Historia haitamsahau Lissu kwa kuipigania Tanganyika

Historia haitamsahau Lissu kwa kuipigania Tanganyika

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Lissu anaweza kuwa na mapungufu yake kwa sababu ni binadamu. Lakini kwa jinsi alivyoipigania Tanganyika tokea akiwa bungeni hata sasa akiwa nje ya Bunge, Historia haitamsahau.

Watanganyika wa leo wasipomwelewa, wazalendo wa kesho watakuja kumjengea sanamu la heshima kumuenzi.

Kajipatia heshima Zanzibar na Tanganyika kwa kuusimamia ukweli kuhusu Muungano.

Mungu ambariki Tundu A. Lissu.

PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Kuhoji Je Tanganyika ipo wapi ndaji ya muungano wetu ndiyo kupinga.?

Zanzibar ni Muungano wa nchi mbili na kuzaa Jamhuri ya Muungamo waTanzania, sasa hiyo nchi ya pili ni ipi? tusaidie mtoa hoja.
 
Waliopigania Tanganyika huwajui wewe, hebu muulize mzee Mohamed Said akupe historia japo kwa ufupi.
Sijazungumzia Tanganyika iliyokuwa kiloni la Mzungu, bali Tanganyika iliyokabidhiwa uhuru wake halali kisha hayati Nyerere akaukabidhi uhuru huo kwa mkononi mwingine, Zanzibar.
 
Tuleteeni mkataba orjino wa Muungano tuyaone hayo mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano.
Akili yenye uelewa itafahamu Mambo ya Muungano ni yahusuyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ,ambayo inajulikana kama Tanzania na yasiyo ya Muungano ni yale yahusuyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hivyo tuna
1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya/wa Tanzania
2) Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

Unaposikia kuna mambo si ya Muungano huwaga unajiuliza mambo hayo ni ya nani na ya serikali ipi ?

Isije kuwa bajeti inayoingia kwenye hayo tunayoambiwa si ya Muungano wala si ya Serikali ya Zanzibar inaishia kwa wajanja .
 
Nashangaa kwa nini Magufuli aliwashughulikia wafanyakazi hewa akauacha Muungano hewa!
 
Lissu anaweza kuwa na mapungufu yake kwa sababu ni binadamu. Lakini kwa jinsi alivyoipigania Tanganyika tokea akiwa bungeni hata sasa akiwa nje ya Bunge, Historia haitamsahau.

Watanganyika wa leo wasipomwelewa, wazalendo wa kesho watakuja kumjengea sanamu la heshima kumuenzi.

Kajipatia heshima Zanzibar na Tanganyika kwa kuusimamia ukweli kuhusu Muungano.

Mungu ambariki Tundu A. Lissu.
Lisu ana faida kuliko chadema yote. anakosa tu chama cha kwenda.
 
Kuhoji Je Tanganyika ipo wapi ndaji ya muungano wetu ndiyo kupinga.?

Zanzibar ni Muungano wa nchi mbili na kuzaa Jamhuri ya Muungamo waTanzania, sasa hiyo nchi ya pili ni ipi? tusaidie mtoa hoja.
Nchi ya pili ni nchi nzuri, kubwa, thabiti iitwayo Tanganyika. Watawala wamejitahidi kwa miongo kadhaa kuifisha lakini wameshindwa, na hawatakaa wafanikiwe kuiua.

Tanganyika will never die!
 
Kunahaja ya kuwepo na Tuzo/nishani ya Heshima itakayopewa jina la Lissu ambayo takuwa anapewa Mtanzania, ambaye bila wasiwasi ataonekana anaonesha uzalendo kwa Taifa, bila kuwepo kwa kampeni za kumsifia au uchawa.
 
Attachments

  • KWA_KAULI_HII_YA_LISSU_KUHUSU_RAIS_SAMIA_JAMANI_JESHI_LA_POLISI_HATUJUI_KAMA_LITAMUACHA_VIZURI...mp4
    30 MB
  • BALAA_LA_LISSU_MIAKA_10_ILIYOPITA_JUU_YA_MUUNGANO,_RAIS_SAMIA_AKIWA_M_KITI_WA_BUNGE_LA_KATIBA(...mp4
    11.7 MB
Hata Mchungaji Christopher Mtikila haku wahi shusha bendera ya Tanganyika kwenye ofisi yake.

Wazee wa G-55 waliona mbali sana.Tanganyika iliuzwa na bwana haambiliki.
 
Hata Mchungaji Christopher Mtikila haki wahi shusha bendera ya Tangany kwenye ofisi yake.

Wazee wa G-55 waliona mbali sana.Tanganyika iliuzwa na bwana haambiliki.
Kumbe kulikuwa na watu wenye bendera ya Tanganyika? Kwa sasa inaweza kupatikana wapi?
 
Lakini kwa jinsi alivyoipigania Tanganyika tokea akiwa bungeni hata sasa akiwa nje ya Bunge, Historia haitamsahau.
Je ni zaidi ya Huyu Mheshimiwa (R.I.P) enzi za uhai wake??
1714751325173.png
1714751152189.png

Back
Top Bottom