Historia imedanganya na kupotosha asili ya mwanadamu

Historia imedanganya na kupotosha asili ya mwanadamu

Naendelea.

4. Nasaba au nisba

Huu ni msingi muhimu sana kuujua na kuufanyia kazi unapotaka au unapoiendea elimu fulani.

Lazia ujue elimu unayoisoma au unayo taka kuisoma ina munasaba gani au ina mahusiano na elimu nyingine,au iko ndani ya elimu gani. Hapa nataka nitoe mfano.

Ukiulizwa leo hii Elimu ya USHAIRI ina munasaba gani na elimu nyingine mama ? Hapa moja kwa moja utasema munasaba wa elimu ya ushairi ni miongoni mwa elimu za lugha.

5. Ubora wa elimu husika

Huu ni msingi mkubwa katika kujifunza elimu. Lazima ujue kwamba elimu husika ina ubora gani,je ni lazima kujifunza au sio lazima ? Je elimu hii wachache wakijifunza hutosheleza wengine au la ?

Katika msingi huu kuna mifano kadhaa. Kiimani ni lazima kila mtu ajifunze elimu ya dini yake hapa hakuna udhuru. Ila si lazima kila mtu awe muhandisi au tabibu au mwalimu wa somo fulani,hapa wachache wakisoma wanakuwa wamewatosheleza wengine.

Narudi kuendelea na msingi wa 6......!
Niko hapa [emoji101][emoji101][emoji101][emoji101]
 
Hapa sasa ndio tunaona maajabi ya Elimu. Hapa nazungumzia Elimu ya uhakiki wa habari.

Nakuuliza tena swali,Je una uhakika gani juu ya ukweli habari hiyo ?

Je wewe baada ya kupata habari hiyo,ulitumia hatua gani au vigezo gani kuisadiki habari hiyo.

Nasubiri jibu bro !
Yaani kila nikiandika nitaibua maswali mengi kutoka kwako. Nilijua tu lazima utauliza kuhusu uhakika kama hao dinosaurs waliexist . Ujue watu hawakukaa tu wakajiandikia kuwa dinosaur aliexist. Ni paleontology inahusika hapo mkuu ambayo ni evidence kubwa sana kuhusu uwepo wa evolution. Je wewe huamini paleontology??. Na kwanini unaona paleontology haipo sawa??. Je wewe unasadiki nadharia ipi ya asili ya uhai?.

Umeuliza nina uhakika gani na hizo mambo, hapa nadhani ndio maana mpaka leo evolution ni theory tu . Kinachofanya mpaka leo hii theory inaaminiwa na wengi ni kwa sababu inamake scientific sense. Ina biological plausibility.

Wakati Darwin anatoa hiyo theory ali Iback up na scientific proof na akatoa mifano mingi tu ya huko alikozunguka. Kwahiyo hapa am not re-inventing the wheel.
 
Naendelea.

4. Nasaba au nisba

Huu ni msingi muhimu sana kuujua na kuufanyia kazi unapotaka au unapoiendea elimu fulani.

Lazia ujue elimu unayoisoma au unayo taka kuisoma ina munasaba gani au ina mahusiano na elimu nyingine,au iko ndani ya elimu gani. Hapa nataka nitoe mfano.

Ukiulizwa leo hii Elimu ya USHAIRI ina munasaba gani na elimu nyingine mama ? Hapa moja kwa moja utasema munasaba wa elimu ya ushairi ni miongoni mwa elimu za lugha.

5. Ubora wa elimu husika

Huu ni msingi mkubwa katika kujifunza elimu. Lazima ujue kwamba elimu husika ina ubora gani,je ni lazima kujifunza au sio lazima ? Je elimu hii wachache wakijifunza hutosheleza wengine au la ?

