Historia imedanganya na kupotosha asili ya mwanadamu

Historia imedanganya na kupotosha asili ya mwanadamu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Sidhani kama huu uongo na upotoshaji bado unafundishwa kwenye shule zetu kwenye somo la historia....
Sisi tulifundishwa na kuaminishwa kuwa asili ya mwanadamu ni mnyama nyani.... Ni katika harakati za kutatua changamoto za maisha yanayomzunguka ndio akajikuta mpaka anaweza kusimama kwa miguu miwili na kutumia mikono kwa shughuli nyinginezo... Ithibati za kuunga zikionesha kutoka hatua za homo sapien mpaka homo habilis.. Ambaye sasa alikuwa ni binadamu kamili....
Kadiri tunavyozidi kuzama na kuhoji kuhusu hizi elimu na uhalisia wake ndivyo tunavyozidi kuangaziwa na kufunuliwa kuhusu uongo na upotoshaji mwingi kisayansi, kibaologia na kihistoria...
Ndana ya binadamu wa kwanza kutokana na nyani inawezekana kabisa ndio dhana dhaifu zaidi na inayoongoza kwa uongo na upotoshaji kuliko dhana nyingine zote kuhusiana na asili ya mwanadamu
Kuna maswali mengi ya kuhoji hapa
. Asili ya huyo nyani ni ipi?
. Kwanini baada ya hapo nyani wengine hawakupitia mchakato wa mabadiliko mpaka kuwa binadamu?
. Kwanini sasa nyani azae nyani na binadamu azae binadamu?
. Kwanini kusiwe na kinyume cha binadamu kuzaa nyani na nyani kuzaa binadamu?

Pamoja na mfanano wa vinasaba kati ya nyani na binadamu kwa zaidi ya asilimia 90.. Lakini ukweli unabaki kuwa hizi ni asili mbili tofauti kabisa
Dhana ya binadamu kubadilika umbo tangu kuumbwa kwa dunia inaweza kuwa na mashiko... Tukisoma misahafu tunaambiwa kuna watu waliishi zaidi ya miaka 800,Lakini pia kuna simulizi za wanefili, majitu makubwa yaliyoishi zamani...rejea zinjathropus
Kadiri miaka inavyosonga umri wa kuishi unazidi kupungua na hata maumbo pia.. Na hii si kwa binadamu tuu bali hata wanyama na vitu vingine vingi...
Dhana pekee ambayo mpaka sasa inajadilika ni Ile dhana ya uumbaji wa kiimani... Dhana ya asili ya mwanadamu na uumbaji wa kimungu...
Upotoshaji huu wa historia ulifanywa na watu maalum... Je lengo lao lilikuwa ninini?
 
Salute
Mimi kitu nachoona kuna baadhi ya vitu tumemiss
Why?
Takwimu zinaonyesha Asilimia 70% ya historian ya mwanadamu Na dunia haikuandikwa/hapo. Hivyo twafahamu robo tu ya historian ya dunia baaasi yawezekana kati ya historia ambayo haikuandikwa kikamirifu ni historia ya mwanadamu.

Hata hivyo hongera kwao wa Egyptus wamejitahidi na wanamchango mkubwa katika Ku preserve historia ya mwanadamu Na dunia kwa ujumla
 
Inategemea unaamini katika nini... Ndio toka hapo unaweza kuanza kujenga hoja
...yeah sure mkuu
....na ndio maana hata wewe umei_crash ya evolution na kuiremba ya creation_just bcoz ndio unachoamini
....all in all zote ni nadharia tu na kama ulivyosema maji hufuata mkondo...I,e imani yako ndio iteditamaini nadharia IPI uifuate
 
Wanadanganya ili kutushusha thamani waafrika.
Ili tuji-feel inferior.
Mbona wazungu hawafundishwi hayo kwao yakuwa tulitokana na nyani?!
 
Yaan swali LA kuhusu binadamu Mwanzo wake ni UPI na wapi anapokwenda ni Magumu sana Mwisho wa siku wabaki na imani na siyo Uhakika...
 
