Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
Miaka ya Nyuma Mabaharia waasi maarufu walioizamisha meli ya Kiingereza iliyoitwa Bounty waliishia kufanya makazi yao wakiwa pamoja na wanawake, wenyeji wa eneo lile katika kisiwa cha Pitcairn katika Bahari ya Pasifiki ya Kusini.
Kundi hili lilikuwa na mabaharia tisa wa Kiingereza, wanaume wa Kitahiti sita, wanawake wa Kitahiti kumi, na msichana wa miaka kumi na mitano.
Mmojawapo wa mabaharia wale alivumbua namna ya kutonyesha [kugeuza kuwa mvuke] alkoholi, na baada ya muda mfupi ulevi ukaliharibu koloni lile lililokuwa katika kisiwa kile.
Ugomvi kati ya wanaume na wanawake ukageuka na kuwa wa kutumia nguvu.
Baada ya kupita muda fulani mmoja tu kati ya wanaume wale wa kwanza waliofika mle kisiwani ndiye alibaki kuwa hai.
Moja ya hawa watu aliyebaki alikuwa anaitwa Alexander Smith, alikuwa ameigundua Biblia katika mojawapo la makasha yaliyochukuliwa kutoka katika ile meli.
Alianza kuisoma na kuwafundisha wengine juu ya kile ilichosema. Alipofanya hivyo maisha yake yeye mwenyewe yakabadilika na hatimaye maisha ya wote waliokuwa katika kisiwa kile.
Wakazi wa kisiwa kile walikuwa wametengwa na ulimwengu wa nje mpaka ilipowasili meli ya Kimarekani iliyoitwa Topaz katika mwaka wa 1808.
Wafanyakazi katika meli hiyo wakakikuta kisiwa kile kikiwa na jumuia inayokua na kusitawi, bila ya kuwa na pombe kali (wiski), gereza, wala uhalifu.
Biblia ilikuwa imekigeuza kisiwa kile kutoka jehanamu ya duniani kwenda katika kielelezo cha vile Mungu atakavyo ulimwengu huu uwe.
Na mpaka leo hii kinaendelea kuwa katika hali hiyo.
Je, hivi Mungu bado anaendelea kusema na watu kupitia katika kurasa hizo za Biblia?
Bila shaka anafanya hivyo.