MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
UTANGULIZI:
Mwaka 2003 Marekani ilivamia Iraq kimabavu na kumuondoa raisi wa nchi hiyo.
Mataifa mengi ya Ulaya yalimuunga mkono Marekani kwamba anapambana na serikali dhalimu inayohifadhi magaidi na kumiliki silaha za maangamizi. Jambo ambalo ilikuja kufahamika baadaye kwamba halikuwa na ukweli wowote ule, zaidi ya maslahi na siasa za kibeberu.
Ili kufanya uvamizi ni lazima taifa lipewe ruhusa na UNSC chini ya Chapter VII ya UN Charter ambayo inazungumzia mambo kama Collective Defense. Hivyo ilitakiwa Marekani aombe kwamba idhini ya UN na kutoa sababu za msingi kwanini Iraq ivamiwe kijeshi, pamoja kutoa ushahidi, kama ilivyokuwa mwaka 1991.
Raisi wa Ukraine Leonid Kuchma, hali akifahamu fika haya ni makosa aliunga mkono Marekani kwa kupelekea wanajeshi zaidi ya 6000 ambao mchango wao mkubwa ulionekana na kusifiwa na vyombo vya habari vya Magharibi.
Kuna watu wanadai kwamba wanajeshi wa Ukraine ndiyo walikuwa wa kwanza kuingia kwenye baadhi ya makasri ya Saddam Hussein kuliko vikosi vya nchi nyingine, jambo ambalo linapingwa mpaka leo kwamba ni uzushi.
Leonid Kuchma alifanya haya kama njia ya kuifanya Ukraine taifa linalokubalika na nchi za Magharibi, jambo ambalo liliwakera mno watu wengi hasahasa raia wake ambao walikuwa wanafahamu fika kwamba Iraq ni moja kati ya nchi rafiki wa Ukraine hasa kwenye ununuzi wa silaha. Urafiki wao ulianza tokea enzi za USSR.
MUHIMU KUKUMBUKA:
Siasa za kimataifa zinaongozwa na Reciprocity na Balance of Power. Endapo jambo baya moja litafanywa na taifa moja kubwa bila kufanyika uwajibikaji wowote ule, basi fahamu fika taifa jingine kubwa litaiga mbinu hiyohiyo kufanya uvamizi kwa taifa jingine dogo.
Marekani, taifa lililokuwa na nguvu zaidi kuanzia mwaka 1991-2008, lisingeingia kwenye hii michezo ya kuvamia mataifa mengine madogo kama Serbia (1998), Afghanistan (2001), Iraq (2003), Libya (2011), na Syria (2011), huenda mataifa mengine kama Urusi na Uchina yasingethubutu kufikiria kuvamia majirani zao bila kuogopa uwajibikaji wowote ule.
NATO wamepoteza, Moral High Ground, a corner stone of Soft-Power Projection.
Leo hii Marekani hawezi kujaribu kukemea uvamizi wowote na dunia ikaheshimu.
JAMBO LA KUJIFUNZA:
Watu wanaweza kuwa wamesahau au hawafahamu, lakini kinachomkuta Ukraine leo hakina utofauti sana na walichokifanya nchini Iraq mwaka 2003. Dunia hailizungumzii hili kwa undani kwasababu waliouwawa ni waarabu na waislamu, na siyo wazungu wa Ulaya.
Mataifa machanga kama Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, DRC, Egypt na South Africa hayatakiwi kabisa kujihusisha na siasa za mataifa makubwa hasahasa linapokuja suala zima la uvunjifu wa sheria za kimataifa na haki za binadamu.
Ukraine wangekuwa ni taifa ambalo lina sifa nzuri, basi naamini mataifa mengi ya Asia wasingeegamia kwa Urusi hasahasa kwenye suala zima la vikwazo. Ukraine ni moja kati ya mataifa yanayoongoza kwa kuuza silaha hatari kwenye soko haramu (Black Market). Silaha za sumu, silaha za makombora ambazo zilifika Syria, Korea Kaskazini na Iraq zimetokea Ukraine hata kabla ya uvamizi.
Miaka nyuma kidogo, Tony Blair akiwa waziri mkuu wa Uingereza alijaribu kuwashawishi viongozi wa Afrika Kusini na Namibia waivamie kijeshi Zimbabwe na kumtoa Raisi Robert Mugabe, jambo ambalo walilikataa waziwazi bila kupepesa macho. Wangefanya yale waliioombwa na waingereza wangefanikiwa, lakini taswira za nchi zao zingeharibika mno.
Endapo jambo baya lingewakuta Namibia na Afrika Kusini, wasingepata kabisa huruma ya dunia, kama ambavyo Dikteta Mobuthu alikosa huruma baada ya kuvamiwa mwaka 1997, au Savimbi kuuawawa mwaka 2002.
Nchi ndogo zinatakuwa kuwa makini sana.