Historia : Mfahamu Ernesto Che Guevara

Historia : Mfahamu Ernesto Che Guevara

Bukayo jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
2,782
Reaction score
1,641
HISTORIA FUPI YA CHE GUEVARA

Che-Guevara-2.jpg

Jina kamili : Ernesto Guevara

Kazi : Daktari, mwanamapinduzi wa kijamaa (marxist)

Uraia : Argentina

Kuzaliwa : June 14 1928

Kufariki : October 9, 1967 ,Bolivia milima ya La heguera

Chanzo cha kifo : kuuwawa kwa kupigwa risasi


Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.

Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.

Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema

“wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”

MGOGORO WA CONGO – DRC

miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha
checongo.jpg

Che Guevara akiwa Congo mwaka 1966

baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores

KUKAMTWA NA KUUWAWA
Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,

Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema

“Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”


Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu René Barrientos kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale

Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
“Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”

Aliacha wake wawili na watoto watano


Corbis-HU006772.jpg


Che ndani ya ukumbi wa UN mwaka 1964
 
sasa mbona kwenye ma-tisheti anaonekana ana mindevu mingi?
 
Sa hv 2na makapi ya viongozi tu mkuu.ww toka miaka hyo w2 wanaona hi mifimo ya kibepari ni ya unyonyaji ulio pindukia leo hii sisi tuna copy & paste kila k2.
Mi,naamini kufuata njia yako pekee ni bora zaidi na kujifunza kiasi toka kwao.Na siku zote mtu akianzisha k2 au mwanzilishi wa jambo hata ufanye nn hutoweza mfikia technique zote atakua nazo,wnye hzo sera wanajua mwisho itakuwaje ila cc hatujui mwisho utakuwaje.
 
ukienda cuba...wanamwita ...che..daa jamaa alikua mpiganaji balaa..hv kwa nn leader kama hao hawapo ckuizi duniani?amebaki mugabe tu.
 
asante sana mkuu, naonaga mat-shirts yana picha za huyu jamaa, kweli alikuwa kamanda. shukrani
 
Maneno yake ya mwisho yamenisisimua sana na nusu chozi linitoke kwa kuwa nipo ndani ya hiace wakti nikisoma histori hii,hivyo nimejitahidi kuvumilia.
Nimejifunza mengi sana kuwa leo hii watawala hao hao walomua Guevara ndio wale wale wanaoendesha vita katika dunia ya leo na maisha ya wengi yatapotea.
Lakini mwisho wa yote wanafki hao watapotea.
Nampa pongezi sana bwana F. Castro na R. Castro kwa kuendelea kulilinda taifa lao,inawezekana mwisho wa tawala zao ndo ukawa mwisho wa utawala wa wacuba kujitawala.
Ni wakati sasa viongozi wazalendo kuhamka na Afrika kuungana.
Vyema KASHENGO,kama vipi naomba unitumie histori hiyo katika email yangu ya iddyallyninga@Gmail.com kama haitokuwa vibaya.
 
just a normal terrorist, hawa warloads ndio wameharibu Africa, sasa africa imejaa warlords na dogs wenginge .Kuifuta hii mentality ya kipuu haitokaa iishe kirahisi. Thinkers wa waafrica hawajajifunza sana kupima vitu ndio maana hooligans km che,malcolm x,ghaddafi wanaonekana mashujaa...ila hawaangalii mambo yao na fikra zao zinavyotutafuna hadi leo.Shida ni kwamba tunadhani enemy of our enemy is our friend.
 
just a normal terrorist, hawa warloads ndio wameharibu Africa, sasa africa imejaa warlords na dogs wenginge .Kuifuta hii mentality ya kipuu haitokaa iishe kirahisi. Thinkers wa waafrica hawajajifunza sana kupima vitu ndio maana hooligans km che,malcolm x,ghaddafi wanaonekana mashujaa...ila hawaangalii mambo yao na fikra zao zinavyotutafuna hadi leo.Shida ni kwamba tunadhani enemy of our enemy is our friend.

Hawa si war load kama kina Joseph konyi ,huyu che Guevara,Thomas Sankara n.k wanaofanana alikuwa wanamapinduzi wanaotafuta usawa na haki kwa wote na kupigana na mfumo wa kikoloni mamboleo na ubepari
 
Hawa si war load kama kina Joseph konyi ,huyu che Guevara,Thomas Sankara n.k wanaofanana alikuwa wanamapinduzi wanaotafuta usawa na haki kwa wote na kupigana na mfumo wa kikoloni mamboleo na ubepari
Che hana lolote, hakuna jambo kubwa alilolifanya mpaka dunia kumpa umashuhuri mkubwa kiasi hiki, alikuwa ni mamluki wa kivita tu, ni mtu aliye kuwa teyari kwenda kupigana vita popote, mfano Kongo DRC.

Kwa hotuba yake ya UN mwaka 1964 watu walimchukulia kama mwanamapinduzi wa kweli, ila kitendo cha kuwa mamluki wa kivita kilinifanya nimuone ni bure kabisa, angeweza kutumia madaraka alokuwa nayo wakati akiwa katika nafasi za kiuongozi Cuba ili kuendeleza movement zake, angeweza kuishi muda wa kutosha ili kuendeleza harakati hizo na agekuwepo kuonaa matunda kidogo ya uhuru wa africa tuliofikia kwa sasa.
 
"MGOGORO WA CONGO – DRC
miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che
alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na
hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae
ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba
na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na
baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika,
vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na
kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na
baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha"

Mwaka 1965 Ernesto Che Guevara ns Laurent Kabila wapi na wapi? Please check your facts
 
"MGOGORO WA CONGO – DRC
miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che
alitoweka katika maisha ya kawaida "public life" na
hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae
ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba
na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na
baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika,
vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na
kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na
baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha"

Mwaka 1965 Ernesto Che Guevara ns Laurent Kabila wapi na wapi? Please check your facts

Aisee we utakuwa mtoto mdogo unakataa usichojua kabisa pole sana

"Among Che's would-be Congolese allies was the then 26-year-old Laurent Kabila, who he met in the Fizi Baraka mountains, now soaring up above me from the Ruzizi River Plain which empties into Lake Tanganyika at the town of Uvira.

[TABLE="width: 203, align: right"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Laurent Kabila did eventually come to power, in 1997. But the revolution he headed was far from left-wing"

source : http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/4036605.stm

" Nonetheless, of all the people he met in the Congo, Che found himself most impressed by Kabila and he said in January 1966: "The only man who has genuine qualities of a mass leader is, in my view, Kabila."(p. 244) At the same time, Che believed Kabila was not quite serious enough for a revolutionary, "he is young and it is possible he will change."(p. 244)"

source : http://www.prisoncensorship.info/archive/etext/bookstore/books/africa/checongo.html
 
Back
Top Bottom