Qwy
JF-Expert Member
- Nov 23, 2018
- 6,238
- 31,190
Alright, let's agree to disagreed on the so called facts. Umeelemea zaidi upande unaofurahisha nafsi yako na truly kuna mengi sana usiyoyafahamu na hauko tayari kuufungua ubongo wako kwa yale yasiyofurahisha nafsi yako.Qwy,
Unaweza kuamini upendavyo.
Siku zote mimi huwaambia wanaonisoma na kupinga haya ninayowaeleza kama ninavyoyajua kuwa si lazima wala si muhimu kwangu kwa wao wakaniamini.
Kwa miaka mingi walikuwa wakiamini historia rasmi na hakutokea mtu kuipinga.
Lakini mimi nilipokuja na historia ya kweli na ni kweli kwa sababu wazee wangu walihusika katika African Association hadi kuja kuunda TANU kwa hiyo ninajua mengi hapo ndipo waliposimama kupinga historia hii.
Mimi sina tattizo ya kupokea nisiyoyafahamu lakini pale ninapoona kuwa hayakubaliani na historia ya TANU ya wazee wangu kwa ''facts'' na ''chronology,'' hapo sina budi kusema niyajuayo.
Kuwa yale yaliyokuwa Kariakoo ndiyo kila kitu huu ni ukweli la huamini hapana shida unaweza kuamini kuwa harakati za kuunda TANU zilianza Tosamaganga.
Mimi nitakueleza kuwa mikutano yote ya siri ya kuunda TANU ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu na ni nyumba hii ndipo alipoishi Nyerere baada ya kuacha kazi mwaka wa 1955 na TANU ilipoundwa kadi ya TANU ya Abdul ni no. 3 na mdogo wake Ally ni no. 2 na Nyerere no.1.
Nitakueleza pia na kadi za TANU 1000 za mwanzo alichapisha Ally Sykes kwa fedha zake na hata usanifu wa kadi aliufanya yeye kutoka na kadi yake ya Tanganyika Legion.
Ikiwa historia ya TANU itaanza Tosamaganga ni wazi ni hii itakuwa ni TANU nyingine si hii iliyotokana na mazungumzo nyumbani kwa Hamza Mwapachu mwaka wa 1953 kati ya Abdul Sykes, Ali Mwinyi na Mwapachu mwenyewe kumjadili Nyerere.
Wala TANU hii haitakuwa TANU ya babu yangu Salum Abdallah ambae alikuwa akihudhuria mikutano yake ya siri kila Jumapili Town School Tabora mwaka wa 1953.
Wala sitasema kuwa mazungumzo hayo ya Tosamaganga hayakuwapo.
Labda nitauliza hiyo TANU ya Tosamaganga ilikuwa mwaka gani?
Kabla Nyerere hajafahamiana na Abdul Sykes au baadae?
Story ulizopewa na wazee wako inawezekana kabisa wakawa walizitia chunvi ili kuzinogesha au kudanganya kwa maslahi yao au kuchanganya ukweli na uongo au kusimulia tu baadhi ya matukio kwa faida au kuonekana walikuwa muhimu kuliko wanavyochukuliwa.
Anything is possible, hivyo kwenye hilo hatuwezi kufikia muafaka.
Sent using Jamii Forums mobile app