Historia ya Abbas Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere (1952 – 1999)

Historia ya Abbas Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere (1952 – 1999)

Miradi mingi tu Tanzania yenye ufadhili, ipo baadhi ina hali mbaya
Dude, makanisa ya Wakatoliki yanajengwa imara na yanakuwa solid architectural structures na kamwe hayawezi kuwa nyang'anyang'a kama misikiti ya Waislam. Njoo Mbweni JKT uone pamoja na misaada ya Oman, msikiti una nyufa, fence haijamalizika tokea 2017 na waumini wanaruka vidimbwi na matope sehemu wazi za fence ili kuingia msiktini sababu hakuna main and single gate.
 
Silijui hilo suala la ujenzi wa huo msikiti,tusaidie kutuhabarisha kwa kina
 
Silijui hilo suala la ujenzi wa huo msikiti,tusaidie kutuhabarisha kwa kina
Zaidi ya mapungufu niliyogusia itabidi uje uone mwenyewe kwa macho kama uko so keen in finding out about the mediocrity of it all.
 
Shukrani Kwa Historia nzuri Mzee Said, na jitihada zako na Wazee wako simulizi adimu sana hizi kuzipata
Nemo...
Afwan.

Hii ndiyo historia ya wazee wangu ambayo imefungamana na historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Huwezi kuandika historia ya TANU bila ya kututaja.
 
KUSAJILIWA KWA TANU ABDUL NA ALLY SYKES WALIMSUBIRI NYERERE MTAA WA KIPATA
Mwalimu wangu aliyenifunza mbinu za kufanya mijadala marehemu Sheikh Haruna Fakir alikuwa heshi kutueleza, ''Haleti mtu matusi katika mjadala ila ameghadhibika na huku kughadhibika husababishwa na kushindwa akawa hana uwezo tena wa kushindana basi hapo nafsi huingia katika fadhaa na matokeo yake ndiyo hayo matusi.''

Wakati ujumbe wa umoja wa mataifa ulipofika Tanganyika, TANU ilikuwa bado haijasajiliwa na serikali.

TANU ilipata tasjila yake tarehe 30 Desemba, 1954 baada ya kuzishinda hila nyingi na vizingiti vilivyowekwa na serikali za kupinga usajili wake.

Bi Zainabu, mke wa Ally Sykes anakumbuka siku moja adhuhuri, jua lilikuwa kali, wakati Nyerere alipokwenda nyumbani kwao Mtaa wa Kipata (Siku hizi Mtaa wa Kleist) ambako Ally na kaka yake Abdulwahid walikuwa wakimsubiri atoke mjini alikokwenda kushughulikia tasjila ya TANU.

Alipofika Nyerere alionekana amechoka taabani na mwenye wasiwasi.
Alizama ndani ya sofa akaufunika uso wake kwa mikono yake na akakaa kimya kwa muda.

Abdulwahid na Ally walikuwa wakimsubiri azungumze.
Nyerere alikuwa na habari mbaya.

Serikali ilikuwa imekataa kuisajili TANU.
Nyerere aliwaambia kuwa serikali ilikataa kutoa usajili kwa sababu za kiufundi.

Serikali ilidai kuwa TANU haikuwa na wanachama.

Baada ya kufahamu kuwa serikali imekataa maombi ya TANU kwa kuwa ati haikuwa na wanachama wa kutosha, mithili ya onyesho la mchezo wa kuigiza unaokwenda haraka, Abdulwahid alitumia hekima na mara moja akamuomba Said Chamwenyewe aende nyumbani kwao Rufiji kusajili wanachama kwa ajili ya TANU.

Rufiji ni sehemu ya Waislam watupu.
Kwa ajili hii TANU haikuwa na tatizo la kuwapata wanachama.

Kwa hakika wanachama wa mwanzo wa TANU walikuwa kutoka Gerezani na Rufiji.

