Unaposema sayansi ni pana kuliko historia unamaanisha nini ?kiukweli unapozungumzia science ni pana kuliko history na history ilikuwa inacopy mambo ambayo hayana utafiti
Je una uhakika na unalolisema ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaposema sayansi ni pana kuliko historia unamaanisha nini ?kiukweli unapozungumzia science ni pana kuliko history na history ilikuwa inacopy mambo ambayo hayana utafiti
Sidhani kama huu uongo na upotoshaji bado unafundishwa kwenye shule zetu kwenye somo la historia....
Sisi tulifundishwa na kuaminishwa kuwa asili ya mwanadamu ni mnyama nyani.... Ni katika harakati za kutatua changamoto za maisha yanayomzunguka ndio akajikuta mpaka anaweza kusimama kwa miguu miwili na kutumia mikono kwa shughuli nyinginezo... Ithibati za kuunga zikionesha kutoka hatua za homo sapien mpaka homo habilis.. Ambaye sasa alikuwa ni binadamu kamili....
Kadiri tunavyozidi kuzama na kuhoji kuhusu hizi elimu na uhalisia wake ndivyo tunavyozidi kuangaziwa na kufunuliwa kuhusu uongo na upotoshaji mwingi kisayansi, kibaologia na kihistoria...
Ndana ya binadamu wa kwanza kutokana na nyani inawezekana kabisa ndio dhana dhaifu zaidi na inayoongoza kwa uongo na upotoshaji kuliko dhana nyingine zote kuhusiana na asili ya mwanadamu
Kuna maswali mengi ya kuhoji hapa
. Asili ya huyo nyani ni ipi?
. Kwanini baada ya hapo nyani wengine hawakupitia mchakato wa mabadiliko mpaka kuwa binadamu?
. Kwanini sasa nyani azae nyani na binadamu azae binadamu?
. Kwanini kusiwe na kinyume cha binadamu kuzaa nyani na nyani kuzaa binadamu?
Pamoja na mfanano wa vinasaba kati ya nyani na binadamu kwa zaidi ya asilimia 90.. Lakini ukweli unabaki kuwa hizi ni asili mbili tofauti kabisa
Dhana ya binadamu kubadilika umbo tangu kuumbwa kwa dunia inaweza kuwa na mashiko... Tukisoma misahafu tunaambiwa kuna watu waliishi zaidi ya miaka 800,Lakini pia kuna simulizi za wanefili, majitu makubwa yaliyoishi zamani...rejea zinjathropus
Kadiri miaka inavyosonga umri wa kuishi unazidi kupungua na hata maumbo pia.. Na hii si kwa binadamu tuu bali hata wanyama na vitu vingine vingi...
Dhana pekee ambayo mpaka sasa inajadilika ni Ile dhana ya uumbaji wa kiimani... Dhana ya asili ya mwanadamu na uumbaji wa kimungu...
Upotoshaji huu wa historia ulifanywa na watu maalum... Je lengo lao lilikuwa ninini?
Radiometric dating!Huwa nahoji sana hayo mamilioni ya miaka.. Kimetumika kipimo gani kuyapima?
Hebu tujuze Archeology inaelezea nini nasi tujifunze hapoMtaalam Mshana Jr! Salute!
Tunaishi katika Ulimwengu ambao watu wako huru kuamini wanachotaka kukiamini! Uwepo wa Mwanadamu Duniani unaelezwa vema sana katika vitabu vya Kiimani - Biblia,Torah,Gita na Quran.(KUELEZWA VEMA HAIMAANISHI NI RAHISI BALI NI KWA SABABU ASILI YA MWANADAMU INAELEZWA KIRAHISI SANAAAA! MUNGU ALIMUUMBA MWANADAMU FULL STOP).
Lakini Kwa sababu ya Udadisi na Shauku ya Kuthibitisha kila kitu na ile hulka ya Mwanadamu ya Kutafakari kwa kina ili apate majibu ya kila Swali ndio imetufikisha hapa tulipo!
