Historia : Mfahamu Ernesto Che Guevara

Historia : Mfahamu Ernesto Che Guevara

Che hana lolote, hakuna jambo kubwa alilolifanya mpaka dunia kumpa umashuhuri mkubwa kiasi hiki, alikuwa ni mamluki wa kivita tu, ni mtu aliye kuwa teyari kwenda kupigana vita popote, mfano Kongo DRC.

Kwa hotuba yake ya UN mwaka 1964 watu walimchukulia kama mwanamapinduzi wa kweli, ila kitendo cha kuwa mamluki wa kivita kilinifanya nimuone ni bure kabisa, angeweza kutumia madaraka alokuwa nayo wakati akiwa katika nafasi za kiuongozi Cuba ili kuendeleza movement zake, angeweza kuishi muda wa kutosha ili kuendeleza harakati hizo na agekuwepo kuonaa matunda kidogo ya uhuru wa africa tuliofikia kwa sasa.

Alifikiri atafanikiwa kama ilivyokuwa CUBA na haikutokea tena...after all alikuwa ni katika WANTED LIST na CIA siku nyingi toka alipokuwa GUATEMALA kabla hata ya kupindua CUBA...

unachosema ni kweli ila ilikuwepo sababu ya kutofautiana na FIDEL kwani aliwatukana URUSI kwa kurejesha MISSILES zilizokuwa zinapelekwa HAVANNA- CUBAbaada ya mkwara wa marekani....na hapo uhusiano wake na Fidel uliyumba akaona isiwe tabu akatoroka na kutokea ZAIRE
 
6208653911_dfb598250e.jpg


CHE with Late KWAME NKURUMAH
 
Aisee we uta
kuwa mtoto mdogo unakataa usichojua kabisa pole sana[/QUO
TE]

Jamani alichohoji ni sahihi. Kabila miaka ya 60? Labda wewe ndo hujui history.

"Among Che's would-be Congolese allies was the then 26-year-old Laurent Kabila, who he met in the Fizi Baraka mountains, now soaring up above me from the Ruzizi River Plain which empties into Lake Tanganyika at the town of Uvira"

SOURCE : BBC NEWS | Africa | Retracing Che Guevara's Congo footsteps

Si kila usichokijua hakipo
 
Nashukuru xana mleta mada!! Nilikuwa na hamu xana kumjua jamaa!!
 
Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.

Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.

Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema

“wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”

MGOGORO WA CONGO – DRC
miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha

baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores

KUKAMTWA NA KUUWAWA
Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilisha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,

Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema
“Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”

Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili asiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabla ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale

Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
“Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”

Aliacha wake wawili na watoto watano
 
Vijana wa Africa kusini mwa jangwa la sahara tuna kila sababu ya kufuata mstari alioufuata che guevara na wanamapinduzi wengine wengi walioanza wakiwa vijana.

Mapinduzi si lazima kwenda msituni kama che na castro. Tuanweza tumia wingi wetu kupanga mustakabali wa nchi hii kwa kuhakikisha tunapiga kura na kuchagua viongozi makini.

Na hata tukiwachagua, wakishindwa basi tuwe na uwezo wa kuingia mitaani na kupinga then tutafute wengine. Kwenye nchi ambazo vijana wana sauti, wanaheshimika sana.

Tukiachia hawa wazee waendelee kula nchi, itakwisha hii kwasababu hawana future. Mtu unakuta atakufa ndani ya next twenty years wewe ukijicheki una kama fifty au sixty years ahead. Je huyu kweli unamwachia future yako?

Tafakari
 
Vijana wa Africa kusini mwa jangwa la sahara tuna kila sababu ya kufuata mstari alioufuata che guevara na wanamapinduzi wengine wengi walioanza wakiwa vijana.

Mapinduzi si lazima kwenda msituni kama che na castro. Tuanweza tumia wingi wetu kupanga mustakabali wa nchi hii kwa kuhakikisha tunapiga kura na kuchagua viongozi makini.

Na hata tukiwachagua, wakishindwa basi tuwe na uwezo wa kuingia mitaani na kupinga then tutafute wengine. Kwenye nchi ambazo vijana wana sauti, wanaheshimika sana.

Tukiachia hawa wazee waendelee kula nchi, itakwisha hii kwasababu hawana future. Mtu unakuta atakufa ndani ya next twenty years wewe ukijicheki una kama fifty au sixty years ahead. Je huyu kweli unamwachia future yako?

Tafakari

Asante mkuu
 
Daaaa bonge lastori naskia alishawahi kufanya harakati za ukombozi kwa nchi zakusini mwa Africa MF.msumbiji kwa kupigana vita kabisa .
Vipi kuusu uraia wake kweli ni muajentina?? Kama ndio kwanini hakufanya harakati nchini mwake??
VP kuusuu watoto wake wanaendeleza harakati au ndio wamezimwa?
 
just a normal terrorist, hawa warloads ndio wameharibu Africa, sasa africa imejaa warlords na dogs wenginge .Kuifuta hii mentality ya kipuu haitokaa iishe kirahisi. Thinkers wa waafrica hawajajifunza sana kupima vitu ndio maana hooligans km che,malcolm x,ghaddafi wanaonekana mashujaa...ila hawaangalii mambo yao na fikra zao zinavyotutafuna hadi leo.Shida ni kwamba tunadhani enemy of our enemy is our friend.

You need to be "re educated" kama unaamini ulichoandika. Inawezekana pia ukweli unaujua ila u're an agent of imperialists
 
Daaaa bonge lastori naskia alishawahi kufanya harakati za ukombozi kwa nchi zakusini mwa Africa MF.msumbiji kwa kupigana vita kabisa .
Vipi kuusu uraia wake kweli ni muajentina?? Kama ndio kwanini hakufanya harakati nchini mwake??
VP kuusuu watoto wake wanaendeleza harakati au ndio wamezimwa?

Wanae wapo hai lakini sio Maxist kama baba yao alivyokuwa

Alipigana DRC wakati huo ikiitwa Zaire hakuingia Msumbiji

na ni kweli Raia wa Argentina mwenye Taaluma ya Udaktari
 
You need to be "re educated" kama unaamini ulichoandika. Inawezekana pia ukweli unaujua ila u're an agent of imperialists
re-education ipi tena?Utakuwa una hang over ya hawa wapuuzi.South Korea hawakufanya huu upuuzi sasa hivi wametupita kila kitu maadili na hata maendeleo.Che alikuwa jambazi tuu aliyepata uhalali kw akupigania upande wa magaidi wengine wajamaa waliojihalalaisha km rushwa inavyopewa majina mengine.
 
Back
Top Bottom