Mataifa makubwa yenye nguvu katika nyanja zote muhimu ni ngumu sana kuzingatia sheria hasa pale linapo kuja jambo ambalo linagusa maslahi Yao.
Uzi bora kabisa.
Baada ya vita za Napoleon (Napoleonic Wars) kuisha mwaka 1815, Ulaya nzima ilikutanika kule Vienna kufanya mkutano ambao ungeweza kuzuia vita nyingine kubwa barani humo. Mataifa makubwa yakakubaliana kuanzisha kanuni iitwayo The European Balance of Power, iliohakikisha kwamba hakuna taifa moja kubwa litakaloweza kujaribu kuwa na nguvu kubwa ya kutawala wengine.
Ili kusimamia hili, wakatengeneza mfumo wa pamoja uitwao The Concert of Europe (The Congress System/The Vienna System a.k.a The Congress of Vienna) , ambao ungesimamia The European Balance of Power. Wakasaini mkataba wa Vienna a.k.a Vienna Convention 1815 kusimamia hili.
Ukisoma sasa, utafahamu kwamba The Concert of Europe ndiyo baba wa mifumo kama The League of Nations na United Nations, kwasababu ndicho kilikuwa chombo cha kwanza cha kimataifa kusimamia maslahi ya pamoja ya mataifa makubwa.
Matokeo yake ni kwamba, mataifa makubwa yenye nguvu wakati huo kama Prussia, Austria, France na Russia walikubaliana kukaa meza moja kwa mara ya kwanza na kutatua changamoto za kiusalama zinazowakumba wote. Huu mfumo haukukosa changamoto, mataifa makubwa kama Urusi, Prussia na Austria yaliutumia kuzuia maendeleo ya nchi nyingine ndogo ambazo zilionesha kutaka kufanya mapinduzi, mabadiliko ya kidemokrasia na hata kujipatia uhuru.
Wao waliamini kwamba kama taifa litafanya Democratic Reforms, badi halitachelewa kugeuka Ufaransa ya pili, ambayo baada ya kufanya mapinduzi ya mwaka 1789 walianza kuyasambaza hayo mapinduzi Ulaya kote na kupindua madola ya kifalme, jambo lililopelekea miaka kumi ya The Napoleonic Wars. Mwaka 1848, lilitokea wimbi kubwa la mapinduzi barani Ulaya, na The Concert of Europe ilitumiwa na baadhi ya mataifa kuhakikisha vitaifa vidogo havifanyi mapinduzi bila kutishiwa kijeshi au kutumia majasusi na kuuwawa.
The Balance of Power ilianza kuvurugwa pale ambao vinchi vidogo vya Italia chini ya Sardinia vilianza kuungana ili kutengeneza nchi kubwa, (The Italian Unification), huku Prussia nayo chini ya Birsmark ikiamua kuunganisha mataifa zaidi ya 300 (Germanic States) ili kutengeneza Ujerumani moja kubwa (The Unification of Germany). Italia ilizaliwa mwaka 1861, na Ujerumani mwaka 1871.
Italia na Ujerumani yalibadilisha mfumo mzima wa usalama barani Ulaya kwasababu, mataifa kama Austria, Great Britain, Russia na France walipata wapinzani wapya ambao walikuwa na lengo la kushindana nao. Ndiyo maana ikalipuka vita kubwa mwaka 1871 baina ya Ufaransa na Ujerumani (The Franco-Prussian War) wakingombania majimbo yenye madini ya chuma na makaa ya mawe, (Alsace and Lorraine).
Ushindani huu ulianza mwaka 1871 na kupelekea mataifa haya kushindana kidogo kidogo, hadi kwenye makoloni ya Asia na Afrika. Ukisoma utafahamu kwamba The Fashoda Incident, Moroccan Crisis, na Building of Suez Canal ilikuwa ni sehemu ya changamoto za kiusalama zilizoletwa na ushindani wa mataifa makubwa. Ujerumani na Italia yamezaliwa na kukuta wenzao tayari wana makoloni miaka zaidi ya 100. Hivyo yakaanza kupambana nao yasiachwe nyuma.
Kupitia The Concert of Europe, Bismark baada ya kuona vita zitakuwa kubwa akaamua kuitisha kikao nchini Ujerumani kule Berlin (The Berlin Convention 1884-1885) ili wakubaliane kugawana bara la Afrika na kuzuia vita na mashindano. Kila taifa likapeleka mikataba ambayo lilisaini la Local Rulers, jambo ambalo likapelekea hadi vitafa vidogo kama Belgima kupata koloni kubwa kama Congo. Yote hii ni The Concept of European Balance of Power.
