Historia ya biashara ya Benki

Historia ya biashara ya Benki

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Biashara ya Benki ilianza mwaka 2000BC. Siria, Misri mpaka India. Hii ilikuwa enzi ya utawala wa Roma na biashara hii ilishamiri katika iliyokuwa himaya ya Alexandra the Great. Wafanyabiashara walikopeshana nafaka kwa riba hasa wale waliosafirisha nafaka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Biashara hii ilishamiri katika miji mikubwa ya Ulaya. Italia, Ufaransa, Ujerumani na Urusi. Mapinduzi makubwa katika biashara ya benki yalikuja baada ya Holicust. Wayahudi waliokimbia Ujerumani kuekekea Marekani walianzisha biashara ya kukopesha pesa kwa riba katika miji waliyofikia.

Wayahudi hawa hawakukopesha tu pesa bali walihifadhi pesa za matajiri na vitu vyao vya thamani kwa riba.
 
Pia zamani dhahabu ilitumika kama pesa au namna ya kuhifadhi utajiri. sasa kuna watu waliona wenzao huvamiwa na kuporwa sana dhahabu. Wakatengeneza mavault ya kuhifadhia dhahabu na ili akutunzie dhahabu basi ulitakiwa kumlipa ada fulani.

wakakaa wakaona mbona watu hawaji kutoa dhahabu zao!!? vipi tukizikopesha kwa wafanyabishara wakanunue mizigo na wakipata faida waturudishie? wakaanza kukopesha watu na wanapata riba.

Wakaona faida ya riba ni kubwa kuliko ada ya kutunzia pesa. wakawaambia watu kwamba mtakuwa mnatunza dhahabu bure.
wengine wajanja wakaona mbona hawa watunza dhahabu wanatajirika sana?! wakagundua mchezo. wakasema tukileta dhahabu na sisi tunataka sehemu ya riba, hapo ndiyo zikaanza hizi investment bank.

Ukitunza dhahabu zako ulikuwa unaandikiwa risiti ambayo inaonyesha kiasi cha dhahabu uliyotunza. Sasa badala ya kila ukitaka kununua kitu ukatoe dhahabu wakakubaliana watakuwa wanatumia ile risiti na huo ndiyo mwanzo wa kutumia pesa za karatasi. kwahiyo kulikuwa na pesa mbalimbali kutokana na kuwa na watunza dhahabu wengi.

Hawa watunza dhahabu wakaanza mchezo mchafu. wakawa wanatengeneza risiti nyingi kuliko dhahabu iliyopo kwenye mavault. watu wakaanza kuguna, "mmh! hivi kweli kuna dhahabu ya kutosha risiti zote hizi? twende tukacheki". kwenda kucheki wakakuta kuna uhuni mkubwa kwasababu ilitakiwa wakipeleka risiti watoe dhahabu yao sasa risiti ni nyingi kuliko dhahabu!!? huo ndiyo ukawa mwanzo wa benki kufilisika na hata leo hii benki haiwezi kubali watu wote kwa pamoja wakatoe pesa lazima itaanguka sababu pesa walizonazo ni chache kuliko wateja wakijumlisha masalio yao.

hapa wakapitisha sheria kwamba risiti/pesa lazima iwe sawa na dhahabu kwa uwiano wa 1:1 baadaye ratio ikaongezeka hasa wakati wazungu wanafanya umerchants ambapo mahitaji ya pesa yalikuwa makubwa sana na hata leo pesa haiko backed na dhahabu tena.

Kwahiyo zamani benki ndiyo zilikuwa na jukumu la kuchapisha fedha lakini sasa serikali ndiyo zimechukua jukumu hilo.
Duh! nimetoka povu!!🙂 cc Malcom Lumumba , zitto junior Wick
 
Biashara ya Benki ilianza mwaka 2000BC. Siria, Misri mpaka India. Hii ilikuwa enzi ya utawala wa Roma na biashara hii ilishamiri katika iliyokuwa himaya ya Alexandra the Great. Wafanyabiashara walikopeshana nafaka kwa riba hasa wale waliosafirisha nafaka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Biashara hii ilishamiri katika miji mikubwa ya Ulaya. Italia, Ufaransa, Ujerumani na Urusi. Mapinduzi makubwa katika biashara ya benki yalikuja baada ya Holicust. Wayahudi waliokimbia Ujerumani kuekekea Marekani walianzisha biashara ya kukopesha pesa kwa riba katika miji waliyofikia.

Wayahudi hawa hawakukopesha tu pesa bali walihifadhi pesa za matajiri na vitu vyao vya thamani kwa riba.
Na pia wayahudi waliinuka sana kwenye hii biashara kwa sababu wakristo muda huo walikuwa wanakataza kukopeshana kwa riba. Wayahudi wao haina shida so walibaki ndiyo mapusher peke yao kitaa🙂
Najiuliza leo hii uislamu ungekuwa unaruhusu Riba na jinsi nchi za kiislamu zilivyo na pesa nyingi za mafuta ingekuwaje!?. Hizi dini sometimes nazo!?
 
Hivi ni mimi sijaelewa 2000BC ina maana gani au?!
 
Sky Eclat na Red Giant mnamjua/mmewahi msoma mtu anaitwa John Pierpont Morgan?

1535628224798.png
 
Gusa hapa uone linavyomiliki dunia Vatican Inamiliki Dunia - JamiiForums

Back
Top Bottom