WanaJF,
Leo kuanzia saa moja usiku nchi itazizima kwa kufanyika tukio kubwa la kihistoria hapa nchini wakati mabingwa kwa kihistoria nchini, Yanga na kampuni ya Laliga ya Spain watakapokuwa wanaingia mkataba wa kuanza kwa mchakato wa mabadiliko ya mfum wa uendeshaji wa timu ya Yanga
Mchakato huo wote utadhaminiwa na kampuni ya Chapa GSM ambao pia ni wadhamini na wafadhili wa klabu ya Yanga. Katika makubaliano hayo wataalamu wa La Liga kwa kushirikiana na Kamati ya Mabadiliko watafanya kazi kupata mfumo sahihi wa uendeshaji wa klabu.
Makubaliano hayo ya leo yatafanyika kwenye hotel ya Serena ya jijini Dar es Salaam na kurushwa live na Azam TV pamoja na youtube channel ya Yanga na kupitia social media zote za Yanga
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mh Jakaya Kikwete ataongoza dozeni ya viongozi watakaokuwepo hapo Serena Hotel kushuhudia historia hiyo ikiwekwa hapa nchini
Yanga sasa inakwenda kuwa klabu kubwa na tishio kabisa Africa
Kama ilivyokuwa ada ya JamiiForums, wanaJF tutakuwa hapa tukifuatilia tukio hilo na kuhabarishana kinachoendelea
Karibuni Sana
Wape Salamu