AVRAM,Sheikh Mohammed Said hawa wanaokataa hii hustoria unayokuja nayo hapa, kama wanaona si kweli wangekuja na yao ingependeza kwelikweli, ila nafkiri wasifanye chuki na maandiko yako bali wanachopaswa ni kujiuliza kwanini unachokijiua wewe hakifanani na walichonacho vichwani mwao.
Nemo,Mzee Said, Abbas Ni mtoto wa nani? Nipe mtiririko vizuri kuanzia baba yao hadi hawa akina Abass na Kaka zake
Nemo,
View attachment 1267416
Kushoto waliokaa: Kleist Sykes (1994 -1949), Abbas Sykes (1929 - ),
Nyuma kushoto Ally Sykes (1926 - 2013), Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
Picha hii ilipigwa 1942 Abdul Sykes aliporudi Dar es Salaam kuaga kutoka Lower Kabete
Kenya kabla ya kwenda Burma Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) akiwa katika
King's African Rifles (KAR) kabla ya kwenda Burma
View attachment 1267431
Bi. Mruguru bint Mussa (1909 - 1974) mke wa Kleist Sykes
na mama wa watoto wake wote watatu
Asante kwa picha nzuri Mzee Said,
Aliyewahi kuja kuwa Meya wa Jiji ni nani?
Nemo...,Ambaye ni Mtoto wa Abdulwahid, Asante sana
Nemo...,
Watu wanasema dunia inazunguka na historia inajirudia.
Picha ya Kleist Abdulwahid Sykes ambae alizoeleka kwa jina la Kleist Sykes akiwa na Karim Aga Khan mimi imenirudisha nyuma karibu sasa miaka 90.
Babu yake Karim Aga Khan, Sultan Mohamed Shah alikuja Tanganyika mwaka wa 1936 na katika sehemu alizotembelea Dar es Salaam ilikuwa shule ya Al Jamiatul Islamiyya mtaa wa New Street na Stanley Street.
Hii Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika iliasisiwa na wale wale wazee wa Dar es Salaam walioasisi African Association.
Waasisi wa African Association wengi wao walikuwa Waislam wakiongozwa na Kleist Sykes.
Tatizo lililojitokeza ilikuwa hata matatizo ya Waislam yakawa yanapitishwa kupitia African Association ambayo kilikuwa chama ambacho hakikutakiwa kufangamana na dini yoyote.
Kwa ajili hii basi wazee wetu wakaona itakuwa bora waunde Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Ndipo Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ikaundwa mwaka wa 1933.
Alipokuja Aga Khan Tanganyika ana kutembelea Al Jamiatula Islamiyya akakuta pana shule inajemgwa lakini haijamilika.
Abdul Sykes akiwa mwanafunzi wa shule hii ndiyo aliyosoma risala ya kumkaribisha Aga Khan.
Aga Khan alivutiwa sana na juhudi hizi za Waislam na katika kujibu risala ile akajitolea kukamilisha ujenzi wa shule pamoja na ofisi za Al Jamiatul Islamiyya.
Kleist Sykes alikuwa na uhusiano mzuri na jamii ya Ismailia kwani yeye alikuwanao katika Dar es Salaam Chamber of Commerce na inaaminika ndiye alikuwa Mwafrika wa kwanza kujiunga na taasisi hii ya wafanyabiashara.
Sasa nikiangalia picha hiyo nikawa nakumbuka historia ya familia hizi mbili kuwa kijana Abdul akiwa na umri wa miaka 12 alikutana na babu yake Karim Aga Khan na ikasadif mi
Nemo...Jitihada za Kleist Sykes kuanzisha shule, au Umoja huo kuanzisha shule ziliishia wapi, je walikwamishwa na nini? au ipo taasisi madhubuti iliyoanzishwa na wazee hao ingali Mpaka sasa?
tatizo una miemko... relaxTatizo ni ulivyojaa hila za makusudi!!
Kusoma kutabu kuhusu Mwalimu ndii kumfahamu kuliko wanavyomfahamu wanae na mkewe?
Nataka siku moja useme hapa, kuwa ulienda kwa mama Maria akakuambia hivi kuhusu hiki! Au unangoja nae afe ili uanze kuandika kwa kupotosha?
Uache kuandika huku unachomeka hila, na upotovu....la sivyo wengine tutaendelea kukudharau kama tinavyovidharau vitabu vingi tu vilivyojaa hila na upotoshaji!
Kulikoni kila mara unaishia ku compare na ku contrast kati ya Waislamu na Wakatoliki? Nauliza, Singasinga, Baniani, Ahmadiyya, Ismailia hata Walutheri, Mabudha na Wapentekoste nao vipi vis-a-vis Uislamu wako?Serikali imetaifisha Al Jamiatil Islamiyya School na Waislam wameomba warejeshewe shule yao lakini hadi leo zaidi ya miaka 20 wanazungushwa ilhali St. Joseph'Convent ilipoombwa tu ikarejeshwa kwa wenyewe,
Nemo...
