Nemo...
Shule ilijengwa na ndiyo shule aliyosoma baba yangu na watoto rika lake kama Abdul na Ally Sykes, Mwalimu Sakina na nduguye Mwalimu Fatna na hawa akaina mama wakajakuwa waalimu shuleni hapo katika miaka ya 1950 na kuendelea.
Shule hii ilikuwa ikisomesha Qur'an, Lugha ya Kiarabu na masomo mengine ya kisekula.
Kiarabu ambacho wazee wetu walipokuwa wakifurahi wakikimwaga walikipata hapo.
Mchanganyiko huu wa lugha hizi mbili Kiarabu na Kiingereza ndiyo iliwafanya wazee wetu wakizungumza Kiingereza utaburudika na ile ''accent,'' yao.
Naambiwa Julius Nyerere akipenda sana kumsemesha Abdul Kiingereza labda alikuwa akifurahishwa na ile ''accent,'' yake.
Mzee Abdallah aliyekuwa muhudumu ofisini kwa Abdul Sykes alipata kunihadithia siku Mzungu Town Clerk alipomvamia Abdul Sykes ofisini kwake Kariakoo Market akamkuta anauza kadi za TANU.
Mzee Abdallah anasema yeye alikuwapo pale siku ile na ingawa hajui Kiingereza lakini alikuwa akistarehe kusikiliza jinsi Abdul Sykes na Mzungu walivyopambana kwa Kiingereza.
Mzee Abdallah anasifia ananambia, ''Abdul alikuwa anasema Kizungu kama maji.''
Kuhofia Abdul kufukuzwa kazi ndiyo wazee wa Dar es Salaam wakaamua kumfanyia Abdul dua kama ile waliyomfanyia Mwalimu Nyerere baadae ambayo imekuwa maarufu watu wengi wanapenda kuihadithia pale wazee walipomwambia Nyerere baada ya kuruka damu, ''Twining amekwisha.''
Historia ya TANU ilikuwa na mikasa.
Dua nyingine aliyofanyiwa Nyerere ilikuwa Lindi dua iliyofanywa na Sheikh Yusuf Badi na dua ya mwisho ni dua ya Uchaguzi wa Kura Tatu Tanga, Mnyanjani mwaka wa 1958, dua ya akina Sheikh Rashid Sembe, Mmaka Omari na Hamisi Heri.
Naona hii ndiyo ilikuwa dua ya kuleta uhuru.
Baada ya hapo uhuru mwaka wa 1961
Serikali imetaifisha Al Jamiatil Islamiyya School na Waislam wameomba warejeshewe shule yao lakini hadi leo zaidi ya miaka 20 wanazungushwa ilhali St. Joseph'Convent ilipoombwa tu ikarejeshwa kwa wenyewe,