaweka tu hela yako inakuwa inakufanyia kazi unasubiri capital gains na dividends hauhusiki 100% kwenye operations.

Wenu kwenye gurudumu la uwekezaji
Geofrey Silumbu
 
Hujanielewa mkuu,hufanyi kitu unakaa tu baada ya kuamua kuwekeza,unafanya research kabla ya kuwekeza then kampuni inakufanyia kila kitu unasubiria gawio lako tu mwisho wa mwaka.

I have deeply understood you Buddy, Am sure this arguement will never End. But all in all Tukubaliane Hii "Passive business/investments" kama una mtaji mkubwa ni biashara tosha kabisa.

In short wenye mitaji midogo tisiwekeze kwenye hizi biashara tukategemea kupata mkate wa kila siku hapa.

Big up guys for this high level discussion.
 
I would like to differ with u.Hata kama mtaji wako ni mkubwa haitafaa with that mindset ya getting rich quickly. Mfano

Nimenunua hisa za kampuni A 1000 kwa bei ya Tzs 1,000,000 na wewe umenunua hisa hizo hizo 100,000 kwa bei ya Tzs 100,000,000 bahati nzuri kampuni ikatangaza gawio la Tzs 200 kwa kila hisa.

Mimi nitapata gawio langu la Tzs 200,000 na wewe utapata Tzs 20,000,000. Si unaona wewe umepata nyingi na mimi kidogo?[emoji15] [emoji15] [emoji15]
Hapo umepata nyingi sababu umewekeza pesa nyingi kunizidi.

Ila rate ya profit ni ile ile tu cheki

Mimi

200,000/1,000,000 * 100% = 20%

Wewe

20,000,000/100,000,000 * 100% = 20%

Kwahiyo gain ni ile ile tu whether uwe umewekeza pesa ndefu au fupi.

Kama mdau alivyosema hapo juu watu wanunua hisa kwa sababu mbali mbali ikiwemo ya prestige ya kua mmiliki wa kampuni fulani aende kwenye AGM kufanya maamuzi n.k. kama lengo lako ni hisa zikutajirishe achana nazo nenda kafanye biashara nyingine zenye high risk na high returns( ceteris paribus).
 

Mzee wa Bukoba hutaki kabisa Kushindwa.
 

Watu wanaosema 850 ni kubwa ni kufananisha na makampuni mengine ya simu Africa/nchi zinazoendelea, sio kwamba wameona tu 850 ni kubwa unavyofikiri.

Vodacom IPO share price highly valued: experts

Kwa kuangalia dividends wanayotarajia kutoa Voda kwa share ni 20-50 shillings hii ni 2%-6% ya 850!
Kwenye fixed deposit benki unaweza kupata 8%-10+% tena kwenye fixed deposit hakuna risk ya mtaji wako kupotea unless benki ifilisike value ya shares inaweza kushuka siku yoyote, kwa hiyo dividend investing haimake sense kwa soko la Tanzania, inamake sense nchi kama marekani ambapo fixed deposit unapata kama 1% returns.

So tumebakia na capital gains, hapa swali ni je growth ya Vodacom itatoka wapi? Teyari ni namba moja TZ na market share yao inashrink kila siku, Tigo wako only 2% nyuma yao, Halotel anakamata share na yeye, so tujiulize growth ya Voda itatoka wapi?

Kama hii IPO iko undersubscribed namna hii, kuna habari za kuaminika kuwa wameuza maybe 1/3-1/2 ya shares zao maana yake hakuna demand na share zitashuka bei zikiwa listed kwa style hii.
 
Bravo.
 
Mkuu hata kwenye hiyo business ya kuwakopesha kinamama kuna risk kibao pia,biashara ya hisa inahitaji timing kali ,na kabla hujanunua unapaswa kufanya analysis ya kina kwenye kampuni unayonunua hisa na angalia pia mabadiliko ya viongozi wa kisiasa wana influence kubwa sana kwenye soko la hisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…