Jiografia ndio somo la kwanza kabisa kuelezea asili ya ULIMWENGU na Sayari zake kuwa ni matokeo ya Mlimpuko Mkubwa sana( Big Bang) Uliotokea miaka takribani Billion 4 iliyopita ndipo zikatokea sayari na Nyota zote.
Somo hili pia likatupatia na tarehe ya mabadiliko ya Mimea na Miti Nini kilianza kutokea na nini kilifuatia na matokeo ya hayo mabadiliko ni mchakato wa asili wa Kisanyansi.(Geological Time Scale).
Historia ni Somo ambalo lilienda mbali zaidi katika kuchambua hatua kwa hatua ya mabadiliko ya Binadamu - ndipo inapodai Kuwa Binadamu tunaemuona leo alitokana na Familia ya Nyani - Apes ambao walishatoweka kabisa ulimwenguni na kwa mabadiliko hayo tumempata Modern Man (Homo sapiens).
Charles Darwin ndiye baba wa nadharia hii ya Mabadiliko ya Viumbe Hai (Evolution Theory) ambayo ameileza vema katika kitabu chake cha Origin of Spicies; Bwana Darwin hakuwa mpagani;alizaliwa katika familia ya Wakristo na Wacha Mungu kabisa, lakini aliamua kutoamini alichojifunza Sunday School na Kutafuta Majibu ambayo wadadisi wote wangependa kusikia.
Alifanikiwa katika Utafiti wake kwa kiasi kikubwa sana hasa pale alipoonesha jinsi gani viumbe wengine walikuwepo na sababu ya kutoweka kwao leo - survival of the fittest theory.Lakini wakati mwingine alikwama kwa sababu alikutana na Wasomi wenzake waliomuuliza maswali ambayo kisayansi hayana majibu mpaka leo - Kati ya YAI na KUKU kipi Kilitangulia iwapo vitu vyote vilitokea kwa Asili moja.
Nimesoma Kozi hii ya Archeology nilikuwa natamani kipindi kiishe! Mambo hayakuwa yanaeleweka kirahisi.
Lakini kuna kitu nilijifunza kinanisaidia mpaka leo - Kupotea ndio Kujua Njia.
Wasio amini Uumbaji wakisoma Archeology wataanza kuamini Uumbaji!(Creationism).
Hata katika Thread zako! unatoa mchango mzuri sana kwa watu wasioamini katika Nguvu za Asili! Hii itawasaidia siku moja Kujua Nguvu iliyobora Kuliko zote ni ipi;Hivyo basi nadhani hakuna upotoshwaji isipokuwa kuna udadisi ambao una heri ndani yake iwapo utamnoa mtu vema na kwa kina (Tahadhari tu - Little learning is a dangerous thing).
Historia haijadanganya! wala haijapotosha asili ya Mwanadamu! Historia ni taaluma iliyoradhi kukosolewa na Kusahihishwa kwa vigezo na ushahidi.
Asante!
Sidhani kama huu uongo na upotoshaji bado unafundishwa kwenye shule zetu kwenye somo la historia....
Sisi tulifundishwa na kuaminishwa kuwa asili ya mwanadamu ni mnyama nyani.... Ni katika harakati za kutatua changamoto za maisha yanayomzunguka ndio akajikuta mpaka anaweza kusimama kwa miguu miwili na kutumia mikono kwa shughuli nyinginezo... Ithibati za kuunga zikionesha kutoka hatua za homo sapien mpaka homo habilis.. Ambaye sasa alikuwa ni binadamu kamili....
Kadiri tunavyozidi kuzama na kuhoji kuhusu hizi elimu na uhalisia wake ndivyo tunavyozidi kuangaziwa na kufunuliwa kuhusu uongo na upotoshaji mwingi kisayansi, kibaologia na kihistoria...