Illife ameandika kuwa:

"Mwelekeo wa kuungwa mkono kwa TANU mjini Dar es Salaam unahitaji uchunguzi, lakini mapato ya fedha kwa mwaka 1958 yanaonyesha sehemu iliyo kubwa ya kuungwa mkono chama ilikuwa kutoka makazi ya Waafrika - Kariakoo, Ilala, Gerezani... kufikia Septemba, 1955 Dar es Salaam ikiwa na watu kama 110,000 - ilichukua kiasi cha 25,000 kati ya 40,000 za kadi za uanachama wa TANU zilitolewa kote nchini.

Huu ulikuwa ndiyo msingi ambao TANU iliteka Tanganyika.''

Abdulwahid sasa akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa amekamilisha lile lengo lake kubwa katika maisha yake, lengo ambalo lilianza kwa marehemu baba yake ambaye miaka ishirini na moja iliyopita alitabiri kuendelea kwa mapambano kati ya Waafrika wa Tanganyika na serikali ya kikoloni.

Kleist Sykes alikuwa halikadhalika ametabiri jukumu la kizazi kijacho.

Katika barua aliyomwandikia Mzee bin Sudi, Rais wa African Association, mwaka wa1933, Kleist katika umri mdogo wa miaka ishirini na tisa, akiwa kijana mdogo sana aliandika maneno haya:

"Tupambane kwa nguvu zetu zote kuelekea njia ya ustaarabu kama vile watu wa makabila mengine wanavyofanya.

Haidhuru kitu ikiwa hatukamilishi kila kitu.
Wale watakaokuja baada yetu watakamilisha yatakayobakia."

Kwa hakika Kleist alikuwa mtu wa fikra.

Alizungumzia kuhusu ''ustaarabu'' ambao hivi leo ungemaanisha ''kujitawala'' na kuhusu makabila ambayo TANU imeyageuza kuwa ''taifa.''

Katika mwaka wa 1954 robo karne baadaye katika jengo lilo hilo, 25 New Street ambalo Kleist alisaidia kulijenga kwa njia ya kujitolea, kizazi kipya nchini Tanganyika kilikuwa kikiigeuza African Association aliyoiunda katika mwaka 1929 kuwa chama cha siasa.

Lengo lake lilikuwa kuwatayarisha Watanganyika kujitawala.

Miongoni mwa waliokuwa wakiongoza harakati za kudai uhuru zilizokuwa zikiibuka walikuwa watoto wake watatu, Abdulwahid, Ally na Abbas."

Bahati mbaya sana nyumba yenyewe haipo hivi sasa badala yake wamejenga ghorofa hiyo hapo chini katika kiwanja kile ilipokuwapo nyumba hii.
Hii nyumba ndipo Ally Sykes alipoficha mashine ya aliyokuwa akichapa makaratasi ya uchochezi dhidi ya Waingereza na kuyasambaza nchi nzima.

1574308507308.png
 
Nemo,

View attachment 1267416
Kushoto waliokaa: Kleist Sykes (1994 -1949), Abbas Sykes (1929 - ),
Nyuma kushoto Ally Sykes (1926 - 2013), Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
Picha hii ilipigwa 1942 Abdul Sykes aliporudi Dar es Salaam kuaga kutoka Lower Kabete
Kenya kabla ya kwenda Burma Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) akiwa katika
King's African Rifles (KAR)

View attachment 1267431
Bi. Mruguru bint Mussa (1909 - 1974) mke wa Kleist Sykes
na mama wa watoto wake wote watatu

Allama, ipitie tena miaka kwenye picha, naona kuna "error".
 
Nemo,
Mbona mjadala umegeuka imekuwaje?
Katika yote haya ninayoeleza hakuna la kuchangia?

Mzee Said

Samahani sikupenda kuchafua mjadala, nilikua namjibu huyo ndugu hapo juu kuwa mjadala wake sio sehemu sahihi.

Ni msingi kujikita kwenye Historia unayotumegea.
 
Allama, ipitie tena miaka kwenye picha, naona kuna "error".
Maalim Faiza,
Toka jana nimeelezwa na tayari nisasahihisha ila hiyo kwa kuwa ni caption katika whatsapp hakuna option ya edit kwa hiyo itabaki hivyo hivyo hadi nitakapo delete na kuweka upya.
 
Allama, ipitie tena miaka kwenye picha, naona kuna "error".