Katika msingi huu kuna mifano kadhaa. Kiimani ni lazima kila mtu ajifunze elimu ya dini yake hapa hakuna udhuru. Ila si lazima kila mtu awe muhandisi au tabibu au mwalimu wa somo fulani,hapa wachache wakisoma wanakuwa wamewatosheleza wengine.

Narudi kuendelea na msingi wa 6......!
Ngoja nikupe mfano mzuri ambao unakuonyesha ni jinsi gani evolution ipo na inafanya kazi.

Katika mafanikio makubwa kabisa katika medani ya matibabu ni ugunduzi wa madawa dhidi ya vimelea vya magonjwa(antimicrobials). Na ikaonekana kama sasa magonjwa yote ya kuambukizwa yatakua historia. Lakini hawakujua kama hii ligi si ya kispoti spoti.

Mwanzo zilifanya kazi vizuri Sana ila taratibu zikaanza kupoteza uwezo wake. Hii yote ni kwa sababu wale viumbe nao ni wajanja na wana system zao ambazo zina operate ili waendelee kusurvive. Hivi vimelea mwanzo vilikua vinakufa sana ila vikaanza kuivolve ili kupunguza majanga yaliyovikumba. Hii yote ni kumaximize chances of survival.

Vimelea vilivyoshindwa kubadilika vilikufa na vile ambavyo vilibadilika ndio vinaendelea kutupa tabu mpaka leo. Ndio maana waathirika wa HIV/UKIMWI wanatakiwa kutumia ARV kila siku ili kuvinyima chance ya kuivolve na kusababisha resistance ambayo ni Mojawapo ya matatizo makubwa katika medani ya afya.

Nadhani haya maelezo yana onyesha uhusiano kati ya evolution na disciplines zingine (swali la 4 ) . Pia yanaonyesha ni jinsi gani knowledge ya evolution ilivyo na msaada kwa Jamii (swali la 5 ) .

Life is all about struggle for existence but wonderful enough nature decides your fate. No matter how strong you are but what matters is how you adapt to the changes in the environment. If you fail to change nature will select you out.
 
...dhana yenye mashiko kidogo ni ile ya kuumbwa na Alliens,..Ananuk....ila hii ya kwenye biblia na Quran haina mashiko hata robo nayo
kwenye quran tunaambiwa Mungu ndio mwenye ujuzi na kila kitu na alichokiumba anakijua yeye kwahiyo swala la kuwepo au kutokuwepo kwa aliens anajua alieumba
 
Angalau mlengo wa kihistoria unaeleweka kuliko huo wa kidini ambao umekaa shaghalabagala ukiwa umejengwa juu ya msingi wa hofu na kila anayetaka kuhoji kwa undani zaidi anaambiwa anakufuru hivyo awe anakubali tu kila anachoambiwa. Hakuna sehemu ambayo historia inasema binaadamu anatokana na nyani ila binaadamu na nyani wana asili moja yaani ancestor wao ni mmoja. Ushahdi kuhusu evolution upo, nyani hawezi kubadilika kuwa mtu kwa kuwa lineage yake ni nyingine so anaendelea kubadilika kivingine ila hatuoni kwa kuwa ni process ambayo ipo taratibu sana na itakuchukua mamilioni mengi ya miaka hadi badiliko dogo liweze kuonekana.
 
Naendelea.

7. Nani wa mwanzoni

Katika kila fani huu msingi huzingatiwa sana. Lazima au unatakiwa kumjua ni nani wa kwanza au wa mwanzo katika fani au elimu husika.

Mfano leo hii ukiniuliza ni nani wa kwanza katika Elimu ya ushairi wa Kiswahili ? Hapa mimi bila kupepesa macho lazima nitakwambia ni Sheikh Kaluta Amri Abeid.

Swali kwanini awe Kaluta hali ya kuwa yeye si wa mwanzo katika utunzi wa mashairi ya Kiswahili ?

