Ndugu zangu, siku hizi tunasoma uzi nyingi kuhusu forex, bitcoins, na kadhalika. Naona watu wengi hawaelewi vizuri, wengine wanadanganywa, na wengine wanakataa kabisa hata kujaribu kuelewa kwa kuhofia kwamba ni kitu kigeni sana.
Nimeamua basi nijaribu kueleza eleza zaidi kuhusu topics hizi. Zote ni njia ya kuwekeza na kupata au kupoteza pesa kadhiri ya unapooperate mwenyewe. Pia ni muundo mpya wa biashara na wa kuelewa maisha wa jamii.
Kwanza forex. Nampongeza Bwana Ontario na uzi zake za Forex. Nimemfuatilia sana na sijawahi kuona kwamba anasema uwongo hata mara moja. Anawashauri wengi na wanaolalamika ni wale hawaelewi bado au wanakuwa na tama ya kutajirika haraka. Forex njia nzuri ya kuwekeza pesa, ukiwa unafuata kanuni muhimu kama kuwekeza kwenye plattform halali, kujielimisha kwa kusoma na kuoperate, kufuata akili na si Tamaa ya moyo, na kadhalika.
Bitcoin. Kwa kweli, hapa tunaingia kweye muundo mwingine kabisa. Cryptoeconomy au cryptocoins na hata cryptotokens. Cryptoeconomy imeanza na blockchain, teknolojia mpya ya kidijital 2008. Ndiyo wameitumia kwa ajili ya kuunda Bitcoin, kama pesa ya mtandao. Kwa muda mdefu wengi wameiona kwamba ni mchezo tu, mpaka ghafla wafanyabiashara na matajiri wamegundua wanaweza kuitumia kwa uwekezaji na kwa kutumia kwa jailli ya kununua na kuuza, kama system ya transactions, nk. Ndiyo maana tumefika leo Bitcoin ndiye sarafu ya kidijitali yenye uwezo kubwa (asilimia 48% ya sarafu ya kidijital ni Bitcoin). Zipo zaidi ya sarafu 1300 ya kijidijital, Sarafu ya pili inaitwa Ethereum. Ethereum ni sarafu inaitumika sana kama sarafu ya kidijitali kama Bitcoin na kama sarafu ya kidijitali makampuni ya Blockchain na fintech wanaitumia wakati wanatumia teknolojia ya Blockchain. Hata hivi leo mtu yeyote anaweza pia kununua kuuza na kuwekeza pia kwa Ethereum na cryptocoins tofauti tofauti. Thamani zao unaweza kuziona
www.coinmarketcap.com
Nimesoma hapa Jamiiforums watu wengi walipoteza pesa kwa kuwekeza kwenye kampuni za wajanja wanaoahidi faida kubwa na ya baraka. Kwa Kweli hatuhitaji kampuni kwa kuwekeza, tunachohitaji ni kuelewa tunachofanya na wapi kuzifungua crypto wallets na kutumia crypto plattform gani bila kuwapa pesa yetu kwa wajanja. Tunachohitaji ni akili na kusoma na kuelewa biashara hii. Kwanza Kabisa tusiweke pesa yetu ya kuendesha maisha ya kila siks kwenye biashara hii. Tukiweka nyumba au gari au ada ya shule ya watoto, ni kosa kubwa sana. Tumia pesa unaoweza kuifanyia Kazi, kwa kutumaini utaipata faida, lakini kwa kuelewa daima hakuna uhakika asilimia mia kwenye uwekezaji wowote. La pili kwa kununua au kuwekeza kweye sarafu za kidjitali njia za kawaida ni rahisi.
Hatua ya kwanza ni kupata crypto coin electronic wallet kama BTC wallet au ETH wallet. Hizo ni private wallets. Hizo wallets zina password refu sana (encrypted key) na ni ya pekee. Ukipoteza umepoteza kila kitu maana hakuna mwingine anayeijua zaidi ya wewe. Andika popote, na usimpe mtu yeyote kwa sababu yeyote. Uhifadhi. La pili ujiunge na cryptocoin exchange yeyote. Zipo soko mbalimbali na inabidi ufanye Kazi kwanza ya kuelewa ipi inakufaa sababu nyingine ndiyo wanakuwa na experience Africa ya Mashariki na wanakuwa na fees tofauti, na muundo tofauti ya kulipa au kulipwa na credit card, au debit card, au Mpesa au nini..
Exchange places watakupa public wallet. Hapa unaweza kufanya transactions, kununua na kuuza, na kadhalika. Inashauriwa sana cryptocoins zako zihifadhiwe ndani ya private wallet, na uziweke kwenye public wallet yako unachohitaji kwa ajili ya transaction tu, kwa usalama zaidi. Daima bitcoin au crypto coin zako utazihifadhi Katika private wallet yako.
Hata hivi uchumi wa crypto (cryptoeconomy) inakuwa na msingi moja unaoitwa Blockchain. Ukitaka kujua zaidi kuhusu Blockchain na cryptocoins, soma kwenye mtandao. Mimi natumia sana
www.blockchaincompany.info kwa habari. Kwanza sababu ya Maelezo mazuri, pia wanarushia Bloomberg Live, na ukiwa member wanakupa Tokens za kampuni bure, na hizo tokens zitakuwa pia kwenye token exchange (cryptotoken) karibuni na utakuwa na faidha kwa baadaye. Pia tovuti ya
www.coinmarketcap.com kwa kuangalia soko la kila siku. Tujielimishe. Kwa mfano, tupo wengi tunalalamika benki zetu hawataki kutupatia mikopo yenye masharti nafuu (ingawa ni kweli wengi wanakuja kuomba mikopo benki zetu bila hata business plan!!). Kwa uchumi wa blockchain utaweza kuweka pesa kwenye start up yako kwa kutumia ICOs (Initial Coin Offering) haraka ukiwa umeitayarisha vizuri, bila kuwategemea mabenki…. Soma utaelewa, jifunze ili milango zifunguliwe, jitayarishe kwa mapinduzi wa blockchain katika uchumi na jamii... uwe tayari kwa Blockchain Africa, na cryptocoins za Africa....