Nemo,

View attachment 1267416
Kushoto waliokaa: Kleist Sykes (1894 -1949), Abbas Sykes (1929 - ),
Nyuma kushoto Ally Sykes (1926 - 2013), Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
Picha hii ilipigwa 1942 Abdul Sykes aliporudi Dar es Salaam kuaga kutoka Lower Kabete
Kenya kabla ya kwenda Burma Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) akiwa katika
King's African Rifles (KAR)

View attachment 1267431
Bi. Mruguru bint Mussa (1909 - 1974) mke wa Kleist Sykes
na mama wa watoto wake wote watatu
 
Maalim Faiza,
Toka jana nimeelezwa na tayari nisasahihisha ila hiyo kwa kuwa ni caption katika whatsapp hakuna option ya edit kwa hiyo itabaki hivyo hivyo hadi nitakapo delete na kuweka upya.

1574307233104.png

Kushoto waliokaa: Kleist Sykes (1894 -1949), Abbas Sykes (1929 - ),
Nyuma kushoto Ally Sykes (1926 - 2013), Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
Picha hii ilipigwa 1942 Abdul Sykes aliporudi Dar es Salaam kuaga kutoka Lower Kabete
Kenya kabla ya kwenda Burma Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) akiwa katika
King's African Rifles (KAR)
 
akina Sykes, Collymore, Titi Mohamed , Kambona, walimsaliti Nyerere kwa kutaka kumpindua
 
Ally Sykes, Collymore walikimbilia Kenya baada ya jaribio lao la kumpindua Nyerere kushindikana
 
akina Sykes, Collymore, Titi Mohamed , Kambona, walimsaliti Nyerere kwa kutaka kumpindua
Laki...
Jina ni Peter Colmore.
Taarifa zako nyingi si za kweli.

Inaelekea wewe hujui historia za watu unaowaandika.

Colmore maisha yake yote ameishi Nairobi mimi nikimjua vyema toka udogo wangu tuliishi jirani ya ofisi yake ya Dar es Salaam Mtaa wa Lindi karibu na International Hotel.

Katika miaka ile ya 1960s hii ilikuwa hoteli kubwa sana ni kuvuka Mnazi Mmoja kuelekea Nkrumah Street.

Ofisi hii ilikuwa ndiyo ofisi ya Ally Sykes.

Hawa wawili walikuwa watu wa biashara na Colmore hakukimbia ila alimwachia ofisi ile partner wake Ally Sykes baada ya kuona biashara ni ngumu Tanzania na yeye akaendelea na biashara Kenya.

Hii ilikuwa 1971.

Ile nyumba ambayo ilikuwa ofisi yao akamuuzia Ally Sykes.

Nyumba hii ilitaifishwa lakini Ally Sykes alirejeshewa hii nyumba na Rais Ali Hassan Mwinyi.

Iko siku nilipata hamu ya kwenda kuona mtaa tulioishi 1964 hapo karibu na ofisi ya Colmore.

Ilinichukua muda mrefu kuiona nyumba ile na kwa kweli sikuitambua kwa haraka.

Ilikuwa nyumba ya gorofa moja na ngazi za kupandia zilikuwa nje pembeni ya nyumba.

Nyumba tuliyokuwa tukiishi imevunjwa kuna gorofa ndefu.

Kulikuwa na njia ya mkato inatokea Chox Cinema.

Kote kumebadilika ile barabara kuna majengo.

Zaidi ya miaka 50 imepita.

Sina taarifa kuwa watu hawa walifanya jaribio la kupindua serikali.

Ally Sykes alibakia Dar es Salaam hadi alipofariki 2013.
 
Mohamed Said Hivi kweli Umeshindwa kusema "Waislamu wawili" ???!!
Ndivyo wanavyojulikana...

Qadiani or Qadiyani refers to Ahmadi Muslims, primarily in Pakistan. The term originates from Qadian, a small town in northern India, the birthplace of Mirza Ghulam Ahmad, the founder of the Ahmadiyya movement. While it is pejorative to the Ahmadiyya Muslim Community, it is used in official Pakistani documents. Wikipedia
 
Back
Top Bottom