Historia ya ajabu ya kisiwa cha Pitcairn

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Miaka ya Nyuma Mabaharia waasi maarufu walioizamisha meli ya Kiingereza iliyoitwa Bounty waliishia kufanya makazi yao wakiwa pamoja na wanawake, wenyeji wa eneo lile katika kisiwa cha Pitcairn katika Bahari ya Pasifiki ya Kusini.

Kundi hili lilikuwa na mabaharia tisa wa Kiingereza, wanaume wa Kitahiti sita, wanawake wa Kitahiti kumi, na msichana wa miaka kumi na mitano.

Mmojawapo wa mabaharia wale alivumbua namna ya kutonyesha [kugeuza kuwa mvuke] alkoholi, na baada ya muda mfupi ulevi ukaliharibu koloni lile lililokuwa katika kisiwa kile.

Ugomvi kati ya wanaume na wanawake ukageuka na kuwa wa kutumia nguvu.

Baada ya kupita muda fulani mmoja tu kati ya wanaume wale wa kwanza waliofika mle kisiwani ndiye alibaki kuwa hai.

Moja ya hawa watu aliyebaki alikuwa anaitwa Alexander Smith, alikuwa ameigundua Biblia katika mojawapo la makasha yaliyochukuliwa kutoka katika ile meli.

Alianza kuisoma na kuwafundisha wengine juu ya kile ilichosema. Alipofanya hivyo maisha yake yeye mwenyewe yakabadilika na hatimaye maisha ya wote waliokuwa katika kisiwa kile.

Wakazi wa kisiwa kile walikuwa wametengwa na ulimwengu wa nje mpaka ilipowasili meli ya Kimarekani iliyoitwa Topaz katika mwaka wa 1808.

Wafanyakazi katika meli hiyo wakakikuta kisiwa kile kikiwa na jumuia inayokua na kusitawi, bila ya kuwa na pombe kali (wiski), gereza, wala uhalifu.

Biblia ilikuwa imekigeuza kisiwa kile kutoka jehanamu ya duniani kwenda katika kielelezo cha vile Mungu atakavyo ulimwengu huu uwe.

Na mpaka leo hii kinaendelea kuwa katika hali hiyo.

Je, hivi Mungu bado anaendelea kusema na watu kupitia katika kurasa hizo za Biblia?

Bila shaka anafanya hivyo.

images%20(4).jpeg
images%20(3).jpeg
images%20(2).jpeg
images%20(1).jpeg
 
Thibitisha.
Nithibitishe nini tena?

Siku moja jamaa mmoja anaitwaJimi alimwuliza mtu mmoja anayekana kuwa kuna Mungu endapo alipata kujaribu sana, hata kwa dakika chache tu, kupigana na wazo lisemalo kwamba huenda Mungu yuko.

“Sawa kabisa!” mkana Mungu yule akajibu, akimwacha Jimi na mshangao. “Miaka mingi iliyopita, mimi nilikuwa karibu sana nigeuke na kuwa mtu anayemwamini Mungu. Nilipokiangalia kile kiumbe kidogo sana lakini kikamilifu katika kitanda chake kidogo, nilipochungulia na kuviona vidole vile vidogo fahamu za kwanza za kutambua, nilipita katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo katika hiyo mimi nilikuwa karibu kabisa niache kuwa mkana Mungu. Kule kumwangalia mtoto yule kulikuwa kumenishawishi karibu kabisa kuwa hapana budi Mungu alikuwa yuko.”

person-1317770_640.jpeg
 
Alaa, kumbe Ukristo ni dini "kikongwe" (kibabu)!![emoji1787][emoji1787].

Uislamu ni dini ya kisasa (modern)
Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK.
 
Nithibitishe nini tena?

Siku moja jamaa mmoja anaitwaJimi alimwuliza mtu mmoja anayekana kuwa kuna Mungu endapo alipata kujaribu sana, hata kwa dakika chache tu, kupigana na wazo lisemalo kwamba huenda Mungu yuko.

“Sawa kabisa!” mkana Mungu yule akajibu, akimwacha Jimi na mshangao. “Miaka mingi iliyopita, mimi nilikuwa karibu sana nigeuke na kuwa mtu anayemwamini Mungu. Nilipokiangalia kile kiumbe kidogo sana lakini kikamilifu katika kitanda chake kidogo, nilipochungulia na kuviona vidole vile vidogo fahamu za kwanza za kutambua, nilipita katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo katika hiyo mimi nilikuwa karibu kabisa niache kuwa mkana Mungu. Kule kumwangalia mtoto yule kulikuwa kumenishawishi karibu kabisa kuwa hapana budi Mungu alikuwa yuko.”

View attachment 1280854

Huyo mtoto akikuwa naye anaweza kuwa mbishi akipinga uwepo wa Mungu.🤣🤣
kristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi

Acha Uongo.
 
Nithibitishe nini tena?

Siku moja jamaa mmoja anaitwaJimi alimwuliza mtu mmoja anayekana kuwa kuna Mungu endapo alipata kujaribu sana, hata kwa dakika chache tu, kupigana na wazo lisemalo kwamba huenda Mungu yuko.

“Sawa kabisa!” mkana Mungu yule akajibu, akimwacha Jimi na mshangao. “Miaka mingi iliyopita, mimi nilikuwa karibu sana nigeuke na kuwa mtu anayemwamini Mungu. Nilipokiangalia kile kiumbe kidogo sana lakini kikamilifu katika kitanda chake kidogo, nilipochungulia na kuviona vidole vile vidogo fahamu za kwanza za kutambua, nilipita katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo katika hiyo mimi nilikuwa karibu kabisa niache kuwa mkana Mungu. Kule kumwangalia mtoto yule kulikuwa kumenishawishi karibu kabisa kuwa hapana budi Mungu alikuwa yuko.”

