tanzania bahima wako karagwe ,ngara,kigoma na bukoba
mimi nmezaliwa na kukulia Karagwe mpakani mwa Tanzania na uganda (near
Murongo boarder) kandokando ya mto Kagera. hili ni eneo ambalo linakaliwa sana na mchanganyiko wa makabila ya watu kutoka nchi za maziwa makuu yaani
Batutsi, bahutu from rwanda, barundi from burundi, banyankole, baganda and bachiga, barela from uganda, bakongo from DRC,etc.
Padre Privatus Karugendo aliwahi kuelezea short history ya
BAHIMA na chimbuko lao kwenye moja ya makala zake kwenye gazeti la
Raia Mwema. Kihistoria kuna tofauti kati ya hao BAHIMA na BATUTSI ukisoma kitabu cha
THE SHORT HISTORY OF TANGANYIKA ; Bahima( pastoralists) waliingia eneo la maziwa makuu na kujipenyeza mpaka kaskazini magharibi mwa tanzania miaka mingi hta kabla ya ujio wa wakoloni. Kuna nadharia kwamba ukitrace chimbuko la BAHIMA utakuta asilimia kubwa ya wakazi wa wilaya za KARAGWE, KYERWA NA NGARA ni jamii ya watu hao ingawa bahima wenyewe ni pastoralists in nature wakati wakazi wa wilaya tajwa hapo juu ni wakulima na wafugaji, hapa tunapata watu wengine amabao ni BAHIRU ambao kiasili ni Cultivators , wenyewe hawa ndio wabantu wa asili wa eneo hilo (Rejea historia ya BUNYORO KITARA uone '
batembuzi
', 'bahima', 'bahiru', 'bachwezi', 'batwarwa' na 'batwazi'). Nadharia nyingine inaelezea kwamba asili ya wakazi wa eneo la maziwa makuu hususani Ankole,Buganda,Toro, bunyoro, karagwe na Buhaya(bukoba) ni BUNYORO KITARA nchini Uganda (Rejea kitabu cha
Prof, Israel Katoke,
THE MAKING OF KARAGWE KINGDOM). Nijuavyo mm, wakazi wengi wa Karagwe na Kyerwa hawajui kutofautisha kati ya Bahima na Batutsi... wanawaita wote kwa pamoja '
Bahima' (
abhahima) means, the pastolalists from RWANDA with tutsi bood in nature. Niko nafanya utafiti, hivi soon ntawafahamisha hii Bahima empire ni nini, chimbuko lao ni lipi? Je, bahima ndio batutsi? vipi kuhusu kuwepo kwa sehemu inaitwa
Mpororo kingdom ambayo ndio inasadikiwa kuwa chimbuko la Bahima empire? vipi kuhusu mambo ya
Museveni na
Kagame kuhusu mpango wa kuendeleza Bahima empire?....n.k. ILa ukitaka kufahamu vizuri hii dhana ya Bahima empire kwanza ni vizuri ukajua kuhusu:
-The Kingdom of Bunyoro Kitara.
-Karagwe kingdom.
-The kingdoms of Ankole, toro and Buganda.
-The kingdoms of Rwanda-Urundi.
NO RESEARCH, NO RIGHT TO SPEAK.