Historia ya Ali Msham na Julius Nyerere 1954

Historia ya Ali Msham na Julius Nyerere 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HISTORIA YA ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE 1954

Kuna picha ya Mtaa wa Jaribu Magomeni iliyowekewa maelezo kuwa ni Mtaa wa Congo mwaka wa 1920.

Picha iko hapo chini.

Huu si Mtaa wa Congo wala si mwaka wa 1920.

Huu ni Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa miaka ya katikati 1950s na hapo ni nyumbani kwa Ali Msham aliyehamia Dar es Salaam kutokea Kilwa, aliyefungua tawi la TANU nyumbani kwake mwaka wa 1954 kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ali Msham alikuwa fundi seremala na akifanya shughuli zake Mtaa wa Kariakoo na Kibambawe.

Mimi naishi jirani na hii nyumba.

Watoto wa marehemu Ali Msham ni jirani zangu hapa Magomeni Mapipa na walisikia siku moja nafanya kipindi Radio Kheri kuhusu TANU ndipo waliponiletea picha na wakanieleza historia ya baba yao Ali Msham na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baba yao marehemu Ali Msham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na tawi hili lilikuwa na wanachama wengi hasa wanawake.

Mwalimu Nyerere alipohamia Magomeni mwaka wa 1955 Ali Msham alimfungulia Mama Maria kijiduka kidogo hapo kwake cha kuuza mafuta ya taa.

Mama Maria alikuwa pia akiwa dukani kwake akifuma sweta.

Siku moja Ali Msham alikwenda ofisini kwa Mwalimu Nyerere pale New Street akakuta samani alizokuwa akitumia Mwalimu ni duni sana.

Ali Msham alisikitishwa na hali ile.

Ali Msham alitengeneza samani mpya kiwandani kwake na akanunua na saa ya ukutani kwa ajili ya ofisi ya Rais wa TANU na akamuomba Mwalimu Nyerere wamkabidhi samani zile kwenye tawi lake la TANU Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu katika sherehe maalum.

Angalia picha hapo chini Ali Msham ni wa kwanza kulia na Mwalimu Nyerere amekaa kwenye meza.

Picha ya sherehe hii na nyingine za harakati za baba yao katika TANU watoto wa Ali Msham wamezihifadhi kuanzia mwaka wa 1955 hadi leo.

Nilichofanya mimi niliaandika historia ya Ali Msham na nikaiweka katika blog yangu mohamedsaidsalum.blogspot.com pamoja na picha zile.
 
HISTORIA YA ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE 1954

Kuna picha ya Mtaa wa Jaribu Magomeni iliyowekewa maelezo kuwa ni Mtaa wa Congo mwaka wa 1920.

Picha iko hapi chini.

Huu si Mtaa wa Congo wala si mwaka wa 1920.

Huu ni Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa miaka ya katikati 1950s na hapo ni nyumbani kwa Ali Msham aliyehamia Dar es Salaam kutokea Kilwa, aliyefungua tawi la TANU nyumbani kwake mwaka wa 1954 kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ali Msham alikuwa fundi seremala na akifanya shughuli zake Mtaa wa Kariakoo na Kibambawe.

Mimi naishi jirani na hii nyumba.

Watoto wa marehemu Ali Msham ni jirani zangu hapa Magomeni Mapipa na walisikia siku moja nafanya kipindi Radio Kheri kuhusu TANU ndipo waliponiletea picha na wakanieleza historia ya baba yao Ali Msham na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baba yao marehemu Ali Msham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na tawi hili lilikuwa na wanachama wengi hasa wanawake.

Mwalimu Nyerere alipohamia Magomeni mwaka wa 1955 Ali Msham alimfungulia Mama Mariam kijiduka kidogo hapo kwake cha kuuza mafuta ya taa.

Mama Maria alikuwa pia akiwa dukani kwake akifuma sweta.

Siku moja Ali Msham alikwenda ofisini kwa Mwalimu Nyerere pale New Street akakuta samani alizokuwa akitumia Mwalimu ni duni sana.

Ali Msham alisikitishwa na hali ile.

Ali Msham alitengeneza samani mpya kiwandani kwake na akanunua na saa ya ukutani kwa ajili ya ofisi ya Rais wa TANU na akamuomba Mwalimu Nyerere wamkabidhi samani zile kwenye tawi lake la TANU Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu katika sherehe maalum.

Angalia picha hapo chini Ali Msham ni wa kwanza kulia na Mwalimu Nyerere amekaa kwenye meza.

