Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HISTORIA YA ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE 1954
Kuna picha ya Mtaa wa Jaribu Magomeni iliyowekewa maelezo kuwa ni Mtaa wa Congo mwaka wa 1920.
Picha iko hapo chini.
Huu si Mtaa wa Congo wala si mwaka wa 1920.
Huu ni Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa miaka ya katikati 1950s na hapo ni nyumbani kwa Ali Msham aliyehamia Dar es Salaam kutokea Kilwa, aliyefungua tawi la TANU nyumbani kwake mwaka wa 1954 kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ali Msham alikuwa fundi seremala na akifanya shughuli zake Mtaa wa Kariakoo na Kibambawe.
Mimi naishi jirani na hii nyumba.
Watoto wa marehemu Ali Msham ni jirani zangu hapa Magomeni Mapipa na walisikia siku moja nafanya kipindi Radio Kheri kuhusu TANU ndipo waliponiletea picha na wakanieleza historia ya baba yao Ali Msham na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Baba yao marehemu Ali Msham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na tawi hili lilikuwa na wanachama wengi hasa wanawake.
Mwalimu Nyerere alipohamia Magomeni mwaka wa 1955 Ali Msham alimfungulia Mama Maria kijiduka kidogo hapo kwake cha kuuza mafuta ya taa.
Mama Maria alikuwa pia akiwa dukani kwake akifuma sweta.
Siku moja Ali Msham alikwenda ofisini kwa Mwalimu Nyerere pale New Street akakuta samani alizokuwa akitumia Mwalimu ni duni sana.
Ali Msham alisikitishwa na hali ile.
Ali Msham alitengeneza samani mpya kiwandani kwake na akanunua na saa ya ukutani kwa ajili ya ofisi ya Rais wa TANU na akamuomba Mwalimu Nyerere wamkabidhi samani zile kwenye tawi lake la TANU Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu katika sherehe maalum.
Angalia picha hapo chini Ali Msham ni wa kwanza kulia na Mwalimu Nyerere amekaa kwenye meza.
Picha ya sherehe hii na nyingine za harakati za baba yao katika TANU watoto wa Ali Msham wamezihifadhi kuanzia mwaka wa 1955 hadi leo.
Nilichofanya mimi niliaandika historia ya Ali Msham na nikaiweka katika blog yangu mohamedsaidsalum.blogspot.com pamoja na picha zile.