Shule ilijengwa na ndiyo shule aliyosoma baba yangu na watoto rika lake kama Abdul na Ally Sykes, Mwalimu Sakina na nduguye Mwalimu Fatna na hawa akaina mama wakajakuwa waalimu shuleni hapo katika miaka ya 1950 na kuendelea.
Shule hii ilikuwa ikisomesha Qur'an, Lugha ya Kiarabu na masomo mengine ya kisekula.
Kiarabu ambacho wazee wetu walipokuwa wakifurahi wakikimwaga walikipata hapo.
Mchanganyiko huu wa lugha hizi mbili Kiarabu na Kiingereza ndiyo iliwafanya wazee wetu wakizungumza Kiingereza utaburudika na ile ''accent,'' yao.
Naambiwa Julius Nyerere akipenda sana kumsemesha Abdul Kiingereza labda alikuwa akifurahishwa na ile ''accent,'' yake.
Mzee Abdallah aliyekuwa muhudumu ofisini kwa Abdul Sykes alipata kunihadithia siku Mzungu Town Clerk alipomvamia Abdul Sykes ofisini kwake Kariakoo Market akamkuta anauza kadi za TANU.
Mzee Abdallah anasema yeye alikuwapo pale siku ile na ingawa hajui Kiingereza lakini alikuwa akistarehe kusikiliza jinsi Abdul Sykes na Mzungu walivyopambana kwa Kiingereza.
Mzee Abdallah anasifia ananambia, ''Abdul alikuwa anasema Kizungu kama maji.''
Kuhofia Abdul kufukuzwa kazi ndiyo wazee wa Dar es Salaam wakaamua kumfanyia Abdul dua kama ile waliyomfanyia Mwalimu Nyerere baadae ambayo imekuwa maarufu watu wengi wanapenda kuihadithia pale wazee walipomwambia Nyerere baada ya kuruka damu, ''Twining amekwisha.''
Historia ya TANU ilikuwa na mikasa.
Dua nyingine aliyofanyiwa Nyerere ilikuwa Lindi dua iliyofanywa na Sheikh Yusuf Badi na dua ya mwisho ni dua ya Uchaguzi wa Kura Tatu Tanga, Mnyanjani mwaka wa 1958, dua ya akina Sheikh Rashid Sembe, Mmaka Omari na Hamisi Heri.
Naona hii ndiyo ilikuwa dua ya kuleta uhuru.
Baada ya hapo uhuru mwaka wa 1961
Serikali imetaifisha Al Jamiatil Islamiyya School na Waislam wameomba warejeshewe shule yao lakini hadi leo zaidi ya miaka 20 wanazungushwa ilhali St. Joseph'Convent ilipoombwa tu ikarejeshwa kwa wenyewe,
Kulikoni kila mara unaishia ku compare na ku contrast kati ya Waislamu na Wakatoliki? Nauliza, Singasinga, Baniani, Ahmadiyya, Ismailia hata Walutheri, Mabudha na Wapentekoste nao vipi vis-a-vis Uislamu wako?
Ndjabu,Kulikoni kila mara unaishia ku compare na ku contrast kati ya Waislamu na Wakatoliki? Nauliza, Singasinga, Baniani, Ahmadiyya, Ismailia hata Walutheri, Mabudha na Wapentekoste nao vipi vis-a-vis Uislamu wako?
Nemo,
View attachment 1267416
Kushoto waliokaa: Kleist Sykes (1994 -1949), Abbas Sykes (1929 - ),
Nyuma kushoto Ally Sykes (1926 - 2013), Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
Picha hii ilipigwa 1942 Abdul Sykes aliporudi Dar es Salaam kuaga kutoka Lower Kabete
Kenya kabla ya kwenda Burma Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) akiwa katika
King's African Rifles (KAR)
View attachment 1267431
Bi. Mruguru bint Mussa (1909 - 1974) mke wa Kleist Sykes
na mama wa watoto wake wote watatu
Wao ni kina nani hao? Muddy et al? Kama ni ndiyo, Muddy et al ni nani? Nipo Mbweni hapa nimepita local mosque asubuhi hii, nashangaa msikiti mpya lakini umezungukwa na vichaka ndani na nje, kuta za msikiti zishajenga nyufa halafu kuna bango barabarani lenye picha za bendera za TZ na Oman, na kwamba fence imejengwa kwa msaada wa Waislamu wa Uarabuni.Mkuu usiwe na jazba, tupo imani tofauti humu ila tusichukulie kwa mitazamo mibaya, je si haki kwa wao kutodai haki hiyo? Je sababu za kuporwa ni zipi?
Wao ni kina nani hao? Muddy et al? Kama ni ndiyo, Muddy et al ni nani?
Njoo Mbweni JKT uone msikiti wao ulivyo licha ya misaada kutoka Waarabu wa Oman ilhali huyu Muddy kutwa anajamba jamba Sykes na kulalama wanaonewa na adui yake mkubwa ni Wakatoliki via Serikali.