Ndana ya binadamu wa kwanza kutokana na nyani inawezekana kabisa ndio dhana dhaifu zaidi na inayoongoza kwa uongo na upotoshaji kuliko dhana nyingine zote kuhusiana na asili ya mwanadamu
Kuna maswali mengi ya kuhoji hapa
. Asili ya huyo nyani ni ipi?
. Kwanini baada ya hapo nyani wengine hawakupitia mchakato wa mabadiliko mpaka kuwa binadamu?
. Kwanini sasa nyani azae nyani na binadamu azae binadamu?
. Kwanini kusiwe na kinyume cha binadamu kuzaa nyani na nyani kuzaa binadamu?
Pamoja na mfanano wa vinasaba kati ya nyani na binadamu kwa zaidi ya asilimia 90.. Lakini ukweli unabaki kuwa hizi ni asili mbili tofauti kabisa
Dhana ya binadamu kubadilika umbo tangu kuumbwa kwa dunia inaweza kuwa na mashiko... Tukisoma misahafu tunaambiwa kuna watu waliishi zaidi ya miaka 800,Lakini pia kuna simulizi za wanefili, majitu makubwa yaliyoishi zamani...rejea zinjathropus
Kadiri miaka inavyosonga umri wa kuishi unazidi kupungua na hata maumbo pia.. Na hii si kwa binadamu tuu bali hata wanyama na vitu vingine vingi...
Dhana pekee ambayo mpaka sasa inajadilika ni Ile dhana ya uumbaji wa kiimani... Dhana ya asili ya mwanadamu na uumbaji wa kimungu...
Upotoshaji huu wa historia ulifanywa na watu maalum... Je lengo lao lilikuwa ninini?
Hebu tujuze Archeology inaelezea nini nasi tujifunze hapo
[emoji121][emoji121][emoji121][emoji121][emoji121][emoji121][emoji121][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji123][emoji109][emoji115][emoji112][emoji112][emoji112][emoji112]Mkuu Archaeology( Akioloji) ni somo linaoleza kuhusu mambo ya kale kabla ya kuwepo kwa historia kwa kupitia masalia ya
Ustaarabu wa kale.
Tulifundishwa kuwa Somo hili ni Sayansi tupu! Hakuna Kubashiri wala Kubabia!
Hawa Maakiolojisti wanajikita zaidi katika kuthibitisha mambo ya kale kisayansi kwa kuchimbua na kupima masalia ya kale na Utamaduni wake.
Mfano Asili ya Binadamu wa kwanza na uwepo wa Miji ya Kale na ustaraabu wake.
Archeologia inagusa uwepo wa miji na majiji ya kale sana! Ancient World Civilizations. Hapa Unagusa Ancient Egypt(Misri),Mesopotamia( Iraq,Iran na Viunga vyake),Bonde la Mto ganges (india),Mesoamerica(Amerika ya kati) na Uchina.
Kati ya Wana - akiolojia maarufu Duniani ni pamoja na Dr. Leakey ambaye 1959 alivumbua mabaki ya zamadamu katika bonde la Olduvai gorge Tanzania;inathibitishwa kuwa ndio mabaki halisi ya Zamadamu anayesadikiwa kuwa ndio chimbuko la asili la Binadamu ( The crandle of mankind).
Wanaakiolojia pia wamesaidia sana kuthibitisha usahihi wa Biblia kwa kulinganisha habari zake na habari walizozigundua hivi karibuni kutoka katika vitu vya kale kama mawe magombo ya ngozi na maandishi katika karatasi za Papylus;Mfano The Dead sea Scrolls,Rosseta stone na nk.
- Uwepo wa Gharika la Nuhu
-Uwepo wa miji kama Pompei
-Mtu aliyeishi miaka 5000 iliyopita Otzi Mwanabarafu; ambaye alivumbuliwa na watafiti katika Vilele vya Milima ya Alps Ulaya
- Makaburi ya mafarao Misri na nk.