Picha ya sherehe hii na nyingine za harakati za baba yao katika TANU watoto wa Ali Msham wamezihifadhi kuanzia mwaka wa 1955 hadi leo.

Nilichofanya mimi niliaandika historia ya Ali Msham na nikaiweka katika blog yangu mohamedsaidsalum.blogspot.com pamoja na picha zile.
Angalia picha za Tawi la TANU la Ali Msham Mtaa wa Jaribu katika miaka ya 1950.
Screenshot_20200608-073121.jpg
IMG-20200531-WA0084.jpg
IMG-20200328-WA0219.jpg
 
Safi

Historia ya nchi hii ingefaa iandikwe upya na Kila aliyehusika katika kupigania uhuru apate nafasi yake kwenye historia.

Laana nyingine Ni za kujitakia. Haiwezekani wengi wa watu waliopigania uhuru wasienziwe na Bado tukaendelea kuwa salama.

Waenziwe kwa kutajwa..kujengewa monument, majina yao kupewa mashule, mahospital, mabarabara,mitaa,majengo ya chama Cha mapinduzi na kadhalika.

A society that forget to honor its own heroes is doomed to fail.
 
Mkuu nchi hii historia imevulugwa mnoo cjui ilivulugwa kwa manufaa gn.. daaah
 
Hivi ukitangaza leo kila aliyefanya harakati za kupigania au kuupinga ukoloni warithi wao wajitokeze unadhani patatosha?
 
Hivi ukitangaza leo kila aliyefanya harakati za kupigania au kuupinga ukoloni warithi wao wajitokeze unadhani patatosha?
Mrithi wa Nini? Yule yule aliyepigania Uhuru ndio aenziwe kwa kumbukumbu flani......
 
Mrithi wa Nini? Yule yule aliyepigania Uhuru ndio aenziwe kwa kumbukumbu flani......
rr3,
Muhimu si kuenziwa kwa yeyote awaye yule tatizo ambalo mimi nililigundua na jambo la kushangaza ni kuwa nimekuta Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wanasomesha historia ya Tanzania ambayo imejaa upungufu mkubwa sana.

Na nilikuwa nikwaeleza walimu wangu kuwa mathalan haiwezekani kusomesha historia ya TANU ukaanza na Julius Nyerere.

Kilichokuwa kikinisikitisha sana ni pale hata nilipojaribu mathalan kueleza niliyoyajua kuhusu TANU nikageuzwa kichekesho kwani hakuna aliyataka kuamini kuwa babu yangu ni mmoja wa waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru.

Ilikuwa ile, ''Wewe kwani babu yako nani mbona hatujamsikia?''
Ndipo nilipoamua kuandika kitabu cha Abdul Sykes.

Yaliyotokea baada ya kitabu kuchapwa London mwaka wa 1998 hii leo yamegeuka kuwa historia nyingine.
 
Mrithi wa Nini? Yule yule aliyepigania Uhuru ndio aenziwe kwa kumbukumbu flani......
Nimemaanisha wengi wameshatangulia mbele ya haki, hivyo huenda watajitokeza Watoto/Warithi wao....na iwapo watakuwa na vielelezo vya kumbukumbu.
 
Nimemaanisha wengi wameshatangulia mbele ya haki, hivyo huenda watajitokeza Watoto/Warithi wao....na iwapo watakuwa na vielelezo vya kumbukumbu.
Ok..... Ila muhimu hata Kama Kila mkoa ukiweka monument ya watu kumi (10) nadhani kwa makadirio ya watu 300 tutakuwa tumewapa heshima mashujaa wetu......
 
Hizi historia tutaenda nazo tu hivyo hivyo, tutamsikila huyu na yule mwishowe tutachanganya na zetu.
May...

Mimi nisingefanya utafiti wa maisha ya Ali Msham kama kungekuwa hakuna ushahidi.

Watoto wake walinipa picha ndiyo hizi nimeziweka mtandaoni Ali Msham akiwa kwenye tawi la TANU nyumbani kwake na Sheikh Suleiman Takadir, Zuberi Mtemvu, John Rupia, Bantu Group nk.
 
