Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HISTORIA YA PEKEE YA PEMBA NA WAPEMBA
Wenyeji wangu wamenifikisha Wete kiasi cha saa nne asubuhi jua limepanda na mji umechangamka.
Gari yetu imeegesha pembeni na mkuu wa msafara katoka nje na kuvuka barabara kwenda upande wa pili.
Mimi nimelazimishwa lazima nikae kiti cha mbele naambiwa nipate kuiona Pemba vizuri.
Gari nzuri na imefunguliwa nasikiliza FM Station - Radio Istiqama.
Hii ni Radio ya Ibadh.
Nilipokuwa Tanga nilikuwa mjumbe wa Bodi ya Radio Istiqama ya Tanga kituo kilipofunguliwa.
Utastaajabu lakini ndiyo ukweli wenyewe radio inayosikilizwa ni hiyo tu.
ZBC haina wasikilizaji.
ZBC watu huifunguwa muda maalum kusikiliza matangazo ya vifo.
Bado niko ndani ya gari emeegeshwa pembeni ya barabara.
Jicho la camera yangu limevutiwa na mnara mrefu wa msikiti mkubwa lakini naona pia nyumba zilizochakaa kupita kiasi pembezoni yake ingawa mjengo wa nyumba hizi unaonyesha zilikuwa wakati wake nyumba za kupendeza.
Nimewauliza wenyeji wangu kuhusu nyumba moja iliyochoka iweje iachiwe kuporomoka kiasi kile.
"Hiyo ni ofisi ya serikali zamani ilikuwa nyumba ya mtu binafsi na bwana huyu mwenye nyumba hiyo alikuwa mtu mwema, karimu akisaidia shughuli nyingi za Kiislam.
Mtaa mzima huo ulikuwa na nyumba nzuri za watu wema.
Wema huu uliondoka na mapinduzi mwaka wa 1964 na hadi leo mtaa na majengo yote mazuri yamejiinamia."
"In Shaa Allah nema na salama vitarejea," nawaombea dua ndugu zangu.
Nimekuwa mzoefu wa historia ya Zanzibar na mimi binafsi ili kupoza machungu ya historia ya visiwa hivi hupenda kutazama historia hii kama, "tragicomedy," (kichekesho ndani ya huzuni) yaani mimi hutafuta lililo laini ndani ya ugumu wa historia ya Zanzibar kulieleza.
Kukaa ukaekeza machungu matupu kunaumiza nafsi.
Jicho langu linarejea kwenye ofisi ya serikali iliyokuwa nyumba ya kuishi.
Hakika iko hoi.
Kuta zinahitaji rangi.
Nje kuko hivi ndani kutakuwaje?
Kichekesho kikanijia nikacheka.
Jicho langu sasa likaangukia nje ya dirisha la gari.
Nakaribishwa na maandishi yaliyopo kwenye barza ya kahawa: "Karibu Domo Free Kazi Iendelee."
Haraka nikapiga picha kimya kimya.
Nasoma maneno kutoka Qur'an Tukufu: "Fantashiruu Fil Ardhi," hayako mbali na, "Domo Free Kazi."
Najichekea moyoni.
Najiuliza kama hii barza naweza kuipa jina la Kiswahili, "Kazi Bure."
Tupia jicho lako kwenye meza iliyo na jiko la mkaa na mabirika ya kahawa hapo chini kwrnye picha.
Hao hapo ndiyo Wapemba.
Nimeelezwa kuwa Mpemba akikuambia, "Nakuja," msubiri.
Ukimsikia kasema, "Naja ondoka haraka."
Hapana tena salama hapo.
Haya nimeelezwa Kojani.
Wakojani ni mabingwa wa bahari.
Hawaiogopi bahari na vitimbi vyake.
Kwa Wakojani sufuria imepata mfuniko.
Bahari inamuheshimu Mkojani sembuse binadamu?
Nilishuka kutoka kwenye gari nikawatolea salama wanabarza wa "Domo Free," ukipenda, "Kazi Bure."
Waliniitikia na wakaendelea na mazungumzo yao wakizungumza kwa sauti ya chini.
Lakini nilijua toka mwanzo kuwa walikuwa wakinitazama na walijua kuwa mimi ni mgeni.
"Huyu mtu kafuata nini?"
Hili lazima walijiuliza.
Huwa wakati mwingine najiambia mweyewe nimesoma mengi kuhusu Gestapo kiasi kila sehemu nifikayo yenye historia ya mateso naingiwa na hofu.
Pemba ina mgao wake wa kutosha wa historia ya kusikitisha.
Wenyeji wangu wakanifahamisha kuwa barza mfano wa hiyo ziko Pemba nzima na yalikuwa matawi ya CUF sasa ni ya ACT Wazalendo na kahawa katika matawi hayo ni bure si biashara.
Pita barzani toa taarifa au kunywa kahawa nenda na hamsini zako.
Matawi haya yana nguvu isiyomithilika.
Usidanganyike na ile kahawa na chochote kilicho machoni pako.
Wapiga kura wao wanafahamika kwa sura na majina na wanajigamba hawajapata kupiga kura iliyoharibika wala kushindwa uchaguzi.
Barza hii ipo jirani na uwanja ambako baada ya mapinduzi wananchi walikuwa wakiletwa kupigwa viboko hadharani.
Miaka ni mingi imepita na nimesimama mahali watu wakiadhibiwa kwa viboko lakini uwanja ule wa henzerani haupo tena.
Kilichobakia ni historia ya viboko vile na majina ya wapigaji viboko.
Mmoja aliyekuwa akisimamia adhabu hii ya kudhalilisha tulikuja kufahamiana vyema Dar es Salaam.
Lakini naamini kwa wakati ule alikuwa kajuta maana alikuwa mcha Mungu.
Mmoja wa rafiki zangu aliniambia katika sifa zake alikuwa kahifadhi Barzanji yote kifuani.
Turudi vibokoni.
Waliopigwa viboko vile baadhi wa hai na ukisimama mahali pale ukawatafuta utawapata.
Nilibahatika kukutana na mmojawapo.
Pemba ina historia nzito na ina watu tofauti sana kwa kila kitu.
Nidhamu ya watu wake ni ya kipekee.