Bitcoin is a digital coin. Its value is more than any currency. Its value today: 1 btc = 13,870 usd =31,000,000 TZS . Hiyo ni standard exchange rate. Ukitaka kuinunua utanunua kwa about 40 milion TZS.
Hii coin ilianza mwaka 2009 wakati huo 1 btc iliuzwa chini ya 50 cents usd. Na value yake inapanda kwa kasi ya mwanga. Mwezi May 2017 iliuzwa kwa TZS 5mln, kufika mwezi August ikauzwa kwa TZS 8mln, baada ya hapo haikushikika....ikapanda mpaka about 45-50mln....na inategemewa kufika milioni 100 soon. Hii currency ni legal kwa nchi nyingi za ulaya na usa. Katika nchi hizo kuna hadi ATM za kutolea na kuweka bitcoin. Labda niweke wazi....hakuna noti au sarafu utakayoishika physically inaitwa btc...isipokuwa ktk atm za btc utatoa hela ya currency ya nchi ile. Sifa kuu zinazofanya bitcoin ikimbiliwe hususani na matajiri wakubwa ni hizi: 1. Untreacable- hakuna benk kuu yeyote duniani inaweza kujua unahela kiasi gani, au umetuma hela au umepokea kiasi gani. 2. Fast transaction- ukitaka kufanya malipo pesa yako haipitii middle man kama benks, nk na huenda moja kwa moja between two end users. Kwa mfano kama unataka kulipia gari nje ya nchi( kuna yard zinakubali btc payments) utatuma hela moja kwa moja kwa ile yard au auction bila kupitia benk na huitaji kufanya currency conversion . 3. Digital- hela zako zipo kwenye simu/kompyuta yako 4. N.k
Kwa baadhi ya makampuni yanayoa huduma za bitcoin hutoa na visa au mastercard kwa malipo mengine ya online au kutoa fedha. Kwa kuhitimisha tu ni kuwa hakuna namna ya kuipinga bitcoin isifanye kazi ndani ya nchi yeyote duniani. Baadhi ya Benk kuu mfano China na India walijaribu kuizuia wakashindwa baadae walianua kutengeneza regulation za kuicontrol ili kwanza kuhakikisha kodi ya hizo serikali zinapatikana kutokana na btc transactions. pili, kuzuia uharifu ambao unaweza kufanyika kupitia btc. Uharifu kama money laundering, drug traffic, human traffiking nk. Kuna baadhi ya nchi kama naweza kuzikumbuka ipo Botswana na South Afrika nao wametengeneza regulations. Pia nilipata kusikia kuhusu kati ya kenya au uganda nao.wapo katika mpango huo. Hitimisho ya mwisho ni kuwa: kama mna kumbukumbu nzuri, telegram ililiua shirika la posta, baadae simu za mobitel na voda za mwanzo ziliua kabisa posta na telegram, baadae smartphone zimeiangamiza kabisa hizo old tecknolojies. Mnakumbuka jinsi mabenk yalivyokuwa yanapigia kelele mpesa, na sasa imeruhusiwa kuoperate kama benk. Kwa kufanya hivyo imepunguza wateja na savings za benk, sasa mabenk na mpesa wana threat mpya ya bitcoin. Ndo maana mabenk ya TZ yakaungana kulaani na kuwatahadhalisha watu kuhusu kuwekeza katika bitcoin na kuita majina ya utapeli na mengine. Na BOT nao walifanya hivyo hivyo....ni ukweli mtupu kuwa bitcoin ni tishio kubwa la mabenk duniani kwa sasa. Hata mimi kama ningekuwa na ukwasi wa kutosha ningeuweka huko. Hebu waza. Ukiweka 100,000 benk baada ya mwezi itakatwa service charge, ukitoa utakatwa withdrw chajis, hela haiobgezeki thamani...Tofauti sana na bitcoin. Ukiacha hela yako kwa muda furani utaikuta bitcoin zako zipo vile vile, isipokuwa utakuta imeongezeka thamani dhidi ya coins km dola, yen nk..... Ombi kwa serikali zetu za Afrika, wakati wazungu wanakimbia na sisi tukimbizane nao, isije tukajisahau wakati huo hakuna tena kitu kinaitwa benk ulaya kwa matumiz ya btc harafu tunaaza kujikokota tukiwa still underdeveloped interms of btc technology....tukimbizane nao. Nimefarijika sana mwezi uliopita nimesikia nchi moja ya Afrika inaanzisha blockchain
. Pia kuna nchi ya ulaya inampango wa kutumia blockchain kwenye uchaguzi mkuu....wake up Africa