casto mhadisa
New Member
- Jun 3, 2024
- 1
- 0
Tanzania imekuwa ikikumbwa na changamoto ya ajali za barabarani ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa vifo, ulemavu na uharibifu wa Mali na vyombo vya usafiri. Katika taarifa zinazotolewa nyingi zimekuwa zikizungumzia idadi ya vifo na majeruhi, lakini wengi wa majeruhi wanakua wamepoteza viungo vyao vya mwili ambavyo ni mtaji katika kutafuta riziki, wengine wamepooza viungo vya mwili na kuwa tegemezi katika familia na vifo vilivyosababishwa na ajali vimechangia kupoteza watu wa fani mbalimbali ambao wangechangia maendeleo kuanzia ngazi ya familia Hadi taifa. Ili kupunguza athari hizi hatua zifuatazo lazima zifuatwe;
1. Iundwe taasisi ya serikali ambayo itashughulika na maslahi mapana ya madereva wa vyombo vya usafiri binafsi na serikali ikiwemo utatuzi wa haraka wa kero zao pamoja na ufuatiliaji mikataba yao.
2. Kuwepo kwa askari polisi, ambaye atasafiri na Basi la abiria kwa kubadilishana na askari mwingne katika kuhakikisha Sheria zinafuatwa kikamilifu ndani ya basi la abiria kutoka sehemu moja na nyingine hii itachangia utiii wa Sheria.
3. Katika vijiwe vya bodaboda na bajaji visajiliwe kisheria na utambulisho wa madereva kuanzia ngazi ya mtaa Hadi kata na uwepo wa afisa mkaguzi ambaye ataratibu na kuhakikisha watoa huduma katika kijiwe husika wamehudhuria mafunzo ya usalama barabarani pia kutoa kibali Cha huduma kwa dereva aliyezingatia vifaa vya usalama vya kwake na abiria.
4. Madereva wa vyombo vya usafiri wasajiliwe katika mfumo rasmi na aina ya chombo anachoendesha na chuo Cha mafunzo yake ya udereva amba.
5. Sheria ya kuwa na madereva kuanzia wawili katika safari za masafa marefu iwe ni ya lazima kuanzia malori Hadi mabasi, hii itasaidia kuepusha athari za uchovu katika kusababisha ajali za barabarani baada ya kusafiri kwa muda mrefu na kupunguza umakini katika matumizi ya barabara inapelekea kusababisha ajali.
6. Ziwekwe motisha kwa kutoa zawadi kwa madereva na taasisi iliyojizatiti kuhakikisha Kuna weledi wa kuzingatia usalama barabarani ili kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ajali hizo

Upvote
0