Mashairi yalikuwepo ila wa kwanza kuweka kanuni za utunzi wa mashairi huyu ndio husemwa wa mwanzo katika elimu ya ushairi,kwani yeye ameyasoma kwa makini mashairi na akagundua yaliyofichikana katika ushairi na namna ambavyo utunzi ulivyokuwa unapita mapito gani. Kisha akatengeneza kanuni kutokana na mashairi.

Kwahiyo lazima umjue yule aliyedhibiti mambo muhimu mpaka yakapelekea kuwepo elimu husika.

Narudi kuendelea......!
 
kuna teacher mmoja wa history aliwahi kimbia darasa letu form one alivyokuja mwingine alikuwa anaingia na bible na kitabu ya history ndio maana hadi leo katika somo ambalo silielewi hata robo ilo hapo
_20180711_205211.JPG
 
Yaani kila nikiandika nitaibua maswali mengi kutoka kwako. Nilijua tu lazima utauliza kuhusu uhakika kama hao dinosaurs waliexist . Ujue watu hawakukaa tu wakajiandikia kuwa dinosaur aliexist. Ni paleontology inahusika hapo mkuu ambayo ni evidence kubwa sana kuhusu uwepo wa evolution. Je wewe huamini paleontology??. Na kwanini unaona paleontology haipo sawa??. Je wewe unasadiki nadharia ipi ya asili ya uhai?.

Umeuliza nina uhakika gani na hizo mambo, hapa nadhani ndio maana mpaka leo evolution ni theory tu . Kinachofanya mpaka leo hii theory inaaminiwa na wengi ni kwa sababu inamake scientific sense. Ina biological plausibility.

Wakati Darwin anatoa hiyo theory ali Iback up na scientific proof na akatoa mifano mingi tu ya huko alikozunguka. Kwahiyo hapa am not re-inventing the wheel.
Kwanza bro sijui maana ya Paleontology. Kabla hatujaendelea nielezee maana yake na unipe mifano ikibidi.
 
Na sijajua mpaka sasa kwanini Historia imesimamia ktk msimamo huu licha ya sasa hivi kutambulika kuwa ni uwongo....
Inasimamia hapo kwa sababu hakuna hoja mbadala inayoeleza asili ya binadamu ili kuchukua sehemu ya hiyo unayosema ni ya uongo.pamoja na kwamba maswali na hoja zako zina mashiko.
 
Inasimamia hapo kwa sababu hakuna hoja mbadala inayoeleza asili ya binadamu ili kuchukua sehemu ya hiyo unayosema ni ya uongo.pamoja na kwamba maswali na hoja zako zina mashiko.
Inabidi wachukue vitabu vya Dini ndio vinaeleza vizuri mambo ya kale.....tubaki tukipambana na Sayansi tu kuujua ukweli wa chanzo cha binaadam
 
Naendelea kutafuta which is which kati ya binadamu kutengenezwa ma Aliens au Binadamu kuhamia dunian from other planets hizi kidogo zinamake sense kwangu ni proof tu napata tabu kidogo
 
Naendelea kutafuta which is which kati ya binadamu kutengenezwa ma Aliens au Binadamu kuhamia dunian from other planets hizi kidogo zinamake sense kwangu ni proof tu napata tabu kidogo
Hivi sanaa ya Allien au kisasili cha hawa Allien kimeanza kusikika lini ?
 