Huu mfumo, The Concert of Europe, mbali na madhaifu yake ulifanikiwa kuzuia vita kubwa ambazo zingehusisha nchi zote za Ulaya kwa zaidi ya miaka 100, tokea 1814-1914, ambapo mfumo huu ulianguka baada ya Urusi na Ujerumani kuleteana vitimbwi. Ukisoma utafahamu vyanzo vya vita ya kwanza ya dunia ya mwaka 1914-1918, moja ya sababu kubwa ilikuwa ni Collapse of The European Balance of Power. Matatizo ya mwaka 1871 yalikuja kuonekana mwaka 1914.
Ufaransa alikaa na kinyongo cha kunyang'anywa majimbo yake na Ujerumani tokea mwaka 1871 na kuamua kulipiza kisasi mwaka 1914, miaka zaidi ya hamsini baadaye. Nchi huwa zinaongozwa na matukio kama haya, ndiyo maana huwa tunasema, Reciprocity na Good-Faith ni nguzo muhimu kwenye diplomasia na siasa za kimataifa. Mataifa makubwa hayawezi kufanya kitu halafu kusiwe na madhara, ndiyo maana huwa napata shida kuona watanganyika wanakaza mafuvu kupinga kwamba matatizo ya taifa kama Marekani hayajapelekea vita za Ukraine.
Marekani leo hii angekuwa na amani sana pale Middle-East kama wakina Allen Dulles na Eisenhower wasingeamua kumpindua Waziri Mkuu wa Iran, Mohammed Mossadegh mwaka 1953 na kuligeuza taifa kuwa la kidikteta chini ya Shah. Marekani kaleta matatizo mwaka 1953, Iran akaja kulipiza mwaka 1979, kwa kutaifisha mashirika ya Marekani, kuteka ubalozi na kuiba maelfu ya nyaraka za kijasusi ambazo zilisababisha mamia ya CIA kupoteza maisha kwasababu Ubalozi wa USA nchini Iran ndiyo ulikuwa makao makuu ya CIA barani Asia.
Mfano mwingine, Marekani aliweka makombora yake ya nyuklia (Thor and Jupiter Missiles) Uturuki, karibu kabisa na mpaka wa USSR. Nikita akishawishiwa na kina Ernesto Che Guevarra, ambao walitaka kuikomesha Marekani kwasababu alituma majasusi zaidi ya 2000 kuvamia Cuba (The Bay of Pigs Incident) kuipindua serikali ya Castro, akaamua kupeleka makombora ya kinyuklia nchini Cuba karibu kabisa na Marekani, dunia ikanusurika kuingia kwenye vita ya kinyuklia.
Bahati nzuri Kennedy alikuwa ni kiongozi mwenye hekima sana akaamua kulimaliza tatizo kidiplomasia na kuondoa makombora yake Uturuki. Mambo yakaisha, ila mpaka leo Marekani ana kinyongo kikali na Cuba, akifahamu kwamba ndiyo taifa pekee duniani, tena dogo ambalo liliweza kutishia usalama wake na kufanya dunia isimame. Walimsaka mno Che Guevarra hadi wakamuua na mpaka leo Cuba haijaondolewa vikwazo.
MUHIMU KUKUMBUKA TU:
Matukio mengi yaliyofanyika kipindi cha WW2 yalikuwa na mzizi wa WW1.
Matukio mengi yaliyofanyika kipindi cha WW1 yalikuwa na mzizi wa 1860-70.
Matukio mengi yanayofanyika leo hii mizizi yake ni miaka ya 1990's.
NB: Hivi unadhania baada ya vikwazo vya Urusi, Uchina anaweza kuvamia Taiwani kirahisi bila kuogopa madhara yoyote yale???
===================================================
Shida ni kwamba watu tunapenda kukaza mafuvu, hasahasa watz tukishaangalia filamu za Hollywood na kupata habari za MSM. Ila uzuri ni kwamba REALITY HITS EVERYONE, hadi Wamarekani wenyewe siku hizi wanaanza kutia akili na kugundua kumbe tulikuwa tunapigwa changa la macho, mataifa kama Uchina yako mbali mno kwenye baadhi ya maeneo kuliko Marekani.
===================================================
Baada ya Wamarekani kujiunga kwa wingi na The Red Note, baada ya kufungiwa kwa TikTok, wakagundua kwamba, Hiiiiiiiii dunia wanayoishi iko nyuma ya dunia ile wachina wanaishi. Haijapita muda, wakaleta DeepSeek, ndiyo watu wakalewa kwamba kumbe dunia iko hivi, mengine yote ni Propaganda za kijinga tu. Hakuna taifa litaleta Ubeberu kama Marekani anavyofanya halafu kusiwe na madhara.