View attachment 1280854
Thibitisha Mungu yupo, na kwamba hizo habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.
 
Alaa, kumbe Ukristo ni dini "kikongwe" (kibabu)!![emoji1787][emoji1787].

Uislamu ni dini ya kisasa (modern)
1. Maana ya neno "lslam"
Neno 'Islam' Asili yake ni lugha ya 'kiarabu' lenye maana ya 'utii' au 'amani'.

2. Mwanzo wa Dini ya Kiislamu
Neno "Islam" ni tofauti na "Dini ya Kiislamu". Hii ni kwa sababu neno "Islam" lilitumika na waarabu hata kabla ya kuanza kwa dini ya kiislamu. Kwa hivyo "Dini ya kiislamu", maana yake ni "kujisalimisha chini ya amri za Allah" au "Amani chini ya sheria za Allah".

i. Muhammad aliambiwa na Allah asema: -
Quran 39: 12 Suratul Zumar (Makundi / Vikosi)
"Na pia nimeamrishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha (kwa mwenyezi Mungu)"

Quran 6: 14 Suratul Al- An'am (Wanyama)
Sema "je nifanye mola (wangu) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, (Ambaye ndiye) muumba wa mbingu na ardhi" naye hulisha wala halishwi" sema hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu na (nikaambiwa). usiwe miongoni mwa wanaomshirikisha (Mwenyezi Mungu).

Katika ufafanuzi wa aya ya 19-20, katika Suratul Yusuf 12:20 kuna maneno haya--
Unaona kuuzana kulikuwako zaidi ya miaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo nabii Muhammad. Kisha wakausingizia uislamu kuwa ndio uliokuja na kuuza watu.

Kadiri ya aya hizi zote tunaona ya kuwa dini ya kiislamu ilianzishwa rasmi hapa duniani Ramadhan siku ya Jumatatu mwezi 17 sawasawa na Tarehe 27 December mwaka 610 Baada ya Kristo (B.K), na mtu aitwae Muhammad Bin Abdalah Bin Abd-Muttalib Bin Hashim Bin Abd Manafu Bin Kusay. Mama yake aliitwa Amina Bint Wahab.
 
Thibitisha Mungu yupo, na kwamba hizo habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.
Kila Kitu Kilichoumbwa Kina Muumbaji Wake

Lakini ushahidi wa kuwako kwake Mungu haufungamani tu na ubunifu wa miili yetu; pia umetandaa huko mbinguni. Acha taa za mjini, angalia juu katika mbingu ya usiku. Wingu lile jeupe kama maziwa lenye nyota, tunaloliita Mkanda wa Nuru (Milky Way) ambalo kwa kweli ni kundi la mabilioni ya majua (galaxy) yanayotoa mwanga mkali wa moto sawa na ule wa jua letu ambao unaweza kuonekana hapa duniani kwa kupitia katika darubini kubwa zilizopo hapa duniani kama ile darubini iitwayo “Hubble Telescope” iliyo katika anga za juu.

Si ajabu, basi, kwamba mtunga Zaburi alihitimisha kwa kusema kwamba nyota zinamtangaza Muumbaji Mtukufu:
“Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu, anga ladhihirisha kazi ya mikono yake” (Zaburi 19:1-3).

Je, hivi sisi twaweza kutoa hitimisho gani la busara kwa kuangalia mpangilio huo unaotatanisha sana na ukubwa wa malimwengu yote?

“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwanzo 1:1).

“Yeye [Mungu] alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote hudumu mahali pale kwa uwezo wake” (Wakolosai 1:17).

images%20(6).jpeg
images%20(5).jpeg
images.jpeg
 
1. Maana ya neno "lslam"
Neno 'Islam' Asili yake ni lugha ya 'kiarabu' lenye maana ya 'utii' au 'amani'.

2. Mwanzo wa Dini ya Kiislamu
Neno "Islam" ni tofauti na "Dini ya Kiislamu". Hii ni kwa sababu neno "Islam" lilitumika na waarabu hata kabla ya kuanza kwa dini ya kiislamu. Kwa hivyo "Dini ya kiislamu", maana yake ni "kujisalimisha chini ya amri za Allah" au "Amani chini ya sheria za Allah".

i. Muhammad aliambiwa na Allah asema: -
Quran 39: 12 Suratul Zumar (Makundi / Vikosi)
"Na pia nimeamrishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha (kwa mwenyezi Mungu)"

Quran 6: 14 Suratul Al- An'am (Wanyama)
Sema "je nifanye mola (wangu) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, (Ambaye ndiye) muumba wa mbingu na ardhi" naye hulisha wala halishwi" sema hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu na (nikaambiwa). usiwe miongoni mwa wanaomshirikisha (Mwenyezi Mungu).

Katika ufafanuzi wa aya ya 19-20, katika Suratul Yusuf 12:20 kuna maneno haya--
Unaona kuuzana kulikuwako zaidi ya miaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo nabii Muhammad. Kisha wakausingizia uislamu kuwa ndio uliokuja na kuuza watu.

Kadiri ya aya hizi zote tunaona ya kuwa dini ya kiislamu ilianzishwa rasmi hapa duniani Ramadhan siku ya Jumatatu mwezi 17 sawasawa na Tarehe 27 December mwaka 610 Baada ya Kristo (B.K), na mtu aitwae Muhammad Bin Abdalah Bin Abd-Muttalib Bin Hashim Bin Abd Manafu Bin Kusay. Mama yake aliitwa Amina Bint Wahab.

Sasa maelezo hayo yako yanapinga au yanakubali kwamba ukristo ni dini kongwe (kibabu) na Uislamu ni dini ya kisasa (modern religion)??!!🤣
 
Back
Top Bottom