Historia : Mfahamu Ernesto Che Guevara

Historia : Mfahamu Ernesto Che Guevara

I will be like Ernest Che,,God Help me,,sipendi,kuona jinsi tunavyonywa na kuzid,kutawaliwa,,wazungu washenzi sana
 
HISTORIA FUPI YA CHE GUEVARA

Che-Guevara-2.jpg

Jina kamili : Ernesto Guevara

Kazi : Daktari, mwanamapinduzi wa kijamaa (marxist)

Uraia : Argentina

Kuzaliwa : June 14 1928

Kufariki : October 9, 1967 ,Bolivia milima ya La heguera

Chanzo cha kifo : kuuwawa kwa kupigwa risasi


Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.

Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.

Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema

“wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”

MGOGORO WA CONGO – DRC

miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha
checongo.jpg

Che Guevara akiwa Congo mwaka 1966

baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores

KUKAMTWA NA KUUWAWA
Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,

Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema

“Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”


Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu René Barrientos kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale

Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
“Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”

Aliacha wake wawili na watoto watano


Corbis-HU006772.jpg


Che ndani ya ukumbi wa UN mwaka 1964
Very poor Guy.Alikufa km terrorist wengine akisema maneno ya shujaa.Alipigana kumkomboa nani tena?Tz ya ccm?Cuba ya castro, zimbabwe ya mugabe, bolivia na colombia ya wauza unga? palestina ya wafilisti ambao siku hizi wanaitwa waarabu ,ingawa waarabu wanawaita wafilist hadi leo. Watu wamejilisha sana ujinga duniani.Na kupiga wrong wars.
 
"MGOGORO WA CONGO – DRC
miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che
alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na
hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae
ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba
na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na
baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika,
vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na
kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na
baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha"

Mwaka 1965 Ernesto Che Guevara ns Laurent Kabila wapi na wapi? Please check your facts
usiwe mbishi kijana, che alikuja congo na mtu,aliyeshirikiana naye ni kabira,kabira hakuanza harakati hizi juzi ni wa zamani tangu kifo cha patrice Lumumba 1960.
 
Watanzania ni lazima tuachane na kuiga historia za mnyonyaji bepari bali tuchukue historia za watu kama guevara tuziapply vema dhid ya bepari wa ndani na nje ya nchi yetu
 
Back
Top Bottom