...dhana yenye mashiko kidogo ni ile ya kuumbwa na Alliens,..Ananuk....ila hii ya kwenye biblia na Quran haina mashiko hata robo nayo
Vitabu vya dini vimeeleza kwa kiwango chake hebu tueleze nawe hawa Aliens walimuumbaje mwanaadamu au wao ndio walijibadilisha...?
 
...yeah sure mkuu
....na ndio maana hata wewe umei_crash ya evolution na kuiremba ya creation_just bcoz ndio unachoamini
....all in all zote ni nadharia tu na kama ulivyosema maji hufuata mkondo...I,e imani yako ndio iteditamaini nadharia IPI uifuate
Noted... Japo sijairemba ila nimeandika mtazamo
 
Kuna mengi yamefichwa Kwa sababu Fulani,hata elimu inayotolewa Kwenye syllabus zetu bado haiendani na mazingira yetu..mbaya zaidi hatustuki tumeingia Kwenye mtego wao..wanasema ukitaka umfiche Mwafrika weka ujumbe kwenye vitabu na hivi hatupendi kusoma..ndio wanazidi kutuburuza.
 
True
 
Una point hapa..
Japo wanasema historia kubwa ya mwanadamu haikuandikwa lakini pia watu Fulani wanachangia historia ya mwanadamu isifahamike dhahiri, wanapanga sisi normal people tujue hiki kile tusijue..
 
Mzungu akitaka kukudhoofisha kisaikolojia pale aonapo una nguvu, maono na kila dalili za kumpiku, hukuharibu kisaikolojia Kwa figisu mbalimbali.....kiukweli hii historia ya asili ya mwanadamu kuhusishwa na nyani (hasa mwafrika ameathirika zaidi na dhana hii,) ilikuwa ni project ya Wazungu katika kumdhoofisha mwafrika kisaiKolojia kwani hata sasa tunashuhudia ubaguzi mkubwa kwa Mwafrika kuliko race nyingine yoyote ilhali dhana yenyewe haikuwahi kumtaja Mwafrika moja kwa moja bali iligeneralize Binadamu wote kama asili moja ya nyani.......Ndio maana hata wakoloni waliitumia kama chambo ya kuwacolonize Waafrika...hii historia imejaa uongo na dhambi tupu!!!!
 
Uko sahihi..unajua kuna kitu kinaitwa "Brain drain" waafrika tuko na akili mingi sana ila Kwenye matumizi ndio tunafeli..na wale wachache wenye akili wakigundulika tu "The so called wazungu" wanafanya hiyo kitu..wako tayari wakupe hata uraia.. Watu wenye matumizi mazuri ya akili ndio wanaendesha hii dunia.
 
Mzungu akitaka kukudhoofisha kisaikolojia pale aonapo una nguvu, maono na kila dalili za kumpiku, hukuharibu kisaikolojia Kwa figisu mbalimbali.....kiukweli hii historia ya asili ya mwanadamu kuhusishwa na nyani (hasa mwafrika ameathirika zaidi na dhana hii,) ilikuwa ni project ya Wazungu katika kumdhoofisha mwafrika kisaiKolojia kwani hata sasa tunashuhudia ubaguzi mkubwa kwa Mwafrika kuliko race nyingine yoyote ilhali dhana yenyewe haikuwahi kumtaja Mwafrika moja kwa moja bali iligeneralize Binadamu wote kama asili moja ya nyani.......Ndio maana hata wakoloni waliitumia kama chambo ya kuwacolonize Waafrika...hii historia imejaa uongo na dhambi tupu!!!!
Historia inaonesha mzungu nae yupo kwenye kundi hili la Nyani sio mwafrika peke yake
 
Kutaka kujua asili/chimbuko la mwanadam ni sawa na kutaka kujua asili/chimbuko la Mungu
Tumeletewa vitabu tukaambiwa history ya binadam na tukaamin kupitia ivo vitabu (Bible na Quran)
Lkn kuna vitabu vingine vinavyopinga vitabu vya dini lkn cha ajabu hatuviamin
Hp ndo shida ipo!!
 
Back
Top Bottom