- Uwepo wa miji kama Sodoma
Cheikh Anta Diop Msomi na Nguli wa Historia Barani afrika akirejea Somo hili la Akiolojia aliweza kujenga Hoja Kuhusu wenyeji wa Misri ya Kale walikuwa Watu Weusi.
Inasemekana ulikuwepo mji maarufu sana pwani ya Tz kati ya mto pangani na Kilwa;Mji huo ulipotea kwa sababu za kimazingira- yaani ulimezwa na bahari au ulifukiwa na udongo ukapotea Utafiti bado unaendelea mpaka leo.
Hiyo ndio Kazi ya archaeologists.MAMBO YA KALE kwa Kupitia VITU vya Kale.
Natumaini nimejaribu kidogo kufafanua.
Shukrani.
Divide n rule theory... Na imefanikiwa kweli... Na ndio chanzo cha extremismmizimu mizimu mizimu ya mababu zangu ilikuwa na taratibu na kufahamu yaliyo mengi kupitia mila na desturi walipokuja watu weupe wakaharibu kila kitu wakatuachia imani mbili katili zinazosigana hata leo.mkwawa ni sehemu ya mzimu wa jadi ulioitia aibu sana hii ngozi nyeupe,tuirudieni mizimu.
Sasa tatizo ni shule yangu ndogo au ni msamiati 'ya' kiswahili!? Usichanganye mambo mengi kwenye reply moja tafadhaliNani kakufundisha binadamu alikuwa nyani? Shule yako ni ndogo kwenye historia..
Binadamu asili yake ni zamadamu wala sio nyani.. Tatizo ni msamiati ya kiswahili..
Ila mizimu huwa Haifi nakupotea IPO siku itatoka mapangoni huko,na niwakumbushe watu ngozi nyeusi ni kizazi kikuu sana kisicho na mfano.walilijua hili na ndio maana waliwekeza sana kuwavuruga,hili ni kama walilolifanya kwa shirishama wa amazoni huko brazilDivide n rule theory... Na imefanikiwa kweli... Na ndio chanzo cha extremism
Nilikuwa msomaji mzuri sana wa majarida ya X-factors... Wanatoa elimu kubwa sana kuhusu weusi, kuanzia ustaarabu mpaka ugunduzi mbalimbali.... Wazungu wanajaribu kwa hila zote kuficha ukweli lakini ni ngumuKatika tafiti zangu nilizofanya baada ya kutoka katika darasa la akiolojia niligundua kwamba Wazungu ni Wajinga sana halafu wanasahau haraka sana!Kwa hoja zifuatazo:-
1. Zamadamu (primates) hawa inavyoonesha wametapakaa ulimwenguni kote: Afrika ya Kusini,Kenya,namibia,Ethiopia na Tanzania bara la ulaya na Asia.
Sasa hawa wa hapa Afrika Australopithecus(afarensis,boisei na africanus) Ndio wenye umri mrefu na wakongwe zaidi.
Na ndio wanaokidhi kivigezo kutoa chimbuko la binadamu hasa wa hapa kwetu Tz.( Zinjathropus).
2.Zamadamu waliogunduliwa nje ya bara la afrika; yaani waliopatikana Ulaya na Asia wanonekana sio wakongwe kiumri ukilinganisha na wa bara letu.Homo neanderthalensis .
Hawa waligunduliwa katika bonde la Neandathal Huko ujerumani.Hawakidhi vigezo vya mabadiliko kuelekea ubinadamuni.
Hivyo Basi Mzungu akubali yaishe asili ya Manhood ni afrika na yeye hapa maana yake ni Nyumbani.
Wazungu rudini nyumbani aseee.
Hivi kwanini wasinge cheat hapa ikaonekana wao ndio asili ya Binadamu??
Sijawahi ona sehemu Mzungu anasumbuka kugombania asili ya Binadamu wa kwanza awe yeye! Ila nimeona na nimesikia jinsi mzungu anavyosumbuka kumuonesha mweusi ni dhaifu na hafai ila Mweupe ndio sura ya Mungu!.