Mkuu nchi hii historia imevulugwa mnoo cjui ilivulugwa kwa manufaa gn.. daaah
Weng waluopigania uhuru ni waislam

WAKRISTO na wapagani hawafiki ht 2%, bahati mbaya, baada ya uhuru, wale waoga na wachoyo kutoa Mali zao kwa ajili ya maslahi ya taifa ndo wakapendelewa na kukabidhiwa keki ya taifa, mwisho ndo wakawa wanabadilisha kila kitu ili kuficha aibu yao na dhulma walizofanya kwa waislam

REJEA mapendekezo ya mh mzandeke wakati yupo UK anasoma,
Alimwambia mwalim ahakikishe baada ya uhuru jamii inakuwa na haqq sawa, waislam na wao wawe na mashule sambamba na vyuo

Lkn Hali kufanyia kazi Hilo, badala yake hata umoja wao wa eac ulivunjwa n kuunda bakwata

Ila kwa upande flani, waislam walizidi uzembe, kivip walikubali kuwapa nafasi wakristo, wakati wao ndo waliojitoa mganga kupigania taifa hili,

Hivi walisoma kitab gani kinachoonesha wakristo wamewahi kuwapendelea waislam?
Haikuwa na tija kwao kulalamika kwani nafasi walitoa wenyewe

Sent by alshabaab blog [emoji12][emoji12][emoji12]
 
Hizi historia tutaenda nazo tu hivyo hivyo, tutamsikila huyu na yule mwishowe tutachanganya na zetu.

African history is oral history - mambo ya mdomo. Babu zetu hawakujua kusoma na kuandika masuala ya maisha yao.

Ndio maana na uongo wenye agenda za kisiasa na kijamii unaongezwa.

Hizi furniture sio ihsani.

TANU haikuwa na hela kununua furniture za dukani, ndo ikaweka service order kwa huyu Mzee mwenye mgongano wa kimaslahi na chama pamoja na insider information za mahitaji ya furniture chamani. Furniture zikachongwa, akalipwa.

Na wengine wakala 10% zao kwenye order mumo mumo, magumashi hayajaanza na kina Abdulrasul ( Mweka Hazina) wala Aikaeli (Mwenyekiti). Kuna Mkuu alikalia mafaili ya ankara za mapato na matumizi ya chama kuanzia 1954 mpaka 1990 alipong'atuka, MIAKA 36.
 
African history is oral history - mambo ya mdomo. Babu zetu hawakujua kusoma na kuandika masuala ya maisha yao.

Ndio maana na uongo wenye agenda za kisiasa na kijamii unaongezwa.

Hizi furniture sio ihsani.

TANU haikuwa na hela kununua furniture za dukani, ndo ikaweka service order kwa huyu Mzee mwenye mgongano wa kimaslahi na insider information za mahitaji ya furniture chamani. Furniture zikachongwa, akalipwa.

Na wengine wakala 10% zao kwenye order mumo mumo, upigaji haujaanza na kina Aziz wala Aikaeli. Kuna mwenyekiti alikalia mafaili ya ankara za mapato na matumizi ya chama kuanzia 1954 mpaka 1990, MIAKA 36.
Shukran kwa taarifa Kaka. Uzuri ni kwamba nimeshamjua vizuri Mzee Said na nimeshajua namna ya kwenda na maandiko yake.

Anapingana na historia ya TANU iliyoandikwa kivukoni na anataka tukubaliane na kila anachoelezea yeye...kuna mengi sana ukisoma Mtu ukitumia akili unashindwa kabisa kuunganisha dots.
 
Wakina makamba wamepewa mitaa wakati hawajafanya chochote cha maana halafu sio kweli kwamba wakiristo hawakufanya chochote kuna kina Rupia, Lupemba ambaye sijawahi kusikia hata siku moja akitajwa kina Barongo lakini inabidi uelewe harakati za uhuru kuanzia Taa na baadae Tanu zilianzia wapi?
Harakati hizi zilianzia pwani au Dar es salaam( Mzizima) ambako asilimia kubwa wakazi wake ni waislamu sema waislamu wa wakati ule walikuwa ni waislamu haswa kwani waliweza kukaa na wakiristo bila kujiona wao bora ndio maana wakamchagua Mwalimi kuongoza na kumfanyia dua awe kiongozi pia waliweka maslahi ya taifa mbele nafikiri hii ndio ilileta msukumo kwa Nyerere kutaifisha shule ambazo nyingi zilimilikiwa na wamisionari ili waislamu wasihofu kupeleka watoto wao shuleni kuwa watabadirishwa dini
 
Shukran kwa taarifa Kaka. Uzuri ni kwamba nimeshamjua vizuri Mzee Said na nimeshajua namna ya kwenda na maandiko yake.

Anapingana na historia ya TANU iliyoandikwa kivukoni na anataka tukubaliane na kila anachoelezea yeye...kuna mengi sana ukisoma Mtu ukitumia akili unashindwa kabisa kuunganisha dots.
May Day,
Mimi inanitosha ukisoma si lazima uniamini.
 
Back
Top Bottom