Sidhani kama huu uongo na upotoshaji bado unafundishwa kwenye shule zetu kwenye somo la historia....
Sisi tulifundishwa na kuaminishwa kuwa asili ya mwanadamu ni mnyama nyani.... Ni katika harakati za kutatua changamoto za maisha yanayomzunguka ndio akajikuta mpaka anaweza kusimama kwa miguu miwili na kutumia mikono kwa shughuli nyinginezo... Ithibati za kuunga zikionesha kutoka hatua za homo sapien mpaka homo habilis.. Ambaye sasa alikuwa ni binadamu kamili....
Kadiri tunavyozidi kuzama na kuhoji kuhusu hizi elimu na uhalisia wake ndivyo tunavyozidi kuangaziwa na kufunuliwa kuhusu uongo na upotoshaji mwingi kisayansi, kibaologia na kihistoria...
Ndana ya binadamu wa kwanza kutokana na nyani inawezekana kabisa ndio dhana dhaifu zaidi na inayoongoza kwa uongo na upotoshaji kuliko dhana nyingine zote kuhusiana na asili ya mwanadamu
Kuna maswali mengi ya kuhoji hapa
. Asili ya huyo nyani ni ipi?
. Kwanini baada ya hapo nyani wengine hawakupitia mchakato wa mabadiliko mpaka kuwa binadamu?
. Kwanini sasa nyani azae nyani na binadamu azae binadamu?
. Kwanini kusiwe na kinyume cha binadamu kuzaa nyani na nyani kuzaa binadamu?

Pamoja na mfanano wa vinasaba kati ya nyani na binadamu kwa zaidi ya asilimia 90.. Lakini ukweli unabaki kuwa hizi ni asili mbili tofauti kabisa
Dhana ya binadamu kubadilika umbo tangu kuumbwa kwa dunia inaweza kuwa na mashiko... Tukisoma misahafu tunaambiwa kuna watu waliishi zaidi ya miaka 800,Lakini pia kuna simulizi za wanefili, majitu makubwa yaliyoishi zamani...rejea zinjathropus
Kadiri miaka inavyosonga umri wa kuishi unazidi kupungua na hata maumbo pia.. Na hii si kwa binadamu tuu bali hata wanyama na vitu vingine vingi...
Dhana pekee ambayo mpaka sasa inajadilika ni Ile dhana ya uumbaji wa kiimani... Dhana ya asili ya mwanadamu na uumbaji wa kimungu...
Upotoshaji huu wa historia ulifanywa na watu maalum... Je lengo lao lilikuwa ninini?
Kitu kingine wanadaiii kadriii muda ulivozidiii kwenda uyo nyaniiiii alikua anabadilika kidogo ndo unakutana na akina homoerectus, homohabilis, zinja adii morden man homosapien sasa kwanini uyu morden man asiendeleee kubadilika awe kiumbe kingine kadriii muda unavyozidiii kwenda akwamie kwenye homosapien tu? Lakini walituaminisha kwamba fufu la binadamu wakwanza lilipatika uko gorge ya Olduvai sasa hawa waaarabu wazungu wachina ambao wao wana rangi ya tofauti na sisi walitokeaje tokeaje?
 
Naendelea kutafuta which is which kati ya binadamu kutengenezwa ma Aliens au Binadamu kuhamia dunian from other planets hizi kidogo zinamake sense kwangu ni proof tu napata tabu kidogo
Allies ni michezo ya warusi na wamarekani mbona hatujawahi kuwaona wakija Afrika?
 
Allies ni michezo ya warusi na wamarekani mbona hatujawahi kuwaona wakija Afrika?
Nimeacha kuamini sayansi ya anga na vyote vinavvyo husu sayansi hiyo kitambo sana.

Ila nilishangazwa na nilichokiona chuo mwaka wa kwanza. Kulikuwa na somo linaitwa "Development Study" katika topic "Science and Technology". Mwalimu akawa anazungumzia suala la natija ya sayansi na teknojia,akasema "Miongoni mwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ni kufanikiwa mtu kwenda mwezini. Nilisikitika sana. Nikajisemea tuna nini sisi ? Jambo ambalo uongo wake umefichuka zaidi ya miongo miwili na nusu sisi huku bado linapigiwa upatu ?

Kwa ufupi huwa siamini sayansi ya anga kutokana na uongo wake mwingi na kukithiri kwa maigizo yake.

Narudi kumalizia ile misingi kumi ya kila elimu........!
 
Naungana nawe katika hili... Nasubiria umalize palipobaki
 
Back
Top Bottom